Ukitaka kula basi kubali nawe uliwe, hili halikwepeki

JABALI LA KARNE

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
2,513
2,000
Ukitaka kula, sharti uliwe.....

Nimemkumbuka JK, uongozi wake ulikuwa na kashfa za kifisadi ila uliweza kutengeneza fedha, sehemu za fedha zilifisadiwa sana, ila nchi bado ilikuwa na fedha za kuendesha uchumi, kulipa mishahara na kuiongeza, mikopo kwa wahitimu wa sekondari hata walipogoma iliongezwa, mabenki yalikuwa yana uwezo mkubwa wa kukopesha, wananchi walikuwa wana uwezo wa kukopa na kurejesha. Serekali ilifahamu namna ya kutengeneza fedha kutoka wa watu wake, baadhi ya watu walifahamu namna ya kufisadi fedha za serikali, mambo yalikuwa bam bam kibiashara. Mwendo wa kula uliwe. Fedha zilitengenezwa, ufisafi ukaongezeka halafu fedha zikatengenezwa zaidi.

Leo JK nimemkumbuka baada ya kukutana na swali hili kutoka kwa mtaalam wa management internal control

Aliuliza, "Sasa ungependa nikuletee mtumishi wa aina gani? Mwaminifu asiyejua namna ya kutengeneza faida kubwa au mtumishi mjanja anayejua kutengeneza faida kubwa ila atakwapua sehemu ya faida kwa ajili yake kiujanja ujanja? Kabla hujajibu nikukumbushe tu kuwa hakuna mwaminifu anayeweza kukutengenezea faida kubwa unless unamlipa vizuri sana, malipo ambayo gharama zake ni kubwa kuliko hiyo sehemu ya faida ambayo angeichukua kiujanja ujanja, Mtumishi mwenye uwezo wa kukutengenezea fedha nyingi ana gharama na si mjinga wala mwoga ila unaweza pia kuchukua mwaminifu, mwoga asiye na skills za kukuza faida yako ukamlipa mshahara mdogo sana na hao ndio wapo wengi, wahindi wanawatumia sana kwenye taasisi zao level za chini, level za juu wanatumia wahindi wenzao ambao ni wajanja. Tumia weekend hii kufikiri kisha nipe jibu ili nikamilishe kazi yako".

Maamuzi ni anipe mjanja, anitengenezee faida mm nitaishi nae kwa akili huku nikiziba mianya asijisahau, yeye achukue pale nisipoweza kupaziba. By the way anachukua sehemu ndogo ya alichonitengenezea, halafu atakuwa na sababu za kupambana kuleta kikubwa ili apate kikubwa zaidi.
 

XII Tz

JF-Expert Member
Aug 16, 2020
1,895
2,000
Aaah kuna Uzi nilikua nacomment mkuu asa nikajikuta mambo yameingiliana .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom