Ukiona viashiria hivi, basi ujue mumeo anatoka nje ya ndoa……………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukiona viashiria hivi, basi ujue mumeo anatoka nje ya ndoa……………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 12, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Zifuatazo ni baadhi ya dalili ambazo endapo mwanandoa atazibaini kwa mwenzake, anapaswa kuanza uchunguzi au kujadili naye jambo hilo ili kujiondoa katika wasiwasi. Lakini nitahadharishe kwamba dalili za mtu anayetoka nje ya ndoa ziko nyingi sana, kiasi kwamba siwezi kuziweka zote hapa, ila hizi nitakazozitaja zimethibitika kuwa zinapojitokeza, uwezekano ni mkubwa kwamba, mhusika anatoka nje ya ndoa yake.

  1. Kuongeza upendo ghafla: mwanaume anapoanza kutoka nje yandoa, kama ndoa yake haina vurugu , anaweza kuonesha upendo mkbwa hadi mkewe akashanaa na kujiuliza . inakuwa kama vile ndiyo amekutana na mkewe kwa mara ya kwanza. Hii ni kutokanana kushitakiwa na dhamira kwa sababu anajua anachokifanya ni makosa huku akijua ndoa yake haina matatizo, na mkewe hajawahi kumkosea na anatimiza wajibu wake. Hata hivyo haina maana kuwa kila upendo ukiongezwa na mwanaume ghafla mwanaume huyo anatoka nje ya ndoa…………. Na ndio maana nikasema awali kuwa ni vyema uchunguze.

  2. Kuona kasoro nyingi za mke: kama mume anaanaza kuona kasoro nyingi za mkewe ambazo hapo nyuma alikuwa hazioni, basi ana lake jambo. Hii ni katika kujitetea nafsini mwake, na kuhalalisha kwamba kutoka kwake nje kuna sababu

  3. Mabadiliko ya kipato: Kuna wakati mabadiliko ya kipato yanaweza kuwa ni kiashirio cha mwanaume kutoka nje ya ndoa. Mwanaume anaweza kuwa na ajira ile ile au shughuli zilezile lakini ikaonekana kwamba kipato hakitoshi. Suala la fedha linaweza kuanza kuwa ni tatizo kubwa kwa familia.

  4. Kujibadili sana: Ingawa siyo lazima, lakini hutokea wakati mwingine mwanaume ambaye ameanza kutoka nje ya ndoa kuanza kujibadili sana pia. Anaweza kuanza kuvaa nguo nzuri nzuri, kujipulizia manukato tofauti , kunyoa kwa mitindo tofauti na mengine yanayofanana na hayo. Mara nyingi mabadiliko hayo hufanywa na hiyo nyumba ndogo akijaribu kumbadili huyo mwanaume kwa kadiri anavyotaka yeye.

  5. Alama na harufu mpya: Kama mwanaume siyo makini sana, kupatikana kwa rangi ya mdomo kwenye shati au nguo zake za juu ni rahisi sana. lakini hata kama ni makini, harufu ya pafyumu tofauti na ile anayotumia mkewe inaweza kusikika sana kwenye nguo zake.

  6. Mazungumzo ya simu: Kama mwanaume anaanza kuzungumza kwenye simu kwa kukatishakatisha au kusema tu, ‘nitakupigia baadae,' ama wakati mwingine kuonekana amebabaika baada ya kupokea simu, inaweza kuwa dalili. Kuna wakati anaweza kuwa anakata simu kila ikiita na kubadilika hata usoni kwa tahayari.

  7.
  Ratiba ya kazi kubadilika: Kazi huwa inatumiwa kama kisingizio na wanaume wengi sana, hasa wanapoanza kutoka nje ya ndoa zao. Dalili kubwa kabisa ni ile ya mwanaume kuanza kuchelewa kurudi nyumbani kwa kisingizio cha kazi, kusafiri sana kwa kisingizio cha kazi, kulala nje kwa kisingizio cha kulala kazini (Night Shift).

  8. Mbele ya wanawake wengine: Tafiti nyingi zinaonesha kwamba, wanaume huchukua wanawake ambao wako karibu nao, au wamewazoea kwa njia ya kukutana mara kwa mara. Ni rahisi mwanaume kuwa na hawara ambaye ni jirani, mfanyakazi mwenzie, mshiriki wake kibiashara, rafiki wa familia, au hata mwanafunzi wake. Kwa kawaida mwanamke mbaye anatembea na mume wa mtu anaweza kujionesha kirahisi anapokuwa na mwanaume huyo. Kwa hiyo mwanamke asijidanganye kwamba, kwa kuwa mwanamke fulani ni rafiki wa familia, ni jirani, ni mwanafunzi wa mumewe, hawezi kuwa na uhusiano naye, hapana. Kwa mwanaume, hao ni mawindo rahisi sana.
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Umefikwa na haya? Ama unahisi!
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  asanteee, uje na ya mwanamke anayatoka pia
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Vuta subira..........nitazianika hapa siku si nyingi.............
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Good one mtambuzi... lakini there are alot of other factors to consider coz pretenders could skew expectations
   
 6. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Yeah... Nilishasema hapo mwanzoni kwamba dalili ziko nyingi kutegemana na aina ya mwanaume, maana kuna wengine ni silent killer, wala huwezi kuwagundua kirahisi labda utumie mbinu za kiintelijensia.....................
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,581
  Trophy Points: 280
  no comments.
   
 8. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,672
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
  Na wewe hujaacha tu kuchukua sample ya familia yako...
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkwe... hujaacha tu utundu wako, nilijua tu hutakosa la kusema, nimefurahi kuwa leo umejifunza jambo jipya...............
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa nini jamani.... weka basi hata neno moja.......................
   
 11. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wanaume watakukoma mwaka huu!!
   
 12. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mkuu ni sawa usemayo ila kuna uwalakini maana kuna tabia nyingine si kwamba wanaume anaweza kuwa anatoka ila anaweza kuwa anakwepa maudhi ya nyumbani.. si unajua sie wanaume huwa tunaamini kuchelewa kurudi home au kuwa na muda mdogo wa kuwa na familia ni kukimbia tatizo au ndo suluhu yake
   
 13. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,672
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
  Wewe naona umetumwa na mwovu kuondoa amani kwenye ndoa za watu, sasa unataka mtu aanze kumuhisi mumewe anatoka nje ili iweje jamani
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Haki ya Mungu unanisingizia.................!
   
 15. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mweee asante kwa somo zuri baba,wakati ukifika nitalifanya kazi!
   
 16. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  shule nzuri sana
   
 17. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,649
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  umejitahidi katika utafiti wako lakini nyingine mwanaume huwa anapanic anapoulizwaulizwa alipo au utarudi sa ngapi leo?
   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  lazima kutakuwa na tofauti mkuu...............
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mhhhhh......interesting...lol
   
 20. y

  yusra Member

  #20
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio ndo ukafanye kweli!
   
Loading...