Ukistaajabu ya Escrow utaona ya Mwakyembe

Ukistaajabu ya Escrow utaona ya Mwakyembe

Penye kustahili sifa wacha mtu apewe sifa,pamoja na yote Mwakyembe kafanya kazi kwa uadilifu na dhamira kwenye wizara ya uchukuzi,wanofurahia kuondoka kwa Mwakyembe wizara ya uchukuzi hasa wale wa TPA nadiriki kusema ni wezi na wala rushwa waliokubuhu,kabla ya Mwakyembe pale bandarini palikuwa kama pango la wala rushwa,kwa msafirishaji yoyote wa mizigo hili analifahamu na sio siri,na kwa hilo Mwakyembe alijiwekea maadui wengi akiwemo yule wa Home Shopping Centre na balozi wetu mdogo wa Guazhong,yale makonteina yao yaliyokuwa yanapita bure ikawa mwisho.Kilichonishangaza ni uamuzi wa JK kumchomoa mtu ambaye alikuwa mchapakazi kwenye wizara nyeti na kumleta Mr porojo,halafu matokeo yake mapato yanashuka chini tunaanza kumtafuta mchawi,sana sana mi ningekuwa ndio mwenye dhamana ningempeleka wizara ya Nishati na Madini
 
Umenena,...full shangweee au ndio njia ya kupata kura za maselaaa hukoo
 
Hamjamjua sitta subiri moto wake mtauona atakavyotikisa kwa kishindo.
 
Yes, kilichobakia Bandarini ni kukomba mboga tu hadi kufikia October kitakuwa kimeelewekamo.
 
Wewe Umtetumwa kuandika upuuzi humu. tunataka mawaziri km HM wachapakazi na sio wachapa usingizi na kusoma hotuba na kukata utepe tu.
Mwakyembe aliona udhaifu wa wasaidizi wake ndio maana alikuwa akitoka yeye mwenyewe kwenda kuweka mambo sawa.
Nchi hii tangu kuuawa kwa Sokoine imelaanika na kila mchapa kazi ataonekana mbaya tu. Bora mtu kama huyu hata kama anakula lakini kinaonekana kitu anachokifanya .
Lakini kila jambo lina ukomo wake hivyo hata ufisadi utakuja patiwa dawa tu.
 
Mimi binafsi namkubali sana Mwakyembe, huyu jamaa alikuwa mwiba mkali kwa mafisadi pale bandarini. Kwa muda mfupi ameifanya bandari yetu kuaminika kwa watumiaji kutoka nchi jirani waliokuwa wamehamia bandari ya Mombasa. Pia amewezesha mapato ya bandari kuongezeka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwanzo. Chini ya Mwakyembe ikitokea hata taa ya gari la mteja imeibiwa ni lazima bandari au kampuni iliyohusika ilipe mara moja, ama kweli bandari yetu ilianza kuaminika.

Bila shaka sasa wafanyakazi wa bandarini watakuwa wanafuraha isiyo na kifani maana mwenye nyumba sasa ameondoka, kama Sitta asipokuwa makini ni wazi kuwa watu wataikimbia tena hiyo bandari kwa kuwa bandari yetu imejaa mchwa wa kutosha. Ukiagiza gari utakuwa huna uhakika kama utaipata ikiwa na taa zake kama. Pia ni vigumu kuwa na uhakika kama kontena lako kama litafika salama

Hakuna mtelemko kwa sitta mwenyewe utaona kivumbi chake sitta harembi wala hakurupuka matokeo makubwa sasa utayaona mapema.
 
Mimi binafsi namkubali sana Mwakyembe, huyu jamaa alikuwa mwiba mkali kwa mafisadi pale bandarini. Kwa muda mfupi ameifanya bandari yetu kuaminika kwa watumiaji kutoka nchi jirani waliokuwa wamehamia bandari ya Mombasa. Pia amewezesha mapato ya bandari kuongezeka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwanzo. Chini ya Mwakyembe ikitokea hata taa ya gari la mteja imeibiwa ni lazima bandari au kampuni iliyohusika ilipe mara moja, ama kweli bandari yetu ilianza kuaminika.

Bila shaka sasa wafanyakazi wa bandarini watakuwa wanafuraha isiyo na kifani maana mwenye nyumba sasa ameondoka, kama Sitta asipokuwa makini ni wazi kuwa watu wataikimbia tena hiyo bandari kwa kuwa bandari yetu imejaa mchwa wa kutosha. Ukiagiza gari utakuwa huna uhakika kama utaipata ikiwa na taa zake kama. Pia ni vigumu kuwa na uhakika kama kontena lako kama litafika salama

Aende tu kawa simamisha kazi watu hawana hatia hapo bandarini watu wana familia zao
 
Haya tunasubiri lala salama, inawezekana mzee sita anasafishiwa njia; bandarini wakae sawa, wataona moto zaidi ya ule wa Mwakyembe.
 
Mimi binafsi namkubali sana Mwakyembe, huyu jamaa alikuwa mwiba mkali kwa mafisadi pale bandarini. Kwa muda mfupi ameifanya bandari yetu kuaminika kwa watumiaji kutoka nchi jirani waliokuwa wamehamia bandari ya Mombasa. Pia amewezesha mapato ya bandari kuongezeka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwanzo. Chini ya Mwakyembe ikitokea hata taa ya gari la mteja imeibiwa ni lazima bandari au kampuni iliyohusika ilipe mara moja, ama kweli bandari yetu ilianza kuaminika.

Bila shaka sasa wafanyakazi wa bandarini watakuwa wanafuraha isiyo na kifani maana mwenye nyumba sasa ameondoka, kama Sitta asipokuwa makini ni wazi kuwa watu wataikimbia tena hiyo bandari kwa kuwa bandari yetu imejaa mchwa wa kutosha. Ukiagiza gari utakuwa huna uhakika kama utaipata ikiwa na taa zake kama. Pia ni vigumu kuwa na uhakika kama kontena lako kama litafika salama

Kwani mzee wa speed and standard nae amekwisha speed zake mbona walikuwa wanamwita mtendaji ama tuseme amefolewa speed
 
Mwakyembe, Sasa umehakikisha kauli yetu kwamba CCM ina wenyewe??!! acha kabisa kugusa maslahi ya wenye nchi. Tatizo lako wewe huwa husikii - haya katutetee huko Afrika mashariki - Kaa mbali ya viwanja vyetu vya ndege, Tuachie Reli yetu, Tukabidhi Bandari yetu.
 
Siyo wafanyakazi wa Bandarini tu wanaofuerahia, hata Mkuu wa nchi naye Furaha tupu pamoja na Mafisadi.

Huyu jamaa alikuwa anakorofisha Channel za watu kwa kuyumbisha madishi yakose mawasiliano.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Aende tu kawa simamisha kazi watu hawana hatia hapo bandarini watu wana familia zao

Wanaotumia bandari yetu wanaweza kukuhakikishia kuwa bandari yetu ilikuwa imeoza. Kama hawana hatia inakuwaje wateje wahamie Mombasa, mimi kuna rafiki yangu alihamua aagize gari kupitia Mombasa
 
Wanaotumia bandari yetu wanaweza kukuhakikishia kuwa bandari yetu ilikuwa imeoza. Kama hawana hatia inakuwaje wateje wahamie Mombasa, mimi kuna rafiki yangu alihamua aagize gari kupitia Mombasa
Kwani ajabu kushushia gari Mombasa? si ni uamuzi tu, mbona wa Mombasa wengine wanapitisha mizigo yao Tanga? Achane kusifia wezi, Harrison ni mwizi tu kama walivyo viongozi wote wa ccm, anajua kucheza na media na nyie kama mazuzu mnafata tu.
 
Hamjamjua sitta subiri moto wake mtauona atakavyotikisa kwa kishindo.

Nimeipenda hiyo Picha ya slaa na mwezake , Nauliza jee huyu ndiye yule mke wake wa ndoa, au ni yule aliyempora .
 
Hivi wafanyakazi wa reli wamelipwa mishahara yao??? Mbona wa tz tunakuwa kama kima vileeee 😱 . Mwakyembe asepe zake, hadi utendaji anatafuta jukwaa
 
Aende tu kawa simamisha kazi watu hawana hatia hapo bandarini watu wana familia zao
.

Wao wanapokuwa wanaiba kwani huwa hawajui kwamba itaathiri familia zao, nchi kama Korea kaskazini na China watu wananyongwa na mama zao wapo....huwezi pinga kuwa kabla ya mwakyembe kuwa bandarini ukiagiza gari eti ukute Redio ama virembeshi vingine vya magari na hakuna aliyekuwa anajali. Mimi naamini time will tell.
 
Watz kweli tumerogwa. Kama hii 'article' inavyotuhumu ni kweli basi tumeliwa! It seems hamna system inayofanya kazi yenyewe bila ya kusubiri kiongozi fulani a-push hiyo ajenda! Mfano mzuri ni rais eti kusubiriwa atoe hukumu ya Escrow..sasa mtu mwenye busara anajiuliza je police, Pccb,mahakama na vyombo vingine vinafanya kazi gani? Je ilikua ni kazi ya bunge kutumia pesa za wavuja-jasho kujadili wizi ?

Swali ni kwanini hakuna system inayojiendesha yenyewe na kujifanyia self-diagnosis? Kwanini tujadili utendaji wa kila siku wakati zipo sheria na taratibu halali ktk sekta/taasisi/kampuni husika ambazo sio ambiguous?? Kama kila tukio basi linatakiwa kufanyiwa mdahalao basi ni wazi tuna matatizo kwenye vichwa vyetu!
 
Binafsi sina sifa ya kuwa hata mjumbe wa serikali ya kitongoji, lakini najua namna ninavyotaka niongozwe. Nakubali Mwakyembe aniongoze. Dr. Mwakyembe ni miongoni mwa watanzania wenzetu wachache ambao wanahesabika walioonyesha kwa vitendo kukerwa na aibu za wazi za taifa hili.

Wasiwasi wangu ni kama Mwakyembe na wenzake hao wako kwenye foleni (lane) sahihi katika kutumia usomi, moyo na uzalendo wao kwa nchi yao katika harakati za kuliondolea aibu taifa. Dk. Mwakyembe mnayo akili ya kutosha kuweza kulikwamua taifa hili kutoka hapo lilipo sasa, wewe na wenzako bila shaka mnajua vilivyo nani ni nani na nani anafanya nini katika kusababisha shida za taifa hili, historia itakuja kuwahukumu kama ninyi wenye upeo mkubwa nchini mkikubali nanyie kuamua mfie uvunguni kwaajili ya kulinda maslahi yenu ya muda mfupi na kuyaacha maslahi mapana ya wajukuu na wapwa zenu. Maana siku za mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke si nyingi, lakini taifa litakuwepo kwa miaka karne kwa karne. Wako wanaotamani kuwaachia wajukuu zao urithi wa mali za wizi wa taifa hili, na wako watu wema wanaotamani kuliachia taifa hili urithi wa japo mti mmoja tu wa kivuli ili watakaokuwepo wajisitiri na jua kali.

Ni heri uwe masikini jasiri anayetembea kifua mbele bila aibu kuliko kuwa tajiri rofa anayenyooshewa vidole vya choli choli kila anapopita.

Hamia foleni ile bana!
 
Back
Top Bottom