Ukistaajabu ya musa...!

Jidu

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
1,232
754
Na Richard Bukos
MREMBO mwenye mvuto wa kimahaba, Evonia William, juzi Jumatano alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive, Dar es Salaam kwa kosa la kufanya biashara haramu ya ukahaba.
Awali, mrembo huyo aliwahi kutupa karata yake kwenye ulingo wa filamu za Kibongo kwa kushiriki sinema tatu (scene chache) lakini ‘akalamba galasha’.

KUTOKA MAHAKAMANI
Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi alimsomea Evonia shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi, William Mutaki na kumwambia kuwa kosa alilokutwa nalo ni la kukaa eneo la wazi na kufanya ukahaba.
Mwendesha mashitaka huyo aliiambia mahakama kuwa, Januari 17, mwaka huu, saa 2:00 usiku, mshitakiwa huyo alinaswa eneo la Buguruni karibu na Baa ya Kimboka akifanya kosa hilo.

AKANA SHITAKA
Evonia alikana shitaka hilo na kumwambia hakimu kuwa alikamatwa eneo hilo kwa kosa la kupigana na changudoa aliyekuwa akijiuza, lakini yeye hakuwa na lengo la kufanya biashara hiyo.
Baada ya mrembo huyo kukana shitaka, mheshimiwa hakimu alimwambia kuwa, dhamana ipo wazi, lakini alikosa mdhamini hivyo alipelekwa rumande.

AMWANGUSHIA LAWAMA BABA YAKE
Mshitakiwa huyo akiwa mahakamani hapo, alimlalamikia baba yake mzazi aliyemtaja kwa jina la William Molo, kuwa ndiye chanzo cha yeye kuteseka na kuzurura hovyo.
Alisema, baba yake pamoja na uwezo wake mkubwa kifedha, alikataa kumsomesha, ndiyo sababu anahangaika mitaani.

“Kama baba yangu angenisomesha, nisingekuwa hivi. Ningekuwa na maisha mazuri kama mabinti wengine. Nimembembeleza sana anisomeshe lakini hataki. Akitokea msamaria yeyote kunisomesha au hata kufanya kazi za ndani, nipo tayari kutulia,” alisema msichana huyo huku akiangua kilio.
Kesi hiyo itatajwa tena Januari 31, mwaka huu mahakamani hapo huku Evonia akiendelea kula msoto rumande.
 
Mimh naona ya Filauni....anataka kusoma au kazi za ndani,bado hajaamua anataka nini...lakini pia uchangudoa ni kazi kama kazi zingine.
 
Hatujawa na sheria hii bado (ndio maana sijaona nukuu ya kifungu cha sheria, labda kosa la uzururaji......................proving ya biashara ya ngono mh!!!!
Na Richard Bukos
MREMBO mwenye mvuto wa kimahaba, Evonia William, juzi Jumatano alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive, Dar es Salaam kwa kosa la kufanya biashara haramu ya ukahaba.
Awali, mrembo huyo aliwahi kutupa karata yake kwenye ulingo wa filamu za Kibongo kwa kushiriki sinema tatu (scene chache) lakini ‘akalamba galasha'.

KUTOKA MAHAKAMANI
Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi alimsomea Evonia shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi, William Mutaki na kumwambia kuwa kosa alilokutwa nalo ni la kukaa eneo la wazi na kufanya ukahaba.
Mwendesha mashitaka huyo aliiambia mahakama kuwa, Januari 17, mwaka huu, saa 2:00 usiku, mshitakiwa huyo alinaswa eneo la Buguruni karibu na Baa ya Kimboka akifanya kosa hilo.

AKANA SHITAKA
Evonia alikana shitaka hilo na kumwambia hakimu kuwa alikamatwa eneo hilo kwa kosa la kupigana na changudoa aliyekuwa akijiuza, lakini yeye hakuwa na lengo la kufanya biashara hiyo.
Baada ya mrembo huyo kukana shitaka, mheshimiwa hakimu alimwambia kuwa, dhamana ipo wazi, lakini alikosa mdhamini hivyo alipelekwa rumande.

AMWANGUSHIA LAWAMA BABA YAKE
Mshitakiwa huyo akiwa mahakamani hapo, alimlalamikia baba yake mzazi aliyemtaja kwa jina la William Molo, kuwa ndiye chanzo cha yeye kuteseka na kuzurura hovyo.
Alisema, baba yake pamoja na uwezo wake mkubwa kifedha, alikataa kumsomesha, ndiyo sababu anahangaika mitaani.

"Kama baba yangu angenisomesha, nisingekuwa hivi. Ningekuwa na maisha mazuri kama mabinti wengine. Nimembembeleza sana anisomeshe lakini hataki. Akitokea msamaria yeyote kunisomesha au hata kufanya kazi za ndani, nipo tayari kutulia," alisema msichana huyo huku akiangua kilio.
Kesi hiyo itatajwa tena Januari 31, mwaka huu mahakamani hapo huku Evonia akiendelea kula msoto rumande.
 
Mkuu wewe hutaki house girl? Na wengine wenye kuhitaji haya,mfanyakazi za ndani huyo.
 
Hapa kwa kweli ngoja tustaajabu ya huyu tuachane na ya mussa kabisa
 
kama ni kweli alitaka kusoma halafu dingi hakum support,atakuwa amefanya kitu mbaya sana aise
sidhani kama kuna mama watoto ataruhusu mumewe aajiri hii kitu,maana ni balaa
 
AMWANGUSHIA LAWAMA BABA YAKE
Mshitakiwa huyo akiwa mahakamani hapo, alimlalamikia baba yake mzazi aliyemtaja kwa jina la William Molo, kuwa ndiye chanzo cha yeye kuteseka na kuzurura hovyo. Alisema, baba yake pamoja na uwezo wake mkubwa kifedha, alikataa kumsomesha, ndiyo sababu anahangaika mitaani.

"Kama baba yangu angenisomesha, nisingekuwa hivi. Ningekuwa na maisha mazuri kama mabinti wengine. Nimembembeleza sana anisomeshe lakini hataki. Akitokea msamaria yeyote kunisomesha au hata kufanya kazi za ndani, nipo tayari kutulia," alisema msichana huyo huku akiangua kilio.
Kesi hiyo itatajwa tena Januari 31, mwaka huu mahakamani hapo huku Evonia akiendelea kula msoto rumande.

Anakana mashtaka at the same time anakubali bila kujijua.
 
hili janga la taifa sipati picha for the coming five years
production ya shule za kata na vyuo vya kata ni hatari hakika!!!!!!!!!!!!
 
kUdadadeki ngoja nikaongee na mama Narubongo tumpatie binti kazi za ndani maana kazi za nyumbani zimemuelemea sana siku hizi. mshahara 100,000/= na atakaa nyumbani
 
Sioni kosa lake. Iwapo ni changudoa hakuna anayelazimishwa kumfuata. Ni maelewano. Iwapo ukahaba siyo ajira basi jamii inabidi ilaumiwe kwa kutompa uhakika wa maisha. Kumbuka huyo anabeba tatizo la vijana wengi wa kike na wakiume. Mfumo mbovu wa Taifa letu hasa katika kugawanya mapato ya mali za Taifa. Kuna ambao wanajilibikizia na kisha kutunga visheria vya kipuuzi. Ni vyema kuwa changudoa kuliko kuwa jambazi. Huyu anatry to make ends meet. She has got to survive or die. It's a matter of survival.
 
Ni aibu kuna wababa hadi leo hawasomeshi watoto wao wa kike na wana uwezo wa kufanya hivyo...aende TGNP

Aluta continua
 
Mpumbavu tu; alikataa shule kwa kujiona mrembo na kufuata mabwana sasa amechacha anadai baba yake alikataa kumsomesha, hajasema alikula ada mara ngapi.
 
Back
Top Bottom