Ukisikia Miujiza Ndio Hii...

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,858
30,259
Ukisikia Miujiza Ndio Hii...
5978730.jpg

Karla kushoto na picha ya X-Ray jinsi bomu lilivyokuwa limenasa ndani ya mdomo wake.
Friday, September 30, 2011 3:52 AM
Mwanamke huyu wa nchini Mexico huenda alipata bahati kubwa sana kuweza kuendelea kuishi duniani hadi leo, alipigwa bunduki iliyoambatana na bomu lililonasa kwenye mdomo wake, wakati wowote lingeweza kulipuka, madaktari walikataa kumtibia, kila mtu alikimbia na hakutaka kuwa karibu naye.
Karla Flores ambaye ni mama mwenye watoto watatu alikuwa akifanya biashara ya kuuza chakula mtaani kwenye mji wa Sinaloa ambao una wauza madawa ya kulevya wengi, wakati aliposikia sauti kubwa ya mlipuko.

Karla alihisi kuna kitu kimempiga usoni, alipopeleka mkono wake kujua ni kitu gani, aliona damu zikivuja kwa wingi.

Karla mwenye umri wa miaka 34 hakuchukua dakika nyingi alidondoka chini na kuzimia.

Karla alikuwa amepigwa risasi kwa kutumia bunduki ambapo bomu liliambatanishwa kwenye risasi lakini bomu hilo halikulipuka kwenye mwili wa Karla na badala yake lilinasa ndani ya mdomo wake.

Wasamaria wema waliojitokeza kumsaidia waliona kuna kitu kimenasa kwenye shavu lake la kulia. Karla aliwahishwa hospitali.

Madaktari walimpiga picha za X-Ray ili kujua ni kitu gani kilichonasa kwenye mdomo wa Karla. Iligundulika kuwa bomu lilikuwa limenasa kwenye mdomo wake.

Kila mtu alihofia maisha yake, wagonjwa wote toka kwenye hospitali hiyo waliondolewa kwa kuhofia bomu hilo lingelipuka wakati wowote. Madaktari wote waligoma kumtibia Karla kwa kuhofia maisha yao.

Hatimaye Dr. Gaxiola Meza alijitoa mhanga kumfanyia operesheni ya kulitoa bomu hilo. Madaktari watatu wengine nao walijitolea kuokoa maisha ya Karla.

Karla alipelekwa kwenye uwanja wa wazi ambapo zana za hospitali zilihamishiwa hapo. Wataalamu wa mabomu waliwaelekeza madaktari njia salama za kulinasua bomu hilo toka kwenye mdomo wa Karla.

Operesheni ya kuliondoa bomu hilo ilianza mchana na ilimalizika usiku wa manane.

Karla alipoteza zaidi ya nusu ya idadi ya meno yake, alibaki na kovu kubwa sana kwenye shavu lake la kulia.

Madaktari wanasema kuwa Karla anahitaji miaka mitatu zaidi ndio aweze kupona vizuri jeraha kubwa kwenye mdomo wake.

Polisi wa Mexico wameanzisha msako kuwatafuta watu waliohusika na tukio hilo lililohatarisha maisha ya Karla.

<tbody>
</tbody>


chanzo: yu Mwanamke ana umri Mrefu Mwenyeezi Mungu amemsaidia ......
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom