Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
Kina cha fikara zako chazidi, chazidi wingi wa mawazo yako,
unawajali wenzako,kwa kuwatoa mchoko, Rutashubanyuma uwezo wako,umekutoa uliko,
Endelea...
Siyo rahisi kujua kilichoko ndani ya moyo wa mwanadamu
Mara nyingi kauli hupimika lakini kamwe siyo dira ya ukweli
Jicho laweza kurashiarashia nia lakini siyo kisemea moyo
Tabasamu laweza kukutikisa lakini lisitoboe la moyoni
Walakini magoti yanapomgonga-gonga jua kweli anajigonga.
Kilichoko moyoni ni kificho japo chakuchungulia-chungulia!
Mtihani wako ni kutafakari moyoni kwake kuna nini lakini?
Lengo ni kuujua moyo wake ili uthibiti hila kama zipo
Mwanadamu asilia yake ni usiri na usibwatuke na siha...
Walakini magoti yanapomgonga-gonga jua kweli anajigonga.
Moyo wa mwanadamu ni pasua kichwa na hata mmilikiwe kuzuzuliwa!
Anachodhani kipo moyoni leo, kesho kukikana yeye mwenyewe!
Moyo wa mwanadamu ni kizungumkuti kamwe usiuamini!
Kwani umekithiri hila na vitimbi, hivyo, kuwa tatanishi!
Walakini magoti yanapomgonga-gonga jua kweli anajigonga.
Mwanadamu hapendi kuanguka hivyo magoti kuyalinda vyema.
Sasa magoti yanapoweweseka ujue umemshika pabaya.
Hana ujanja wa kujitunzia siri hapo kwani hata wewe shahidi.
Chunga magoti yake na wala siyo moyo wake kuujua undani wake.
Walakini magoti yanapomgonga-gonga ujue kweli anajigonga.
N.B Haya siyo mashairi bali ni tenzi za nyimbo...........kwa hiyo hakuna swala la vina kushahibihana n.k kama ummu kulthum anavyopendelea na wengineo.....sentensi ya mwisho ni kibwagizo tu au chorus/kiitikio n.k
Rutashubanyuma we mkare ya hiyo yote ni kwa sababu ya ummu kulthum
Sasa Rutashubanyuma, last week ulisema utampenda yule tu anayekupenda. Big question ni utajuaje kama anakupenda; kwani maneno, wala macho yake havielezie yaliyo moyoni.
Na hiyo ya kujigonga, haiwezi kutafsiriwa as kuwaka tamaa tu?
[MENTION]Kina cha fikara zako chazidi, chazidi wingi wa mawazo yako,
unawajali wenzako,kwa kuwatoa mchoko, Rutashubanyuma uwezo wako,umekutoa uliko,
Endelea...
Ofcoz kujigonga kuko both sides, si kwamba wadada tu ndiyo hujigonga kwa wakaka.
Na ndivyo maumbile yanavyotupelekea,
kwani haiyumkini ukajigonga kwa mwenza wa gender ifananayo na yako.
"wayajua mahanjamu ya chuchu weyee ?"
Rutashubanyuma siku hizi kwa tenzi....mi waniacha hoi......
Judgement hapo kwenye nyekundu hebu tukumbushane.........kulikoni................