Mwakamajoka
Senior Member
- Nov 21, 2017
- 170
- 149
Kabla hatujasahau tukumbushane kitu muhimu ambacho kimepelekea au kunishawishi kuandika uzi huu. Katika ulimwengu huu wa sasa na kwa mda mrefu Marekani ndiye taifa kubwa na lenye nguvu katika nyanja mbali mbali kwa mfano kiuchumi, kisiasa na kijeshi. Marekani pia amekuwa mstari wa mbele kama Kiranja Mkuu wa Dunia kwa kuwawekea vikwazo vya kibihashara mataifa mbali mbali akiwemo Urusi. Vikwazo hivi amevifanya kupitia nguvu yake na ushawishi wake alionao ndani ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya.
TUENDELEE NA MADA KUU :
Urusi imesafirisha gesi (Liquefied Natural Gas) kwenda Marekani. Sababu kubwa iliyopelekea kufanyika kwa mpango huo ni kupanda kwa bei ya gesi katika maeneo ya mwamboa wa pwani ya Mashariki ya Marekani.
Meli inayomilikiwa na kampuni ya nishati (Engie) kutoka Ufaransa imepata deal la kusafirisha gesi (Liquefied Natural Gas) kutoka Uingereza mpaka pwani ya mashariki kwenye kituo cha gesi cha Everett karibu na Boston Marekani.
Gesi inayosafirishwa kwenda EVERETT-BOSTON-USA inatoka Urusi kwenye kiwanda cha gesi(Liquefied Natural Gas) kinachofahamika kwa Jina la YAMAL LNG.
Meli kubwa inayofanya kazi ya kusafirisha gesi (Liquefied Natural Gas) kutoka bandari ya Isle-Grain-British kwenda kituo cha gesi cha Marekani kinachopatikana Everett karibu na Boston itafika kwenye kituo cha Marekani tarehe 22/1/2018.
Mpango huu umeitikia mfumko wa bei ya gesi usio wa kawaida unaofikia dola za kimarekani 6,300/= per thousand cubic metres katika pwani ya mashariki ya Marekani.
Vikwazo vya Marekani dhidi ya sekta ya nishati ya Urusi haijazuia moja kwa moja usambazaji na uuzwaji wa gesi kutoka Moscow mpaka Marekani. Ijapokuwa, Washington imeendeleza msimamo wake wa kumzuia URUSI kuwa Mfalme wa biashara ya gesi katika bara la ULAYA.
Meli inayosafirisha mzigo imepokea mzigo wa gesi(Liquefied Natural Gas) katika bandari ya Isle-Grain-British baada tu ya meli ya Urusi (Christophe De Margerie) kufika Uingereza mwezi wa 12/2017 na mzigo wa gesi kwa mara ya kwanza.
Meli ya Urusi iliyosafirisha mzigo wa gesi mpaka Uingereza ilipewa Jina la Christophe De Margerie baada ya aliyekuwa CEO wa kampuni ya TOTAL Bwana Christophe De Margerie kuaga dunia/ku-rest in peace, baada ya ajali mbaya ya ndege kutokea huko Urusi. Meli hiyo inauwezo wa kubeba shehena ya liquefied natural gas kiasi cha 173,000 cubic metres. Urusi ili kufanikisha malengo yake mengine ya badae anampango wa kutengeneza meli zingine kubwa 15 zenye ukubwa kama Meli ya Christophe De Margerie.
Source: Kommersant daily report