Ukishiba mshukuru Manani

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,084
Kuna wakati nilisema chakula ni ibada kiheshimiwe kisichezewe wala kutupwa...! Ukiangalia hii picha unaweza kujua nilimaanisha nini
 
Yani natamani nikakachukue ako kadogo nikatunze basi tu.
 
Hawa ndo wanajua shida, sio wewe unakaa foleni lisaa limoja na kibaby walker chako unakuja kulialia huku
 
Alhamdulillah Alaa kulli Hal. Hapa ndo binaadam ajue kwa nini kasisitizwa atoe zaka na sadaka. Lkn kwa dunia ya sasa alonacho anacho na alokua hana, hana.
 
Mkuu inasikitisha sana, watoto wadogo wana mazito yaliowazidi umri wao, wakati mtu mzima chakula unachagua mara leo sitaki hiki, mara kesho sitaki kile, mara nimechoka aina fulani ya chakula kinanenepesha mno, wakati wenzetu hao wanatamani ambacho wewe hakipo kwenye ratiba yako.

Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi, kwa kweli inasikitisha sana
 
HARUFU tunapaswa kumshukuru Mungu hata kwa hiki kidogo tunachokipata kwakuwa wapo wengine hawakipati kabisa
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…