Ukishindwa kumnyonyesha mtoto miezi sita bila kumpa kitu chochote, andaa pesa ya tuition

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
653
Jamani kumekuwa na tabia ya watu kuwa busy na kushindwa kuwanyonyesha watoto kwa miezi sita bila kuwapa kitu chochote, hili ni kosa na tatizo kubwa sana kwa jamii.

Utafiti unaonyesha watoto wanaonyonyeshwa miezi sita bila kula kitu chochote wanakuwa na kinga imara dhidi ya magonjwa na ubongo mkubwa ukilinganisha na wale wanaoanza kupewa chakula au maji kabla ya muda huo.

Andaa pesa ya tuition kama utashindwa kumnyonyesha mtoto miezi sita mfululizo bila kitu chochote hata kama umempeleka international schools.

Wanawake msiwe busy sana na kazi na kusahau wajibu wenu wa malezi. Lakini pia ni vyema wenza kujipanga vizuri kabla ya kuzaa mtoto ili akizaliwa apate malezi mazuri.

Ukitaka mtoto mwenye afya imara na akili nyingi, anza kwa kumuandaa mke wako kabla ya kumpa mimba na pia lea mimba kwa upendo na uaminifu mkubwa. Mkinge mkeo na magonjwa yanayozuilika akiwa mjamzito. Baada ya mimba mpe malezi mazuri akizaa mpaka miaka miwili kwa maana ya chakula.

Nawaasa watu kuuiga pia utamaduni wa Wachagga katika kulea mke akizaa na utamaduni wa Wairaq katika kulea mimba.
 
Wengine hua wananyonyesha miezi sita inatimia kisha wanaacha, eti kisa maziwa yao yatashuka watakua na mi-nido mikubwa kama vile wana tenda ya kunyonyesha. Matokeo yake mtoto ananyonya kisha miezi 6 tu hanyonyeshwi tena. Hawa nao inabidi waanze kabisa kuchanga hela ya twisheni kwa ajili ya baadae!!
 
matajili wanajulikana wala huna ya kujionyesha kama kweli wewe tajiri. watanzia wengi ni masikini kwa taarifa tu. inawezekana wewe umekulia kariakoo kwa hiyo hujuitanzania tunaizungumzia ikoje. tanzania yako inawezekana niposta na kariakoo. watanzia ni masikini ndio maanahata bajeti yetu ni yakuomba omba na watotowetu wanakaa chini
 
Mbona umemjibu hivyo?
 
pakamwam, sisi tulinyonyesha watoto wote miezi 6 bila chochote. Na wakaendelea kunyonya kwa miaka miwili kila mmoja.

Sikuona tofauti yoyote na wengine kiafya. Msimu wa mafua wameumwa, vipele, kila kitu tu.

Darasani hawajaonyesha makali saana ila wanaelewa mambo mengi haraka sana na uwezo mkubwa kuunganisha mambo.

Wana nguvu sana lakini. Nafkiri ndo walichopata kwenye huko kunyonya sana.
 
wachaga wana utamaduni mzuri sana wa kulea mke siku arobaini akijifungua. wachaga mwanamke atachnjiwa mbuzi, kondoo na kupewa chakulakizuri, nenda kwa wenzangu wanyakyusa, mwanamke akijifungua ananunuliwa kila ya nyama na mbalaga. wambulu wao humchinjia mwanamke mbuzi kuanzia pale anapokuwa na miezi minne mpaka kujifungua kama wana uwezo. sasa wenzetu wa morogoro nni taabu tupu
 
kutokana na mlo bora na malezi mazuri ya mama na mtoto waangalie watoto wa kichaga au wachaga, ukiondoa walevi wa kupindukia utakuta wengi wana akili nyingi na pia afya nzuri. sasa nenda kwa wenzetu wa kumpa mke ngogwe tuu akiwa mja mzito na wabahili pale majirani, wengii miiili midogo na kudumaa sana, nazungumzia moro na upareni huku. wachaga wengi hawajadumaa ukilinganisha na wengine. mimi ni mnyakyusa siwasifii wachaga sababu mimi ni mchaga.
 
Mtoto akishafika miezi 3 tu maziwa hashibi kila mara mtoto atalia njaa na kupiga mihayo kwa sana, na asiposhiba mtoto kwa miezi hiyo Andaa ela ya tuition pia
 
sidhani kama kweli sana,kuna mtoto alinyonua miezi 3 tu maziwa ya mama yakakauka lakini ni tishio darasani kwa sasa tena anasoma hizo shule zenu za national sijui national park
 
huo niukweli mtupu na hata WHO wameweka kama guidiline ya kwa kuwaelimisha wajawazito nawatu wanaotegemea kupata mtoto. huoni utafiti uliochukua miaka mingi na World health organisation wamethibitisha na ndio maana mpaka wanashauri serikali ziongeze matenity leave hadi kufikia miezi sita
 
pakamwam, sisi tulinyonyesha watoto wote miezi 6 bila chochote. Na wakaendelea kunyonya kwa miaka miwili kila mmoja.

Sikuona tofauti yoyote na wengine kiafya. Msimu wa mafua wameumwa, vipele, kila kitu tu.

Darasani hawajaonyesha makali saana ila wanaelewa mambo mengi haraka sana na uwezo mkubwa kuunganisha mambo.

Wana nguvu sana lakini. Nafkiri ndo walichopata kwenye huko kunyonya sana.
ni vigumu kujua kuwa huyo mtoto anamake difference kwa kumwangalia darasani tu. pia uwepowa mtoto haupimwi katika kitu kimoja tu. pia kuhusu kuumwa mafua au magonjwa sidhani kama rate na uwezo wa kurecover unaweza kuwa sawa na ambao hawakunyonya miezi sita. pia kunyonya miezi sita pekee huku mama anashindia ngogwe haisaidii. hapa ninamaanisha mama atunzwe na apate lishe kamili ili atoe maziwa yenye kiwango kizuri. pia mtoto wako ana akili nyingi sema hujajua jinsi ya kuasses iq yake
 
Mtoto akishafika miezi 3 tu maziwa hashibi kila mara mtoto atalia njaa na kupiga mihayo kwa sana, na asiposhiba mtoto kwa miezi hiyo Andaa ela ya tuition pia
kutoshiba ni imani tu. huwa anashiba labda kama mama hali vizuri. mama inabidi apewelishe bora na awekwe kwenye mazingira maazuri yakisaikolojia ili aweze kula vizuri na kutoa maziwa mengi
 
Back
Top Bottom