Ukiruhusu pesa kuongea, umekwisha!

zeus47

JF-Expert Member
Jul 27, 2014
233
307
Hakuna wakati unakuwa na amani na utulivu wa akili na kuweza kupanga mambo ya maana kama usipokuwa na pesa mfukoni. utapanga mambo mengi ya maana ... sijui kupiga rangi nyumba, kutumia wikiendi kuwafariji wagonjwa, kufungua fixed-deposit account, kupunguza deni la mavuno kanisani, na kadhalika.

Sasa ngoja upate pesa .... ni shida tupu! Kelele za pesa hazina mpangilio, ni fujo tu .... sijui hata kelele zinatokea wapi .... mara utasikia wewe Chacha Mwita marafiki zako wamekukosa sana pale Rose Garden nenda Bwana, Chacha Mwita watu wa nguvu wakitoka kazini lazima wapitie sehemu kupoteza mawazo kwa moja moto moja baridi .... si unakumbuka ile TV 65" pale Amazing Life Sinza iko kwenye sale? Na wale wa Africasana ndo wanaweka kambi pale usiku kucha kuopoa vifaa vipya.

..... ngojea sasa shughuli ya mwisho wa mwezi, ni mtiririko wa message - kama ulijichanganya ukasema nimeajiriwa sijui Benki, TRA, .... basi hizo pesa lazima mgawane. Ndio maana wengine tukiulizwa unafanya kazi wapi ... jibu ni simple tu .... " aaah ... siku hizi nafanya shughuli zangu mwenyewe ndugu yangu." ... yote tunakwepa kelele za Pesa .... kuna watu hunusa hadi mifukoni. Siku huna pesa, hata salamu hakuna!

Usiziendekeze kelele za pesa. Utashindwa kufanya jambo lolote la maana. Wewe ziba masikio .... upate nafasi ya kuzisikiliza sauti za kistaarabu za wakati huna pesa. Hizi kelele zinazongojea uwe na pesa hazina mpngo wowote ... hata siku moja huwi nazo unapopiga magoti kumwomba Mungu akujalie uzima, afya na baraka katika kutimiza agizo lake la kufanya kazi ili ule.

Mpango Mkakati, Mpango Kazi ... taja Mpango wote lakini MWISHO WA MWEZI shughuli nyingine. Na hizi ATM zao ndio sheedah tupu! Unaweza kushtukia unalazimika kuomba bank statement ukiamini kuwa benki wamekwapua senti zako ... kumbe wapi bwana! Shida ni mwisho wa mwezi ... hata ukimkanyaga mtu unamwomba msamaha kwa "Sorry" lakini ngoja uchache utajua kiswahili hata cha kwenye Kamusi .... "Samahani ndugu yangu, sikukuona bwana ...

Mawazo ndugu yangu.
 
Ndio yalishatokea ndugu, Mwenyezi Mungu azidi kukufariji na kukupa uvumilivu.
 
Back
Top Bottom