Ukiona wamevaa lebasi za ulimbwende ujue kuna jambo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukiona wamevaa lebasi za ulimbwende ujue kuna jambo!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 3, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Je umeshawahi kumtazama mkeo au rafiki yako wa kike katika namna yake ya kuvaa? Lakini je, hata wanawake unaowajua ambao unakutana nao kila siku, iwe kazini, mtaani au popote, umeshawahi kuwatazama na kujiuliza kuhusu uvaaji wao? Kama umekuwa ukiwatazama, labda umekuwa ukiwatazama kupendeza au kuchusha kwao tu, na siyo jambo lingine. Lakini kuanzia sasa itabidi uwe unawatazama kwa sababu na namna tofauti kabisa.

  Kwa nini?

  Ni kwa sababu watafiti wamebaini sasa kwamba, mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hatari, yaani kwenye zile siku ambazo anaweza kupata ujauzito kama atashiriki tendo, huwa anavaa tofauti na siku nyingine za kawaida. Utafiti mkubwa umefanywa na wataalamu mbalimbali, umeonesha kwamba, mwanamke hujikuta akivaa vizuri zaidi wakati ambapo yuko kwenye siku za hatari. Siyo kuvaa vizuri, bali pia huvaa nguo zenye kuonesha zaidi maungo au ngozi yake. Kama hiyo haitoshi, huvaa pia marembo au vito kama dhahabu au makochokocho mengine (Lebasi za ulimbwende) tofauti na siku nyingine. Ni kwamba hujipamba zaidi. Uvaaji huo unaelezwa kwamba, unatokana na maumbile, na mwanamke huwa hajui ni kwa nini anavaa vizuri au kujipamba zaidi wakati fulani kuliko wakati mwingine.

  Pamoja na kwamba kuna sababu kadhaa za kujipamba, inapofika kipindi hiki cha hatari uvaaji wa mwanamke unabadilika bila mwenyewe kujua. Huvaa vizuri ikiwa ni nia ya kutoa taarifa kwa mwanaume kwamba, yuko tayari au kumvuta mwanaume, kimaumbile ikiwa ni lengo la kupata mtoto. Hii ni kawaida ya maumbile ambapo mnyama wa kike anapokuwa kwenye nyakati za kutaka kupandwa ili kuzaa huonesha dalili fulani. Kuna wanyama ambao hutoa harufu kali ambayo humfanya dume kujua kwamba mnyama huyo wa kike anataka kupandwa. Wanyama wengine hubadilika rangi ya ngozi.

  Kwa binadamu anaonekana kuvaa kwa namna ya kuvuta ndiyo njia ambayo mwanamke anamjulisha mwanaume kwamba, yuko kwenye kipindi ambacho anaweza kupata ujauzito. Bila shaka, siku za nyuma kabisa kabla ya kile kinachoitwa ustaarabu wa kujua zuri na baya, kabla binadamu hajaanza kuingia katika ustaarabu wa kutongoza na kila mtu kuwa na wake, mwanamke kujipamba ilikuwa ndiyo njia ya kuwashawishi wanaume kufanya naye mapenzi ili kupata ujauzito.

  Kama nilivyosema, hii ni kazi ya maumbile, kwa hiyo mwanamke anakuwa hajui ni kwa nini anachagua nguo fulani, au kujikuta akitamani kujipamba katika siku fulani. Kwa mfano, imebainika kwamba, mwanamke ambaye huwa anapenda kuvaa sketi fupi au wakati mwingine suruali, anapokuwa kwenye siku zake za hatari ni lazima atavaa sketi fupi badala ya suruali. Kama nilivyosema kuna sababu nyingine ni kwa nini mwanamke anavaa kwa njia fulani. Kwa mfano kama anataka kuonesha maungo yake kwa kuvaa nguo fupi au za kubana, akiwa kwenye siku zake za hatari atajikuta akiongeza na mapambo mengine au pengine kuvaa nguo zenye kuonesha maumbile yake zaidi.

  Hii ni kwa binadamu wote, siyo kwa waafrika peke yake kwani ni suala la kimaumbile. Hata wazungu ambao huvaa nguo za kuonesha maungo bila kujali, linapokuja suala la siku za hatari za mwanamke, uvaaji wao huwa tofauti. Ni lazima wataongeza chumvi kwenye uvaaji wenye kuonesha maungo au kubana na pengine kuwa na mapambo mengi maungoni. Jarida la Hormones Behaviour linaonesha kuhusu utafiti ambao ulifanywa kwa wanafuzni wa kike wa vyuo vikuu. Linaripoti kwamba, hata wale wasichana ambao uvaaji wao ni wa hovyohovyo, wakati wa siku zao za hatari walionekana kuvaa kwa kuvutia na kujipamba pia. Mtafiti Martie Haselton wa chuo kikuu cha Califonia Los Angeles nchini Marekani na timu yake ambao wamefanya utafiti kuhusu jambo hili, amesema, hakuna mtu anayeweza kujua kwamba, anavaa kwa namna fulani kwa sababau yuko kwenye siku zake za hatati, hivyo anaweza kudhani anavaa kwa namna fulani kwa sababu nyingine au kwa mazoea.

  Ndio maana unaweza kuona mwanamke anaazima nguo fulani kwa mwenzake, mkufu au kitu kingine kinachoweza kumfanya apendeze zaidi, wakati wala haendi mahali ambapo ingekuwa ni lazima abadili. Kuna kitu kinamsukuma kuvaa tofauti kidogo. Kuna namna nyingi ambapo mwanaume anaweza kujua kwamba, mkewe au mwanamke mwingine yuko kwenye siku zake za hatari. Kuvaa kwa namna ambayo inaonesha kuwa inalenga kuvuta zaidi wanaume ni moja ambayo ni kubwa. Haina maana pia kwamba, mwananamke aliye kwenye siku zake za hatari, ni lazima avae kwa njia yenye kuamsha hisia za mwanaume, hapana. Bali atavaa kwa njia yenye kuonesha zaidi ngozi yake na pia kuwa na mapambo ya ziada.Hivyo mtu asije akadhani kila mwanamke anayevaa kwa njia ya kumtia mwanaume ushawishi yuko kwenye kipindi chake cha hatari.
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ni kama wanyama tu akiwa na hamu anajisogeza kwa madume.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa tusiovaa "Lebasi za ulimbwende" na kila mara aina ya mavazi ni ile ile inakuwaje? Hatuna hizo 'hatari days'?
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Da' Lizzy, kama sio mavazi basi hata kujiremba kusiko kawaida kunaweza ku-reflect na hali hiyo.................Wataalamu wa masuala ya kujamiiana hawahitaji hata kutumia mawani kung'amua kama mwanamke yuko kwenye Heat Period.
   
 5. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Shikamoo baba,
  Mmmh,nilikuwa sijui,
  Kumbe na binadam ni km wanyama.
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hhhm hata kujiremba sijawahi "kujiremba kusiko kawaida". Hua natumia vile vile kila mara, siongezi wala sipunguzi.
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Haya mambo ya wakubwa hayakuhusu, kwanza umeshafanya Home work, au ndo ushatafuta mvulana wa kukufanyia?
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa mtu aliyekuzoea, ni rahisi kujua ni kipindi gani upo kwenye kilele cha utukufu, na hiyoni kwa sbabu hata wewe mwenyewe hujui ni kwa nini unajiremba kwa staili fulani au kuvaa mavazi fulani ambayo yana kushika mwilini au kuonesha ngozi ya mwili wako. Hili jambo ni la kimaumbile zaidi kama nilivyosema.........................
   
 9. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  interesting??????????
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Bado sijapata jibu langu kwasababu kama mtu sio wa kubadilika badilika sioni ni namna gani utamsoma.I mean kama navaa nguo za kubana mara kumi kwa mwezi katika vipindi tofauti tofauti mtu atajuaje nilikua tayari wiki ya kwanza, ya pili, ya tatu au ya nne?Au pengine mwili wangu hauna msimamo. . .heheheh!!

  Swali jingine. . .je inatokea pale mtu anapotoka nje tu (kwenda kwenye mizunguko) au hata akiwa nyumbani? Maana kinyumbani nyumbani mtu anaweza akamaliza muda mrefu bila kujipara!!
   
 11. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna connection gani kati ya siku za hatari na heat period? maana hii heat period huwa naiskia kwa wanyama.Na tofauti ni ipi kati ya siku za hatari au siku za mhemko wa hatari? hebu dadavua kidogo dalili mbili za wazi kubwa za kuwa kwenye siku za mhemko ukiacha ya mavazi.Nataka kujua ili siku nikipata mtoto wa kike nijue control measures................kakionesha dalili nakafungia ndani
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  mmmmmmmmmhhh!!!!!
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kuna wadada wanajiremba mpaka anakuwa kero kwa mhusika anakupotezea kabisa utulivu
   
 14. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hahahhhahahah!
  Kumbe siku ile hukunistukia ilikua mkwara tu!!!
  Poa dady,nafanya home work!!
  Km unajua mie bado mdogo mbona huwa unammind sana yule kaka anayenipaga lift kwenda shule???!!!
   
 15. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ...ndefu lakini imenyoooka!!
   
 16. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  mmh kweli kujua kusoma kuzuri ,, maana ingebidi nisimuliwe hii habari.
  nakushukuru kwa kuniongezea knowledge
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Dada Lizzy nawe...............Unakuwa kama hawa wanangu kina NginaCantalisiaKing'as-t, mbona nimeshajibu hapo juu kama nilivyobainisha, hebu ngoja ninukuu hapa:
  "Ndio maana unaweza kuona mwanamke anaazima nguo fulani kwa mwenzake, mkufu au kitu kingine kinachoweza kumfanya apendeze zaidi, wakati wala haendi mahali ambapo ingekuwa ni lazima abadili. Kuna kitu kinamsukuma kuvaa tofauti kidogo. Kuna namna nyingi ambapo mwanaume anaweza kujua kwamba, mkewe au mwanamke mwingine yuko kwenye siku zake za hatari. Kuvaa kwa namna ambayo inaonesha kuwa inalenga kuvuta zaidi wanaume ni moja ambayo ni kubwa."

   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huyo kijana wako wa lift namtegeshea ndoa ya mkeka, wewe subiri tu....................................
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hivi kiingereza cha neno "siku za hatari" ni kipi?
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Binti hujambo!
   
Loading...