Ukiona penye Upenyo: Usipaachie kama Unapamudu

Ukiona penye Upenyo: Usipaachie kama Unapamudu

Justus_August

Member
Joined
May 2, 2023
Posts
22
Reaction score
104
SEHEMU YA KWANZA:
July 2017 nilihudhuria kikao cha chama cha mchezo wa kuogelea Tz (TSA) kilichofanyika kwenye ukumbi wa Paparazi pale Hotel Sleep Way ~ Masaki. Kwa wakati ule nilikuwa ni muogeleaji mzoefu na part-time nilikuwa nikifundisha watu kuogelea but zaidi kwa wakati ule nilikuwa nimeamua kujikita kwenye huduma za Saikolojia kwenye vyombo vya habari na hasahasa redioni.

Kikao kilichelewa kuanza baada ya washiriki pamoja na viongozi wa Tanzania Swimming Association (TSA) kuchelewa kufika. Wale tulio wahi tuliona wametukosea heshima na baadhi walieleza hisia zao wazi wakati kikao kilipoanza. Kulikuwepo na mvutano wa kutosha viongozi wakiwa wakali huku coaches nao wakiwa juu. Kwa vile hakukuwa na maelewano hata baada ya viongozi kujieleza kilichowachelewesha, ikaamuliwa kuwa kikao kipangwe siku nyingine.

Wakati watu wakijandaa kuanza kutoka ukumbini nikaomba kusema jambo kabla watu hawajaondoka: kwa namna nilivyoishi kwa kumheshimu kila mmoja kwenye jamii ya waogeleaji wa Tanzania nilipewa hiyo nafasi na wengi walikaa/simama kwa utulivu kunisikiliza...

Nilianza kwa kuwashukuru wote kukubali kuwa kikao kipangwe siku nyingine (hii ilikuwa ni mbinu) badae nikawaomba kuwa angalau tujadili jambo moja kuliko kuwa tumekutana kwa ajili ya kuzodoana na kuondoka. Nikawagusia waliosafiri kutoka Mwanza na Arusha kuja kwenye kikao na kuonesha umuhimu wa kufanya jambo kwa siku hiyo. Watu wakaanza kukaa na maongezi yakaendelea kikao kikadumu kwa saa zaidi ya tatu.. tulihudumiwa bites na vinywaji na kuendelea na mipango: kubwa likiwa ni namna ya kuratibu mashindano ya CANA Zone 3 ya waogeleaji kutoka Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Baada ya kikao viongozi walinifuata na kunisifu kwa namna nilivyobadili upepo. Mmoja wa viongozi akaniuliza kuwa ninafanya kazi wapi... nikamjibu kuwa nafanya kazi na vituo vya habari. Akaniuliza kama ninafanya vipindi vya michezo, nikamjibu kuwa najihusisha na vipindi vya Saikolojia. Akashangaa maana alijua mimi ni mtu wa elimu ya michezo.

Alipofahamu kuwa taaluma yangu ni Saikolojia, akaniuliza kama naweza kuifundisha Saikolojia kwenye Mtaala wa kimataifa (IB Psychology). Nikasema sijawahi but ninaweza. Akaniambia jumatatu peleka CV yako...itaendelea..
IMG-20191014-WA0014.jpg
 
Wewe jamaa umeniacha pale UDSM, kila mara tukiwa kwenye vikao vya wanasaikolojia hukuacha kuongelea namna ulivyokuwa hodari kwenye kuogelea hadi nikawa nadhani umesoma BED PESS baadae ndo nikajuwa ni msaikolojia.

Tumekutana kwenye vikao kadhaa vya UDPSA tukiwa wote ni wahitimu tayari.

Hatukuwahi kuwa karibu kihivo lakini unanifahamu na zaidi nahitaji busara zako kuhusu issue za media, mimi nafanya kwenye redio na TV na vipindi ni mwendelezo (niseme ni vipindi vyangu japo sija vinunua lakini nafanya kila week na ni endlessly) kuhusu saikolojia na afya ya akili.

Nahitaji kujuwa je ulifaidikaje na vipindi vya redio?

Au ni kujenga jina tu? Na kama ni hivyo una mafanikio yeyote unayoweza kuyazungumzia kuwa yalitokana na wewe ku advocate saikolojia kwenye vyombo vya habari?

Naona ABC huku tukisubili sehemu inayo fuata ya story yako!

Karibu!
 
Hizi mbinu za kisaikolojia zinawafaa watu wenye matatizo ya afya ya akili!! Tulia andika bandika uzi watu tusome!! Itaendekea waachie watu wa jukwaa la burudani. Jukwaa la Tenda ni jukwaa serious saana.

Paw
Moderator
JamiiForums

Peleka uzi jukwaa la entertainment huko akadanganyane na story taller wenzie
 
Wewe jamaa umeniacha pale UDSM, kila mara tukiwa kwenye vikao vya wanasaikolojia hukuacha kuongelea namna ulivyokuwa hodari kwenye kuogelea hadi nikawa nadhani umesoma BED PESS baadae ndo nikajuwa ni msaikolojia.

Tumekutana kwenye vikao kadhaa vya UDPSA tukiwa wote ni wahitimu tayari.

Hatukuwahi kuwa karibu kihivo lakini unanifahamu na zaidi nahitaji busara zako kuhusu issue za media, mimi nafanya kwenye redio na TV na vipindi ni mwendelezo (niseme ni vipindi vyangu japo sija vinunua lakini nafanya kila week na ni endlessly) kuhusu saikolojia na afya ya akili.

Nahitaji kujuwa je ulifaidikaje na vipindi vya redio?

Au ni kujenga jina tu? Na kama ni hivyo una mafanikio yeyote unayoweza kuyazungumzia kuwa yalitokana na wewe ku advocate saikolojia kwenye vyombo vya habari?

Naona ABC huku tukisubili sehemu inayo fuata ya story yako!

Karibu!
Ninahifadhi uliyoibua kama na hoja na maswali! Nikiweka mwendelezo wa pili nitaomba upate nafasi ya kuupitia kwa kiasi fulani nitakuwa nimejibu baadhi ya hoja ila pia nitakuwa tayari kuyasemea yale ambayo yatakuwa nje ya nilichokwisha andika.

Nimefurahi kusoma kutoka kwako
 
Back
Top Bottom