Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Tokea kuanza kwa sakata la makontena ya mchanga wa Dhahabu sijasikia tamko lolote kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini Proff. Muhongo. Akiwa Waziri mwenye dhamana ya kusimamia wizara hiyo ilikuwa ni muhimu Watanzania kupata maoni yake. Wakati wa ziara ya Rais Magufuli na baadaye Spika wa Bunge Ndugai sikumuona Waziri Muhongo akiambatana nao katika ziara ya ukaguzi wa makontena hayo ya mchanga wa Dhahabu. Proff. Muhongo ni mwanagiologia mkubwa na maoni yake katika sakata hii na mchango wake ni muhimu.
Je Proff. anajua kinachoendelea na ameamua kuwa kimya ? Kwasasa naona kuna mwingiliano wa kikazi mkubwa hapa nchini kufuatia kauli ya Meneja TPA kuongea mbele ya Rais na Spika kuwa anajua zile kontena zina Dhahabu toka lini Meneja wa TPA akawa Geologist ?