Ukitolewa out ni halali kwenda na shoga yako? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukitolewa out ni halali kwenda na shoga yako?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Katikomile, May 5, 2010.

 1. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Tatizo sugu katika hii mitoko ni baadhi ya wanawake kwenda na ‘kampani’ yao/zao. Utakuta mtu kapewa mwaliko, anaamua kubebana na mashoga zake watatu au wanne, eti wanamsindikiza! Hata kama ni mmoja, kwani uliambiwa uende na mtu? Sasa soma mtiririko ufuatao, ujifunze kitu kama una tabia hiyo au ulikuwa na mpango wa kufanya hivyo.

  INAKUPUNGUZIA SIFA
  Kama ulikuwa ni mpenzi wa jamaa huyo, hapa utakuwa umeshapunguza credit za kuwa mke. Kwa vyovyote vile, hata kama hatakuambia, atabaki na donge moyoni. Atakuwa na maswali mengi sana, lakini hatakuwa na majibu na muda wote atakuwa amejenga tabasamu la kutengeneza.
  Amka. Kama una tabia hii na una mpango na mshkaji acha, other ways uwe na nia ya kumchuna na kuanza zako, lakini kama unataka kuingia kwenye ndoa, utampoteza!

  ATAJUA UNAMCHUNA!
  Maswali kichwani mwake yatakuwa mlima, lakini kubwa litakalotawala ni ile hali ya kuhisi kabisa kwamba unafanya buzi. Yes...unamfanya buzi, kwasababu kama ni kinyume chake, kwanini uongozane na kampani? Kama alikuwa na nia wewe, haraka atageuka, ana haja gani ya kuwa na mwanamke mfujaji wa fedha?

  UTAMWOGOPESHA...
  Kama ndiyo anakutaka na wewe kwa mara ya kwanza, utamwogopesha kuongea chochote. Kwanza atajua umekuja na watu ili asiweze kuongea, lakini pia ataogopa kukualika katika mtoko mwingine, maana utakuwa umejipotezea sifa ya ustaarabu.

  BAJETI YAKE VIPI?
  Vyovyote itavyokuwa, utakuwa hujui ana bajeti kiasi kwa ajili ya siku hiyo, lakini kubwa zaidi hufahamu ana kiasi gani kwenye pochi yake siku hiyo. Hata kama ungekuwa wewe, kwa hakika usingeona bajeti yako ikiharibiwa bila mpangilio.
  Halafu utafiti usio rasmi unaonyesha kwamba, marafiki wanaobebwa katika mitoko isiyo yao, huwa wanakula na kunywa vinywaji vya bei ghali zaidi hata mualikwa. Hili ni tatizo, kama hana pesa za kutosha na network ya ATM haisomi itakuwaje?

  UNAWEZA KUUMBUKA
  Iwe unamkomoa, hujui au ni bahati mbaya, lakini vipi kama utakutana na mwanaume ‘fyatu’ kidogo, ambaye hajali. Unajua kitakachotokea, anaweza akalipa bili yako na yake, halafu akasema hao wengine hawakuwa kwenye bajeti yake, kwa maana hiyo ulipe wewe au wajilipie wenyewe! Aibu kiasi gani?
  Mkatili zaidi, anaweza akawaacha mkaagiza sana, bili ikishakuwa kubwa anaenda kaunta na kulipa vyake tu, halafu anamwagiza aje awadai. Akija kwenu anajifanya anakwenda msalani, kumbe kawaachia msala, itakuwaje? Ukute na wewe kwenye pochi yako una elfu kumi tu, halafu bili 45,700, utaumbuka!

  UMENIPATA?
  Umeona eeh! Nadhani ni vizuri kama una haka katabia ukabadilika, kwani si njema hasa kwa mwanaume ambaye unatarajia awe wako. Ukipewa ofa ya mtoko, nenda peke yako.
  Ukweli ni kwamba, ukibebana na wenzako unaibua hisia tofauti ambayo inaweza kukupotezea pointi za kuwa mwenzi mwema hapo baadaye.


  Source: Globalpublisherstz.com
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  The source below does not go well with my "online-thinking"!

   
 3. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  thread nyingine bwana, michosho mitupu.
   
 4. M

  Mundu JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Baba Enock, assume the source is the thread starter; do you like the content? kwa mtazamo wangu, hii maneno ina ukweli mkubwa ndani yake... Vinginevyo mtu atoe taarifa in advance kwamba anakuja na Company.
   
 5. Madabwada

  Madabwada JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2010
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 537
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  it is a copy and paste from the original english version ... GP should acknowledge the source!!
   
 6. T

  Tall JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  1.Mwanamme unapokuwa na appointment na dearheart wako ni busara ukawa mifukoni kwako upo safi. Draw angalau vilaki viwili(sh 200,000) viwe standby
  na ka ATM kadi kako kasicheze mbali,kawe kwenye mfuko wa mbele wa shati. Mpaka hapo na aje tu
  2.Kabla hajaja na mashosti wake lazima amekujudge uwezo wako ukoje.
  3.Kama nina elufu kumi tu mfukoni? yanini kumsumbua mrembo wa watu?
  4.Hawa watu hupenda UHURU, matanuzi na kuwakoga zaidi wanawake wenzao kuwa ''mimi mr wangu ANAZO'',
  5.Kuna wanawake ambo kama wanamikataba vile?Yeye atatolewa na shoga yake akiwa na bwana wake nae mpenzio siku ukimtoa OUT
  lazima alipe fadhila. SASA? unafikiri mpenzi wako kama alipotolewa out alikunywa valuu 6,konyagi chupa 3,kuku wanne...unategemea rafiki yake nae leo atafanya nini?LAZIMA WAKUNYWE.NA KWA KWELI KUBALI UNYWEWE,EEEH SI UMEPENDA?
  6.Kwa hiyo mzee mwenzangu mimi mwanamme mwenzako, nakushauri wala huna haja ya kulaumu.NDIO UDUME HUO.Acha aje nao mashoga kibao,kwanza utajifunza mambo mengi sana yanayomhusu mpenzi wako hasa bia inapoanza kufanya kazi vichwani mwao,kwa vile SIO WOTE WANAOMPENDA KIUKWELI mpenzi wako
  7.Hapa mimi naona faida tu kuliko hasara.
  8.Kama hujajiandaa CANCELL appointment.Kwani unalazimishwa?
  9.Akina dada wengine starehe haikamiliki hadi awepo shoga yake fulani.WEWE hutaki.Acha amlete tu,na hata kama wanamazungumzo yao acha waendelee,mimi nitakuwa na gazeti langu nailisomaaaaaa.nikimaliza story zote narudia tena,eeeh kumbe nifanyaje?
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Mmmh, tunazungumzia Tz hii ambayo serikali inasema haiwezi kumlipa mfanyakazi gross salary ya TZS 315,000 kwa mwezi au..?
   
 8. T

  Tall JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  UNAFIKIRI RAHA UTAIFANYA UKISHAKUFA?RAHA NI HAPAHAPA. HALAFU? Lazma utumie zote? hiyo inaitwa emergency.Hapo ukiwa na kiasi hicho akili imetulia.Waweza tumia 40, 30, 70......hata zaidi ya hapo ikibidi.
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  labda Tanzania ya wajasiriamali
  Mshahara wenyewe hauenei kwenye wallet hivyo vi laki mbili vinatoka wapi??
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Tall !!
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Sawa mkuu nimekusoma:rolleyez:!
   
 12. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Mundu, haya mamb inanikumbusha tukio moja tuliwahi kufanya na jamaa yangu mmoja moshi mjini pale wakati niko "A" level natoka likizo ndio najianda kurudi nyumbani. Tuliwatokea wadada fulani kule Dar es Salaam street kwa wale wenyeji wa moshi watakuwa wanaifahamu hiyo mitaa.Tukiwa na hamu za kukaa boarding siku nyingi hatujanoa mashine. Tukapanga nao waje nao mahali ili tunywe na kuongea wakati tukipanga mambo. Huwezi kuamini Ilikuja group kama ya mtu 5 eti kila mmoja ana mdogo wake amemsindikiza na mwigine rafiki yao.. Habari nilizokuja kupata baadae kwa mabinti waliacha viatu na wengine khanga. Tulipoona ankara inaelekea kuwa kubwa kila mmoja kwa wakati wake unaaga unaenda ****** unaruka jumla kuja kutahamaki wamebaki peke yao na mangi anataka pesa yake.....Kwa kweli haka katabia hata mimi sikapendi eti demu unamtoa out naye analeta na wenzake noma sana.
   
 13. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndio maana watanzania walio wengi wezi kazi ya kuhusudu ngono na mitoko
   
 14. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  iyo picha tu ya mtoa mada imenifanya nifunga haraka na kuichukia mada chapchap. humu ndani watu wengine wana avatar ambazo hauwezi kuziangalia mara mbili ama sivyo utaweweseka usiku watakukuta nyumba ya tatu unakimbia haujui hata unakoenda.
   
Loading...