Ukishangaa ya uvccm utaona ya lipumba na hamadi rashid

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
CHAMA cha wananchi (CUF) sasa kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuonyesha kwa vitendo kupinga kauli ya kichochezi za uvunjaji wa amani zinazotolewa na chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA ) na kudai kuwa Chadema si chama chenye nia njema a amani ya Tanzania.

CUF imesema kuwa Rais Kikwete Kikwete ameshindwa kuwachukulia hatua dhidi ya Chadema pamoja na kuapa kuilinda na kuitetea katiba ya Tanzania ila ameiacha katiba hiyo ikiendelea kuvurugwa kwa kauli za kichochezi dhidi ya serikali yake.

Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa baraza kuu la CUF Taifa Hamad Rashid ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Wawi na kiongozi wa kambi ya wabunge wa CUF bungeni ,kuwa Chadema wasitumia shida za watanzania kwa ajili ya kufanikisha matakwa yao ya kuchochea vurugu na kulifanya Taifa la Tanzania kuwa Misri na nchi nzingine.

Alisema kuwa hakuna mtanzania ambaye anapendezwa na ugumu wa maisha yaliyopo sasa chini ya uongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) chini ya Rais Kikwete ila hakuna mtanzania ambaye yupo tayari kuona amani inapotea na watanzania wakiuana kwa vita kutokana na kauli za uchochezi zinazofanywa na Chadema.

Alisema kuwa vyombo vya dola vya Tanzania vimeendelea kunyamaza kimya na kuchelewa kuchukua hatua ya kulinda amani ya Taifa hili na kuacha Chadema kuendelea kutoa kauli za kichochezi dhidi ya serikali huku vikitambua wazi kuwa kauli hiyo zinakwenda kinyume na katiba ya nchi yetu .

“Hatuna imani na katiba ya Tanzania ila hatupo tayari kuhamasisha wananchi kufanya vurugu ili kuiondoa serikali madarakani kama wanavyo fanya wenzetu Chadema….sisi tunatambua njia pekee ya kuiondoa CCM ni kusubiri uchaguzi mkuu mwaka 2015 na sio vinginevyo..tunasema CUF hatuungi mkono hata kidogo uchochezi unaofanywa na Chadema dhidi ya serikali yetu wananchi mkiano chama chochote cha siasa hakiheshimu maamuzi ya wananchi chama hicho hakifaa kupewa hata kuongoza kundi la watu kumi”
ATTACH]
 
Watu wenyewe anaohutubia hata mia hawafiki , kwisha habari yake , chadema tunatisha jamani, hebu linganisha na hii nyomi ya mzee mbowe pale mwanza furahisha
 
CUF sasa wamesilimu rasmi na kuwa CCM "B" Siamini maneno ya HAMAD RASHID na PROF. LIPUMBA kama kweli wao waliopeleka watu katika maandamano ya Jan 21 leo wanasema wenzao ni wahaini? Hapa waTZ tujifunze kwa hili, wanasiasa wa Bongo sio wa kuwaamini kabisa. SITOSHANGAA KUWAONA LIPUMBA NA HAMAD wakicheza muziki wa TOT kama MREMA pale Dodoma KTK MKUTANO MKUU WA CCM.
 
Poleni sana CUF, ndio jeneza lenu hilo.... hatudanganyiki tena!!!!:tongue:
 
cuf are contradicting themselves! ninaanza kuthibitisha they are no more opposition party
 
Sijui kwa nini watu wanaiogopa CHADEMA kuliko kuogopa Hali ngumu ya Maisha ya Watanzania ambayo ndiyo inayotishia Amani kuliko kitu kingine chochote
 
Sasa hivi ni wakati muafaka wa CHADEMA kuingia Zanzibar kwa hawa CUF hata wapemba wenyewe wamewachoka kwani viongozi wao ilikuwa tamaa ya madaraka na si kuleta mageuzi ya kisiasa na kiuchumi kwa Zanzibar, CHADEMA wakiingia Zanzibar wapatapata wanachama wengi sana toka CUF na uchaguzi ujao wapiga si chini ya majimbo kumi kwa upande wa Zanzibar
 
Prof, uliahidi kuwa utagombea urais mpaka kieleweke. Kwa hali hiyo, prof unajizika. Aibu yako wewe. Au na wewe unataka serikali ya mseto bara? Hapana hao hawakupi, ni Zenji tu ndo wamekubali. Prof, unakumbuka gharama ya mseto kweli? Watu walikuwa wakimbizi.

Umakamu wa rais prof hauji kwa kujikomba hivyo. Msipoangalia mtakuwa mto wa msimu, na eneo lenyewe likageuka jangwa.
 
Nchi yetu ina laana kiasi gani?
CUF inayotajwa hapa ina tofauti gani na ile ya mwaka 1996 na 2001? Hawa jamaa wamefikia hatua hata hawajui waseme nini na waache nini? Walipokuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa waliitwa majina sawa na Chadema ya leo (Wadini, Wachochezi na mbaya zaidi wao waliitwa Magaidi). Cha ajabu badala ya kusaidiana na CDM kupinga siasa chafu za Mafisadi dhidi ya vyama vinavyokuwa na nguvu wao wamechagua kushirikiana na CCM kuua upinzani kwa kudhania watapata nafasi katika kamati Bunge na serikali ya mseto ambayo katika Muungano bado ni ndoto.
Binafsi CUF wananichefua.
 
Prof, uliahidi kuwa utagombea urais mpaka kieleweke. Kwa hali hiyo, prof unajizika. Aibu yako wewe. Au na wewe unataka serikali ya mseto bara? Hapana hao hawakupi, ni Zenji tu ndo wamekubali. Prof, unakumbuka gharama ya mseto kweli? Watu walikuwa wakimbizi.

Umakamu wa rais prof hauji kwa kujikomba hivyo. Msipoangalia mtakuwa mto wa msimu, na eneo lenyewe likageuka jangwa.

Hiyo ndo ccm b kwisha kazi wamekuwa chombo cha propaganda cha ccm wapi lipumba mzee wa hakiiiii toka viwanja vya jangwani hadi kidongo chekundu na sasa wanahutubia manzese hawaizewi pipoz power kwisha habari yao hana tena ushawishi kwa jamii musoma watu walikimbia mkutano wake wakaenda kwa zitto chama kimebaki jengo tu buguruni viva chadema go hard tuko pamoja pipooooooooooooooozz
 
Cuf kwisha kazi!walikula ya mbuzi wameota mapembe!sasa wanaanza kulia,watanzania wote tumaini lao ni Chadema.PEOPLES POWER
 
haya washajidharaulisha hawa wajameni.........:washing:wamefulia Cuf hahahaha...:washing:
 
HR ni hasira za kukosa kuwa KU Bungeni na hiki ndicho kinachomsumbua, hajui ya kwamba nafasi ile haikuwa pale kwa ajili ya CUF pekee, poleni saana wana cuf kwani yale mauaji yaliyotokea miaka ile ilikuwa ni kwa sababu ya nini? Kama HR hujui basi sasa tambua ya kwamba cuf ndo imeshachota maji iko mrama hivyo kama waweza jiokoe sasa kwa kuhamia jahazi lingine. Watz sasa washajua namna ya kudai haki na mimi niwapongeza CDM kwa kuwaelimisha wananchi kwani wameanza kujua nini maana ya siasa ENDELEENI.
Asanteni CDM kwa kututoa matongotongo sasa tunaona vizuri tushindwe wenyewe.
NAWAKILISHA.
 
Jamani mie nauliza: Hivi hizi habari za Prof na Hamadi Rashidi kuisemea CCM dhidi ya Chadema mbona huwa sizisikii katika vyombo vya habari? Huwa zinaandikwa kwenye magazeti yepi, na katika kurasa zipi?

Kama yapo magazeti huziandika basi labda huzificha katika kurasa za ndani!!! Na kurasa za ndani ndimo wahariri wa magazeti wanaona panawafaa!

Ni aibu kubwa wanayofanya viongozi hawa wakuu wa CUF na mtu kama Hamadi Rashidi anasahau usaliti aliofanya kwa Wapemba wenzake miezi michache tu baada ya mauaji ya wafuasi wa CUF kwa risasi za polisi wa CCM pale alipokubali uteuzi kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Mkapa.

Hiyo ilikuwa ni hongo kutoka kwa Mkapa kwamba Hamadi afunge domo lake -- asilalamike sana kuhusu mauaji yale! Kweli kumtumikia Bwana ndiko huku?
 
Hawajui watendalo. Kama wanajua wameamua kusupport ufisadi ili wananchi waendelee kufa kwa njaa, maradhi na matatizo yote yanayosababishwa na ubovu wa serikali.
 
CHADEMA wawemakini sasa muda huu ndio wa kuingia ZANZIBAR na kunadi sera zao na kuwaeleza ukweli kuwa sikweli kuwa wao wana wadharau wa ZANZIBARI bali muungano wa CCM na CUF ktk serikali ya mapinduzi ni kiinimacho na utata wa kikatiba kwa katiba ya jamuhuri ya muungano. Wakiwaendea wazanzibari na kujinadi watajiimarisha sana visiwani huo, kuzomewa na kukejeliwa wakutegemee maana CUF na CCM ni kitu kimoja na wako wengi huko lakini hizo ndio siasa lazima ujumbe ufike visiwani na naamini wazanzibari ni waelewa watafanya maamuzi magumu
 
CUF wanapotea nia kwa kuwa wameonjeshwa madaraka visiwani:lol:
 
Mkuu waliongea hayo wakiwa msikiti upi!? wakuu kuna kiongozi yoyote wa CCM -B I meant CUF ni member wa JF, Maana haja jamaa c prof hadi mtatiro computer "IT" kwao n mtihani, that y harakati zao ni misikitini na kwenye ghahawa, duh! Hawana issue kabisa wamechokaaaaaa
 
Yale mamilioni aliyokuwa anakunja kama KUB yanamuuma saaaaaaaaaaaaaaana. KUTESA KWA ZAMU MAALIM.
 
Back
Top Bottom