Ukistaajabu ya bodi ya mikopo elimu ya juu utayaona ya watumishi

makwagejo

JF-Expert Member
Nov 25, 2019
361
267
Habari zenu watanzania,

Bodi ya mikopo elimu ya juu imekuwa ikifanya uzembe sehemu mbalimbali, unakuta mtumishi amebakiwa na 2.7 milioni linaloonekana kwenye salary slip ukipigiwa hesabu ili ulipe unaambiwa unadaiwa 4.7 huku umeajiliwa baada ya miezi sita wakaanza kukata fedha zao,

Haya umewalipa hiyo fedha na kubaki na chechi yako bado hiyo hela iliyozidi hailipwi ,utasugua nauli kuifatilia mpaka hela ya nauli inazidi kiasi unachodai bodi ya mikopo elimu ya juu,

Ni aibu kubwa miezi miwili hujalipwa fedha yako huku tunajinasibu tunakbizana na uchumi w kati ni uongo mkubwa sana hii nikutaka kufanya dhuruma za wazi kabisa wito wangu serikali ya ccm iache kuupuuza ukweli wa vijana na malalamiko yao

Sisi tunaoitetea ccm tunapobanwa mbavu mtaani unashindwa kuitetea maana ccm inasema kusema kweli daima na fitina mwiko!

Nimwambie mkurugenzi bodi ya mikopo atatumbuliwa muda si mrefu tunazidi kukusanya data za ushahidi wa madudu yake mwisho wa siku ataondolewa mara moja hatuwezi kuwa na watu wanaochelewesha malipo na haki za watu vinginevyo vijana ccm tujiandae kupingwa kwa nguvu na watumishi wa umma,
IMG_20191219_084119_1.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahisi hao jamaa hua wanatoa gawiwo zuri huko serikali maana jana tu nimeshangaa kuona mkuu kule Chato akiwapongeza Jeshi la zimamoto kwa kukusanya bil 73 na akasema kazi yao sio kuzima moto tu bali ni kukusanya na mapato pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bodi ya Mikopo ni majanga kwa wanufaika. Nawahurumia sana ambao wanaendelea kukatwa kitu cha 15% ya basic salary, na pia wale ambao hawajaanza kukatwa.
 
Nahisi hao jamaa hua wanatoa gawiwo zuri huko serikali maana jana tu nimeshangaa kuona mkuu kule Chato akiwapongeza Jeshi la zimamoto kwa kukusanya bil 73 na akasema kazi yao sio kuzima moto tu bali ni kukusanya na mapato pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
kuna fedha huwa hazirudi unapolipa wanakuchelewesha kukuondoa kwenye makato unapoidai huipati ng'o hii ni hovyo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani kuna jamaa deni linapaa kila siku!
Deni la bodi ya mkopo limefika 10,000,000 na hajapata ajira, na ni yatima hana baba wala mama.

Jamani wabunge na wenye mamlaka liangalieni hili maana ni mtihani mkubwa sana.

Kwanini riba iwekwe kubwa sawa na ya taasisi za kifedha wakati inatokewa na taasisi ya kiserikali?

Yani ni majanga kwa kweli


Sent using Jamii Forums mobile app
 
naishukuru heslb kunilipia ada, kateni tu hiyo 15%.

nisimgekuwa na mkopo ningesoma dip ambayo mshahara wake ni sawa na nikitoa makato ya bodi. haina shida asanteni bodi
 
Ujinga mwingine wa bodi ni pale Wanapokukata hela bt kwenye salary slip haipungui. Kwa mfano, Mwezi may 2019, walikata halafu Mwezi June deni likawa ni lile lile lililokuwa may. Means halijapungua. Nikawasiliana na mkurugenzi wao wakaomba eti radhi kuwa walikosea.
 
Back
Top Bottom