Wana bodi historia kweli hujirudia kuna mifano mingi ya kuonyesha kwamba mwosha kumbe nae huoshwa. Hapa nitatoa miwili tu.
1. Huyu Rais Buhari wa sasa aliwahi kuipindua serikali halali ya kidemokrasia ya Shehu Shagari ndani yake kulikuwa na waziri wa mambo ya ndani akiitwa Umaru Dikko wakati wa mapinduzi yanatokea yeye alikuwa ndani ya ndege akirudi toka Uingereza, kufika uwanja wa ndege akakuta taa za uwanja zimezimwa, akawasiriana na waongoza ndege waliokuwa chini na kuwauliza kwa nini taa zimezimwa kwani kuna mtu wa mhimu sana anataka kutua, waongoza ndege wakawasiliana na wanajeshi waliokuwa uwanjani kwamba kuna VIP anataka kutua wakafikiri kwa haraka anaweza kuwa nani wakajua atakua ni Umaru Dikko ambaye walikuwa wanamtafuta sana, basi wakamwashia taa moja alivyotua tu wakamkamata siku hiyo hiyo akaenda kulala Kirikiri maximum security prison, sasa wakati wakulala akauliza mablanketi yako wapi? Wafungwa wenzie wakaanza kumshangaa unamwuliza nani mabalanketi yako wapi wewe si ndiye ulikuwa waziri wa mambo ya ndani? Ulifikiri ungekuwa waziri mpaka lini " No situation is permanent".
2. Huyu John Malecela baba yake Le, Mutuz mwaka 1972 alikuwa waziri wa mambo ya nje , miaka hiyo Uganda ikiwa teyari imepinduliwa na General Amin, Obote akiwa Dar kwa kusaidiwa na Nyerere alitaka kwenda na yeye Uganda kufanya mapinduzi ambayo hayakufanikiwa basi ukazuka uhasama mkubwa kati ya Mzee Nyerere na General Amin , Amin alikuwa anadai Obote na Waziri fulani wa serikali ya iliyopinduliwa ya Obote warudi Uganda ili washitakiwe kwa kutaka kufanya mapinduzi ambayo yalishindwa. Rais wa Somalia General Siadi Barre akajitolea kuwa msuluhishi. Tanzania ikawasilishwa na waziri wake wa mambo ya nchi za nje Bwana John Malacela na Uganda hivyo hivyo Bwana Wanume Kibedi, ndani ya mazungumzo Wanume Kibedi akawa mkali na kusisitiza waliotakiwa warudi Uganda, unajua Malacela babayake Le, Mutuz nation alimwambiaje" Dont` press so much hard on that you will yourself find in the same position in the near future". Kwani Wanume Kibedi alichelewa muda mfupi akawa na yeye mkimbizi.
Wanasiasa mnalo la kujifunza unapokuwa madarakani ni sawa na mtu ambaye ameshiba basi msianze kajeli wooo huyu mgonjwa sijui amajinyea kufanya hivyo ni sawa na mtu aliyeshiba sana akaanza kumwonyesha mungu tumbo akiwemo mwenyewe mkuu wa kaya.