Ukiona una vigezo hivi basi haujakamilika kiume

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
5,707
11,962
Unaume (Masculinity) ni kinyume cha uanamke (Feminity) na hivyo basi ili uonekane au uweze kukamilika then kuna vigezo au sifa kadhaa ambazo zinatakiwa kuonekana ili kuweza kudhihirika uwepo wake.

Zifuatazo ni baadhi ya dalili au viashiria vya mtu ambaye hajakamilika kuwa mwanaume.

1. Hasira au jazba. Ukiona mwanaume anaonyesha jazba au hasira katika mambo ambayo hayana ulazima wa kutumia hasira ni wazi huyu mwanaume anatumia zaidi hisia (emotions) na sio mantinki (logic).

2. Matumizi ya pesa hovyo. Mwanaume anasifa kuu ya kujiandaa kwa majukumu yajayo ili yakifika awajibike kama baba na sio kuwa na visingizio. Ukiona mwanaume ni mtapanyaji wa pesa na mali jua ana msingi mbovu eneo la uanaume.

3. Principles. Mwanaume huwa na misingi ya sheria na kanuni za uendeshaji wa maisha yake. Sasa sio sheria na kanuni za hovyo bali zile zenye faida kwake na kwa wale wanaomtegemea. Ni ngumu sana kwa mwanaume mwenye principles kupelekeshwa na mtu yoyote au mwanamke. Principles ni framework ya utu wake.

4. Kipato. Sifa ya unaume ni kuwa na kipato cha kuendeshea maisha. Ukiona hii sifa haupo nayo jua tayari unaume wako una dosari. Kipato chako kina akisi maisha yako. Utachagua aina ya kipato kukidhi mahitaji ya aina ya maisha uliyochagua asitokee mtu kukupangia otherwise.

5. Heshima kwa wanaume wengine. Heshima maana yake ni mipaka, mwanaume kamili huwa anajua mipaka ya kujibu wanaume wenzake kwa adabu na kutii pale ambapo anatakiwa kujifunza jambo asilolijua. Ujuaji, kiburi, dharau, kebehi, kibesi, ukorofi, ushari, makelele, kupandisha mori hizi zote ni ishara za kukosa heshima kwa wanaume wengine na matokeo yake huwa si mazuri, hata vitabu vya MUNGU vinatuambia hasira hukaa kifuani mwa mpunbavu.

6. Kumuweka mwanamke juu yako badala ya MUNGU. Kanuni ya asili ya uumbaji inaelekeza kuwa anaanza MUNGU, halafu mwanaume, halafu watoto. Ukiweka mwanamke juu yako kama mwanaume tayari uanaume wako unadosari.

7. Ulaji mbovu. Mojawapo ya sifa inayoambatana na uanaume ni pamoja na kula vyakula stahiki vya kiume ambavyo vinalinda afya ya mwili na kuiimarisha. Ukiona mtu hajali afya ya mwili wake kwa kula hovyo bila kufuata balanced diet lakini pia ana hatarisha afya yake kwa kula Junk food then hapa tunazungumzia mwanaume irresponsible. Afya yako si jukumu la mkeo au watoto ni jukumu lako personal usije mlaumu mwanamke wako.

8. Hekima au Busara. Mwanaume anatakiwa kuwa na moja kati ya hivi. Hekima ni asili ya uumbaji na ni bahati sana kuwa nayo, na huwa haipatikani kwa kupewa bali watu huzaliwa nayo. Busara ni hekima ya kuazima au kukopa. Busara hupatikana kwa kucopy au kuazima hekima ya walio na hekima.

Nitakupa mfano, huwa wanasema hata mpunbavu akikaa kimya huonekana ana hekima. So kukaa kimya kwa mpumbavu ni kuiga namna watu wenye hekima wanapoamua kukaa kimya wakitafakari sentensi fupi zenye ujumbe wenye suluhu ya changamoto au tatizo.

Hizi chache ni ishara za kukuonyesha kuwa umekamilika au haujakamilika eneo la uanaume. Zipo nyingine nyingi ambazo tutaendelea kuelimishana tukipata wasaa wa kuandika.

Asante.
 
🙆🏻‍♂️. Mwenyezi akusamehe!! Ndugu yangu jaribu kutafakari kwa undani zaidi labda utajuwa ni wapi umekosea.
Kujiamini kwa Mwanaume kunaanza na Mwanamke alienae sio unakua na Mwanamke hata kumtambulisha kwa watu ni mtihani vigugumizi kibao unamtungiatungia majina na vyeo vya uongo uongo unaogopa kusema Ni mtu wako watu watakupiga madongo, oa mke mzuri hata kumtambulisha usiwe na kigugumizi huyu ni mke wangu watu wenyewe wakimuona heshima inachukua nafasi jamaa ana Chuma kakamatia kisu kikali
 
Back
Top Bottom