Ukiona dhuluma na ukanyamaza,Je dhamiri yako inasemaje?

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
638
Reaction score
1,043
👉🏾Dhamiri ni ile sauti ya Mungu rohoni inayotuambia ni sawa au si sawa, ni mema au ni mabaya. Ni muhimu inatufundisha kutenda haki, na hutoka kwa Mungu mwenyewe, kama ilivyo katika Warumi 2:15, ambapo inasema; "Kwa maana ni ishara ya kazi ya sheria ya Mungu iliyo katika mioyo yao, wakijua kuwa kile wanachokifanya ni kibaya, kwani dhamiri zao zinawashuhudia, na mawazo yao yanawashitaki au kuwatetea.

👉🏾
Dhamiri ni mwongozo wa ndani unaosimamia roho yetu, na ni sehemu ya mawasiliano ya kiroho kati yetu na Mungu, dhamiri inaweza kufifia ikiwa hatutaitunza au tunapozima sauti yake kwa manufaa yetu binafsi.

👉🏾Katika dunia hii inayozidi kuwa na shinikizo na vishawishi vingi, tunapata kuwa watu wengi wanakosa kutenda kwa haki kwa sababu ya hofu, tamaa, na shinikizo la kijamii. Mfano wa wazi tunauona katika hadithi ya Yesu alivyohukumiwa pasipo haki. Pilato alijua ukweli kuhusu Yesu na aliona kuwa hakufanya kosa lolote, lakini alikubali kumhukumu kwa sababu ya hofu ya kupoteza nafasi yake na nguvu zake.

Rejea Mathayo 27:24 inasema: "Basi Pilato alipokuwaona kwamba halitakuwa na faida lolote, bali kutakuwa na machafuko, alichukua maji, akajiosha mikono mbele ya umati, akisema, ‘Sina hatia katika damu hii; ninyi mnakiona.’" Hi

Mimi nakazia kwamba dhamiri za watu zinavyoshindwa kuongoza kwa sababu ya hofu ya kupoteza madaraka, na jinsi tunavyoweza kupuuza haki kwa manufaa ya kibinafsi,hivyo zinahesabiwa kuwa zimekufa.

👉🏾 katika maisha yetu ya kila siku,Tunashuhudia watu wakifanya maamuzi yasiyo ya haki kwa sababu ya shinikizo la jamii, nafasi zao, au faida binafsi. Ingawa wanajua ni nini kinachofaa, wanachagua kuacha dhamiri zao ziishe kwa hofu ya kupoteza yale wanayomiliki. Wengi wamekuwa wahadhiri wa vishawishi vya dunia hii, kama Pilato alivyokuwa, na hawajiulizi ikiwa wanatenda haki au la,Mfano rejea Jamii ya wajiitao Chawa,hawa hawajali hawafikiri lolote kama lina maumivu kwa wengine…!

👉🏾Mfano mwingine unaotufundisha kuhusu dhamiri ni usaliti wa Yuda,na Simon Petro. Yuda alikusudia kumsaliti Yesu kwa fedha, na alikubali kufanya hivyo licha ya kujua kuwa ni uovu. Mathayo 26:14-16 inasema: "Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale kumi na wawili, akaenda kwa wakuu wa makuhani, akasema, ‘Mtanipa nini niwapeleke kwa Yesu?’ Wakakubaliana kumlipa fedha thelathini.

Yuda aliona faida yake binafsi katika kufanya uovu, na hivyo akaacha dhamiri yake, akachagua usaliti kwa ajili ya manufaa ya kifedha. Ni mifano hai ya jinsi vishawishi vya haraka vinavyoweza kufanya watu wasikie sauti ya dhamiri yao na kutenda kwa njia ya kutotenda haki, hasa wakati wanapojikuta kwenye msukumo wa faida za haraka au tamaduni zinazowaelekeza kinyume na ukweli.

👉🏾Vilevile, askari waliosulubisha Yesu walikuwa tu wakifuata amri za viongozi wao, lakini walijua kuwa walikuwa wanatekeleza maamuzi yasiyo ya haki.

Rejea Mathayo 27:54 inasema: "Huyu hakika alikuwa Mwana wa Mungu!"….. Hata hivyo, walikuwa wamejaa roho ya kutii bila kuhoji, wakiendelea na kazi yao, licha ya ukweli kwamba Yesu alikuwa mnyonge na hana hatia. Huu ni mfano mwingine wa jinsi dhamiri inaweza kufifia kwa sababu ya kutii tu amri za wengine bila kujiuliza kuhusu haki au ukweli wa jambo zima.

👉🏾Katika mazingira ya leo, tunaweza kuona mifano mingi ya watu ambao wanatii amri au maelekezo yasiyo ya haki kwa kuogopa athari za kupinga. Hii ni tabia inayodhoofisha dhamiri, kwa kuwa tunakuwa na hofu ya kupoteza mali, heshima, au nafasi zetu. Mara nyingi, dhamiri inahitajika zaidi wakati wa shinikizo, lakini wengi wetu tunafunga masikio kwa sauti yake ili tu kufaidika na vishawishi vya dunia.

Yohana 10:27 inatufundisha: "Kondoo wangu husikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata."

Yesu anatuambia kuwa wale wanaomfuata, husikia sauti yake na kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu. Lakini swali ni, je, tunasikiliza sauti ya Mungu, au tunafuata sauti za ulimwengu zinazotuongoza kinyume na ukweli?

1 Timotheo 4:2 inasema: "Watu hawa wanadanganywa na roho za udanganyifu na mafundisho ya mapepo."
Tunaona jinsi vishawishi vya duniavinavyoweza kutufanya tuishi kwa njia zisizo za haki, na kutupotosha kutoka kwa dhamiri yetu.

Katika Warumi 12:2, Paulo anatufundisha: "Nanyi msifanane na ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kutii mwongozo wa akili zenu, mpate kujua mapenzi ya Mungu, yaliyo mema, yaliyokubalika, na yaliyo kamili."

Tunazidi kuona kuwa hatufai kuishi kwa njia za ulimwengu, bali tunapaswa kugeuzwa kwa kumtii Mungu na kutenda mema.

Dhamiri yetu inahitaji kuunganishwa na Mungu ili iweze kutuongoza kwa njia ya haki. Tunaweza kurejesha dhamiri yetu kwa kutafuta ukweli na kuwa waaminifu katika kutenda mema, bila kujali vishawishi vinavyotuzunguka. Tusikie sauti ya Mungu, na tusikie kama kondoo wake wanaosikiliza sauti ya mchungaji wao.

Mwanenu Chavalikungu nkiwa off napenda kuandika andika
 
Sasa tufanyeje ili dhamira itawale?
 
Sasa tufanyeje ili dhamira itawale?

Sasa tufanyeje ili dhamira itawale?
Ni dhamiri sio dhamira !!!

Basi kuamsha dhamiri mfu tunafanya hivi….!
  • Omba msamaha kwa yaliyopita.
  • Omba Mungu afufue dhamiri yako na akupe nuru ya kujitambua
  • Jiulize: “Je, nilifanya mema leo? Nilimuumiza mtu yeyote? Nilificha ukweli?”
  • Andika hisia zako. Mara nyingi kuandika hufungua milango ya dhamiri.
  • Tafuta mshauri, kiongozi wa kiroho, au rafiki mwenye hekima.
 
Back
Top Bottom