Giambattista Vico
Senior Member
- Apr 3, 2015
- 106
- 24
Katika hospitali moja ivi ya wagonjwa wa akili, daktari alikua akiteremka kutoka floor ya sit a kuelekea chino kabisa,. Alipofika floor ya nne ndipo alioanza kusikia sauti kubwa ikisema "Ukishuka tu nakumeza". Baada ya kujiridhisha kwa akili yake kuwa hakukosea kile alichokisikia, alirudi floor ya juu na kuwajulisha wenzake qmbao nao walikiri kuisikia sauti hiyo ikisisitiza, " Ukishuka tu nakumeza" . Ndipo walipoamua kupiga simu kueleza wenzao wa floor ya chini. Nao walipotaka kupanda kuelekea ju u waliusikia sauti hiyo iliiyoongea kwa sauti na msisitizo usioashiria utani hata kidogo. Waliitwa polisi ili kuokoa raia waliokuwepo pale, na baada ya dakika chache askari wa special forces kama kwenye movie vile walianza kukabili eneo lile ambalo sauti ilikuwa ikiitokea, ndipo walipofika floor ya tatu sauti ile ikaongeza msisitizo "Ukishuka tu, nakumeza" Kwa uangalifu wa hali ya juu sana askari walijipanga na sasa walikuwa karibu kabisa na ngazi ambako sauti ile ilipotokea na sasa ilikua imeongeza kasi na msisitizo, "Ukishuka tu, nakumeza" Ndipo askari wale walipojiandaa kushambulia au kuattack. Walipojitokeza kwa adui hawakuamini macho yao baada ya kukutana na "kichaa" mmoja aliekua ametoroka wodini na kukaa kwenye ngazi kwa utulivu huku akilinyooshea kidole kamasi lililokuwa linatirirka kutoka puani kwake huku likiwa limekaribia sana kufika mdomoni, ndiye aliekuwa akiliambia kamasi hilo kwamba likiendelea kushuka tu analimeza!! Hakika hakuna alieamini kama na wewe ambavyo hujaamini. Naomba kuwasilisha