Ukistaajabu ya Ndugai, utayaona ya TUCTA

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
502
938
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) limeyataka makundi ya wanasiasa kutowatumia wao kama njia ya kujitafutia umaarufu kwa kuzungumzia masuala yao na badala yake wawaachie viongozi wa vyama hivyo kwa sababu wanajitosheleza.

Pia shirikisho hilo limesema litaendelea kuiunga mkono na kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano pamoja na rais wake Dkt. John Magufuli na kwamba watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya ajira zao.

Hayo yamesemwa leo, Januari 7, 2019 na Katibu Mkuu wa TUCTA, Yahya Msigwa katika hotuba yake aliyoitoa kwa wafanyakazi baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kupokea maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi.

Watumishi wa taasisi mbalimbali leo wameandamana jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Squarekwa lengo la kumpongeza Rais Dkt. Magufuli kwa uamuzi wake kufuta kikotoo kipya cha mafao ya wafanyakazi kilichopendekezwa katika kanuni za sheria ya Mifuko ya jamii.

Katibu huyo wa TUCTA amesema mara nyingine makundi ya wanasiasa yamekuwa yakisema maneno ambayo wao hawajayasema jambo ambalo limekuwa likiwachonganisha na wadau wao wakiwemo wanachama pamoja na Serikali.

”Wafanyakazi wanaona fahari kwa sababu Rais Dkt. Magufuli anasikiliza kero mbalimbali zinazowakabili na kuzitatua kwa wakati. Aliposema atafufua Shirika la Ndege Tanzanzia amelifufua na sasa tuna ndege saba pamoja na ujenzi wa miradi mkubwa ya umeme, barabara ambayo yote inaenda kutengeneza ajira.”

Hata hivyo, ameiomba Serikali ifanye uchunguzi kwenye miradi inayotekelezwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa sababu hawana uhakika kama miradi hiyo imerejesha fedha. Pia ameiomba Serikali iongeze mishahara kwa watumishi wa umma.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema Serikali ipo tayari wakati wote kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuboresha mishahara na maslahi yao. “Wito wa Serikali ni kuwa wafanyakazi watekeleze majukumu yao kwa uadilifu,weledi na kujituma ikiwa ndio chachu ya kufikia malengo na ustawi wa nchi yetu.”

Muungwana Blog

Sent using Jamii Forums mobile app
 
alipoingia tu madarakani hao ndio watu wa kwanza kabisa kuwakamata. wapo ambao watto wao wanasomeshwa ulaua hapo! huyo ni mmoja wapo
 
Nina wasiwasi na uwezo wake wa kufikiria huyu katibu wa TUCTA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Dhambi kubwa sana kuwasaliti Wafanyakazi wazalendo maskini wanaolipwa Mshahara usiofikia sh. laki NNE kwa mwezi mzima na kuwashangilia na kuwapigania na kuwasemea na kuwapongeza na kuwasujudia Wale wanaolipwa mamilioni ya fedha kwa mwezi huku hazina zikiwa mikononi mwao.

Hata mkoloni aliyeanzisha siku ya wafanyakazi hakuwa na roho ya ubinafsi kiasi hicho.
Bila shaka Ngozi nyeusi inahusiana na aina fulani ya laana kama wanavyotuona wenzetu weupe!!

Kwani wangekaa kimya wangepungukiwa nini ?
Nani asiyejua jinsi wapinzani walivyopambana na kikokotoo.

Historia haijawahi kuwaenzi na kuwakumbuka wasaliti kwa mema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu kama Hawa wanafaa kunyongwa hadharani kabisaaa walikuwa kimyaa baada tuuu ya watu kupigana kwa kupaza sauti zao leo kusifia ndege mafiii
 
Huyu Msigwa ni pandikizi la CCM!
Unaishangilia serikali ambayo haijaongeza mshahara wa wafanyakazi wake kwa miaka minne sasa?
Huyu jamaa ni mwehu kabisa!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom