Ukimya wake unaniumiza

Ukimya wake unaniumiza

LAKI

Senior Member
Joined
Jun 12, 2013
Posts
100
Reaction score
37
Habarini za asubuhi wana Jamiiforums

Nombeni ushauri wenu, nina mpenzi . Jana nikauliza naomba kujua msimamo wako juu ya mahusiano yetu. Akajibu binafsi nina malengo na ndoto zangu kama unaona nakuchelewesha nakuruhusu nenda kwa mwingine atayekuoa haraka.

Sikumiibu chcochote na mawasiliano yakaishia pale. Kila mmoja yupo kimya, ukweli mimi naumia maana ninampenda,
sasa wadau nishaurini nianze tu mimi kumtafuta? Au niendelee kukaa kimya au nifanyeje?

Ushauri tafadhali- mahusiano yetu yana mwaka sasa.
 
Asee umeshajibiwa kama unaona utacheleweshwa na kumsubiria tafta mwingine, hapo akili kumkichwa. unaweza kua na malengo na maisha yako ndio, ila wewe amekupa nafas gan ndani ya nafsi yake?? Anayathamin maisha yake vizur, je wewe upoje moyoni mwake??? Vunja ukimya ujue hatma yako kwake halafu ukimsubir je atakua wako bado????? Sijaelewa kwa nin kakaa kimya either kuna kitu nyuma ya pazia kua muwazi
 
Sawa, pole sana...

Kwani yeye na wewe ni kama nani? wachumba au wapenzi wa kawaida TU?

Mliahidiana nini kwa muda gani? huo muda umisha pita au bado?

Ok, ni vizuri kujua mapema ili kuona mustakabali wako baadae..

subiri kama siku 3 usimtafute uone kama atakutafuta au lah!!
 
May be ulimuuliza muda ambao hakua vizuri. Jishushe ya ishe kuliko kuendelea kuumia
 
Tatizo mabinti wengi linapokuja suala la ndoa nyie mnachofikiria ni bonge la harusi na makorombwezo kibao ili muwakoge mashosti zenu, hamfikirii zaidi ya hapo. Kinachofuatia hapo ni kushinikiza ndoa kwa namna yoyote ikibidi kutega mimba na ndio maana ndoa nyingi hazidumu. Jamani wadada suala la ndoa sio kama maamuzi ya kununua chipsi, kwamba njaa ikikuuma pesa unayo unaingia kibandani kwa mangi unajikadiria tu. Watu tuna akili tofauti tofauti na huwa tunachukua muda tofauti tofauti kukisoma na kukielewa kitu so usione kama jamaa anakuzingua. Anaposema kama una haraka uolewe haimaanishi hakupendi no, ni kwamba kwa upande wake yeye kifikra hayupo tayari kwa hilo kwa sasa. Mwaka mmoja sio muda mrefu kiukweli, hasa linapokuja suala la maandalizi ya kujiandaa na ndoa. Waswahili walishasema mwenye pupa hadiriki kula tamu, sasa kama wewe unachotafuta ni ndoa tu "waoaji" wapo wengi tu.
 
Wanawake wa siku hizi ukitongozwa tu, baada ya siku mbili naomba kujua muafaka wa maisha, "WTF" mwafaka wa maisha si ningekuwambia siku ile ile nakutungoza.
 
Habarini za asubuhi wana JF!

Nombeni ushauri wenu, nina mpenzi . Jana nikauliza naomba kujua msimamo wako juu ya mahusiano yetu. Akajibu binafsi nina malengo na ndoto zangu kama unaona nakuchelewesha nakuruhusu nenda kwa mwingine atayekuoa haraka.

Sikumiibu chcochote na mawasiliano yakaishia pale. Kila mmoja yupo kimya, ukweli mimi naumia maana ninampenda,
sasa wadau nishaurini nianze tu mimi kumtafuta? Au niendelee kukaa kimya au nifanyeje?

ushauri tafadhali- mahusiano yetu yana mwaka sasa.

Unajuwa hata kama ulikuwa unatikisa kiberiti... angalia usitikise hadi vijiti vikamwagika
 
Wanawake wa siku hizi ukitongozwa tu, baada ya siku mbili naomba kujua muafaka wa maisha, "WTF" mwafaka wa maisha si ningekuwambia siku ile ile nakutungoza.

Muafaka wa dei wani unajulikana kuwa ni mabanduzi.. sasa in few days mtu anapotaka kuhamisha malengo majibu yake ndo hayo
 
Back
Top Bottom