Ukistaajabu ya Jenista Mhagama utayaona ya Ombeni Sefue NSSF

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,922
13,494
Pamoja na kwamba meengi yamezungumzwa kuhusu Shirika La Hifadhi ya jamii la taifa Nssf...Bado Jamii imezid kubakia njia panda na kukosa majibu yenye tija ya kuhusu nin hasa kinachoendelea na kilichojificha Nssf.

Hivi Punde ilizuka hali ya kustaajabisha baada ya Waziri wa kazi na Ajira Mh Jenista Mhagama kufanya uteuzi wa kukurupuka wa mtu wa kukaimu nafasi ya mkurugenz mkuu wa Nssf Nafasi ambayo imeachwa wazi mara baada ya Mkurugenzi Alieacha Mafanikio yasiyo ya Kifani Nssf Dr Ramadhan Dau kuteuliwa kuwa balozi na Mh Rais Dr John Magufuli.

Swali liliobakia hiv sasa baada ya kutokea kwa kioja cha Mh Wazir Jenista Mhagama ni hili la Ombeni Sefue...

Balozi Ombeni Sefue amediriki kinyemela kuvunja bodi ya wakurugenz ya Nssf na kumuondoa hadi Mwenyekiti wa bodi hiyo kinyemela pasi na kuutarifu hata umma wa watanzania...!

Nan kampa mamlaka sefue ya kutengua uteuzi wa Mh Rais Hilo ni moja..

Pili maamuz hayo anayafanya kwa interest ya nani...who is behind who?...

Tatu kikawaida suala la kuvunja bodi ya shirika kubwa la umma kama Nssf siyo dogo ni lazima wananchi kama stake holders wajulishwe na wafahamishwe suala hilo..sasa usiri huo uliopo katika hili sakata zima la Nssf umebeba jambo gani?...

Na Je Mh Rais Usalama wa Taifa wanafanya kazi yao ipasavyo katika kumshauri kwa undani katika masuala kama haya?...

Naomba kuwasilisha.
 
Kipi hasa kinachoendelea baina ya Ombeni Sefue na Shitindi ambacho umma wa watanzania unafichwa?
 
Kwakweli kuna mambo yasiyo ya kawaida, kama yanayosemwa ni kweli. Bw. Big Show, naomba ututajie jina la aliyekuwa M/kiti wa bodi ya nssf na majina japo matatu ya walikota wajumbe wa bodi ili tuwafahamu japo kwa ufupi.
 
Ni kawaida ya serikali ya awamu ya tano..Unakumbuka Prof Mbarawa aliteuliwa wizara ya maji ambayo sio mambo ya muungano.? Baada ya kushtuliwa akatengua..Hii serikali ni mwendo wa mizuka tu mkuu
 
Balozi Ombeni Sefue amediriki kinyemela kuvunja bodi ya wakurugenz ya Nssf na kumuondoa hadi Mwenyekiti wa bodi hiyo kinyemela pasi na kuutarifu hata umma wa watanzania...!

Naomba kuwasilisha.

Tupe uthibitisho wa hili kwanza ndo tuendelee. Tusijekuta tunajadili kitu kisichokuwepo.
 
Ni kawaida ya serikali ya awamu ya tano..Unakumbuka Prof Mbarawa aliteuliwa wizara ya maji ambayo sio mambo ya muungano.? Baada ya kushtuliwa akatengua..Hii serikali ni mwendo wa mizuka tu mkuu

Kwa kweli mimi namuonea huruma sana Mh Rais Dr John Pombe..ana nia njema sana na nchi hii lakin watu kama sefue na shitindi awaangalie vizur washaanza kumtia doa katika utawala wake.

Anajinasibu kutumbua majipu ili hali majipu anayo ndan mle mle ikulu...

Very sad...
 
Kuna fitna kubwa inayoendelea chini kwa chini nssf! anyway yana mwisho haya
 
Tupe uthibitisho wa hili kwanza ndo tuendelee. Tusijekuta tunajadili kitu kisichokuwepo.

Mkuu hivyo hata wewe huna taarifa kuwa balozi ombeni sefue na shitindi kinyemela wamevunja bodi ya Nssf na kumwondoa mwenyekiti wa bodi hiyo ambae ni mteule wa rais kinyemela pia tena hata kuujuza umma?...

Hilo ndilo lilivyo mkuu...

Amin hiki ninachokuambia.
 
Sio kukurupuka hii ni Serikali ya ,,Moto Chini,, mlizoea ile ya kubebwa na kubembelezwa hapa ,,KAZI TU,, Ukiteuliwa saa saba mchana baadae saa mbili Usiku ukaonekana wew ni JIPU,, tunatengua tu uteuzi,, kaeni kimya akili itawakaa sawa siku za mbele wakati Sukari imeshuka na kuwa kilo Tsh.500/=
 
Mkuu hivyo hata wewe huna taarifa kuwa balozi ombeni sefue na shitindi kinyemela wamevunja bodi ya Nssf na kumwondoa mwenyekiti wa bodi hiyo ambae ni mteule wa rais kinyemela pia tena hata kuujuza umma?...

Hilo ndilo lilivyo mkuu...

Amin hiki ninachokuambia.
Sina taarifa mkuu. Nisingeomba uthibitisho. Wapi naupata? Maana umebonyea kinamna kwa nlichorequest
 
Hakuna nchi Duniani iliyowahi kupata mafanikio kiuchumi kwa kufanya maamuzi ya kukurupuka kama hii ya kwetu...

MTU anateuliwa baada ya wiki moja uteuzi unatenguliwa.,
mtu una msimamisha kazi mwezi halafu mwezi ujao unamrudisha kazini.

Binafsi sioni kitu ambacho serikali hii inajaribu kukifanya kwakweli.
 
Mimi nadhani tatizo lililopo kuna watu wanameza Mada za mwanaJF aitwaye AbasMzeEgyptian na kuanza kujenga hoja bila kuchanganua ukweli wake.

AbasMzeEgyptian amekuwa akileta mfululizo wa mada kuhusu NSSF ambazo ukizichanganua kwa umakini utagundua zina uwongo mwingi na ukweli kiduchu.

Mwenye Mamlaka ya kuwateua wajumbe wa bodi ndiye mwenye Mamlaka ya kuwaondoa. Kama Ombeni Sefue ana mamlaka ya kuwateua wajumbe wa bodi, hakuna cha ajabu kama ataamua kuwaondoa lakini kama hana Mamlaka ya kuwateua, itakuwa ni ujinga kuanza kujadili kama atakuwa na uwezo kimadaraka wa kuvunja achilia mbali kuivunja.

Sijawahi kusikia bodi kuvunjwa kinyemela wakati iliundwa kisheria. Kama iliundwa kisheria na itavunjwa kisheria.
 
Mtaongea sana ila majipu lazima yatumbuliwe. Yalilelewa sana na awamu iliyopita.

Watumbue Magu wetu gooooo....

NSSF lazima itumbuliwe ilishafanywa kama sebuleni kwa mtu. Mtaisoma namba na bado...
 
Kwa kawaida Mwenyekiti wa bodi katika mashirika ya umma ni Presidential Nominee.

Na wajumbe wa bodi huteuliwa na waziri mwenye dhamana husika...

Hata katika kutengua Uteuzi hivyo hivyo.

Ombeni Sefue hana mamlaka ya kumwondoa mwenyekiti wa bodi na kuivunja.
Mimi nadhani tatizo lililopo kuna watu wanameza Mada za mwanaJF aitwaye AbasMzeEgyptian na kuanza kujenga hoja bila kuchanganua ukweli wake.

AbasMzeEgyptian amekuwa akileta mfululizo wa mada kuhusu NSSF ambazo ukizichanganua kwa umakini utagundua zina uwongo mwingi na ukweli kiduchu.

Mwenye Mamlaka ya kuwateua wajumbe wa bodi ndiye mwenye Mamlaka ya kuwaondoa. Kama Ombeni Sefue ana mamlaka ya kuwateua wajumbe wa bodi, hakuna cha ajabu kama ataamua kuwaondoa lakini kama hana Mamlaka ya kuwateua, itakuwa ni ujinga kuanza kujadili kama atakuwa na uwezo kimadaraka wa kuvunja achilia mbali kuivunja.

Sijawahi kusikia bodi kuvunjwa kinyemela wakati iliundwa kisheria. Kama iliundwa kisheria na itavunjwa kisheria.
 
Mkuu hivyo hata wewe huna taarifa kuwa balozi ombeni sefue na shitindi kinyemela wamevunja bodi ya Nssf na kumwondoa mwenyekiti wa bodi hiyo ambae ni mteule wa rais kinyemela pia tena hata kuujuza umma?...

Hilo ndilo lilivyo mkuu...

Amin hiki ninachokuambia.
Tufanye Kingmairo hana taarifa ila mimi sina taarifa, naomba unirushiepo some facts ili tuanze kujadili.
 
Back
Top Bottom