Ukimya wa prof baregu juu ya mchakato wa katiba

Ukimya wa prof baregu juu ya mchakato wa katiba

jfmwaipopo

Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
26
Reaction score
20
Ndugu wana jf ni ukweli usiopingika kuwa taifa la tanzania lipo katika hali mbaya takriinaban katika maeneo yote. Leo hii ukimuuliza hata mtoto wa darasa la kwanza atakuambia kuwa hali ya maisha si nzuri kwani wazaz wanashindwa kuwapatia mahitaji yao muhimu kutokana na ugumu wa maisha unaotokana na kupanda kwa gharama za vyakula na nauli kuongezeka, matababu ya kubahatisha, wanafunzi kufeli na kuhitimu bila ya kujua kusoma na kuandika, shida ya maji na mambo mengine mengi yanatofanana na hayo.

Tukiacha itikadi zetu za kichama na kuutanguliza utaifa mbele utajua mambo yote hayo yanatokana na kuwa na katiba mbovu inayoshindwa kumtetea mwananchi wa chini kabisa ili naye afurahie maziwa na asali zilizopo nchini mwake. Katika hotuba ya majumuisho ya waziri mkuu haoni umuhimu wa kulipatia kipa umbele swala hili zito la mchakato wa katiba mpya na kubeza kuwa upinzani unapiginia hili kwa kutazama 2015. Ukitafakari kwa kina kauli hii inathibitisha kuwa kumbe hata wao wanajua kuwa katiba iliyopo inapendelea upande mmoja wa chama cha siasa ndio maana badala ya kufikiri kwa mapana juu ya kuwa na katiba mpya kiongozi mwandamizi anawaza seheu moja tu ya uchaguzi 2015 na hivyo kutoona umuhimu wa kuupa kipaumbele mchakato wa katiba.

Hali inayoendelea sasa kwa anayefuatilia mchakato huu katiba mpya kwa kutanguliza uzalendo wa taifa lake atakubaliana na mimi kuwa mchakato umechakachuliwa kwani wajumbe waliochaguliwa na wananchi wamefanyiwa mchujo na viongozi kata WDC ambao vigezo walivyotumia hakuna anayejua na kuwaacha wananchi katika hali kubwa ya kukosa imani na mchakato unaendelea hivi sasa. Nilifikiri kuwa kwa kuwa katiba ya wananchi uteuzi wa mwisho ungefanywa na wanachi wenyewe kuliko ilivyo hivi sasa ambapo viongozi wachache wa WDC ambao zaid ya asilimia tisini ni kutoka ccm ndio wanaofnya mchujo na hivyo kufanya mchakato mzima kubakwa na chama kimoja cha siasa.

Hili ni swala ambalo pinda na wabunge wa ccm hawapaswi kulibeba kwa ushabiki. Kiongozi wa kambi ya upinzani kalileta kama kipa umbele kwa sasa lkn pinda anabeza na wabunge wengine waliokosa uzalendo wanashangalia .Kama tutalibeba taifa hili kiushabiki ktk masuala mazito hatutafika popote.

Profesa Baregu ambaye ni mjumbe wa tume ya katiba na ndiye mwakilishi pekee wa chadema kinachonishangaza ni ukimya wake na ushirikiano wake kwa chama kilichomteua. Wakati mkt na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni akipambana na udhalimu huu profesa baregu yupo kimya kana kwamba haelewi kabisa kinachoendelea juu mchakato.Sasa nashindwa kuelewa ni kulewa nafasi hizi ndogo ndogo au anaona msimamo wa chama juu hili si sahihi.Kama kiongozi mahili tunayemwamini kwa uzoefu , umri na elimu yake atoe msimamo wake juu hiki kinachoendelea vinginevyo atajishushia sifa na heshima ailiyonayo kwa wananchi na chama chake.
 
Baregu anakula per diem ya kufa mtu ,sidhani kama hata cdm ipo moyoni kwake
 
awww anakula hela aongee nini sasa ........hauoni jamaa wa cuf kule znz ...........pesa bwana kila kitu
 
Nadhani hujawahi kuwa mjumbe wa tume...tume ina msemaji mkuu....kila mjumbe akianza kukiuka taratibu na misingi ya tume ni uvunjaji wa kanuni za tume....Baregu anasheshimu kanuni na taratibu za tume japo yaweza kuwa huwa anawapa dondoo na mambo yanavyokwenda viongozi wake wa Chama....
Tusi-politicize kila kitu...busara za Prof.Baregu kutoku-politicize hiki kitu...kunampa credit ya kufanya kazi na kugundua mengi ndani yake!
 
KWANZA KABISA NI KWAMBA WEWE HUMJUI VIZURI PROF BAREGU.
PILI YULE SIO MTU WA KULEWA HIVYO VIPOSHO VYA MIL 1, ananafasi ya kufundisha chuo chochote,kufanya utafiti sehemu mbali mbali hata angetaka uongozi huko chadema angepata mkubwa tu hata angetaka kugombea ubunge sehemu ambazo ni ngome ya chadema chama kingempitisha. hana njaa hizo ameamua kupumzika.

Taarifa zote akina mbowe na lissu wanazoongea kuhusu mchakato wa katiba mpya unafikiri wanazipata wapi?
Ni mjumbe gani wa katiba kaitisha conference yeye binafsi na kuelezea malalamiko ya mchakato huo? kwani si kuna wa cuf,nccr,tlp,udp wote wapo .
kuna utaratibu maalam kufikisha malalamiko ndio maana kuna mkurugenzi wa habari wa chama na wakuregenzi wengine, hao wanapoongea unafikiri Taarifa wanatoa wapi?
tumia akili.
 
CDM walikosea sana kupeleka jina la Prof Baregu,pesa imemfunga mdomo,amesaliti chama,hana tofauti na magamba.
 
Ni haraka mno kumhukumu, prof ni mtu makini sana na ndiye anakisaidia chama kupata taarifa muhimu be patient!
 
Ndugu wana jf ni ukweli usiopingika kuwa taifa la tanzania lipo katika hali mbaya takriinaban katika maeneo yote. Leo hii ukimuuliza hata mtoto wa darasa la kwanza atakuambia kuwa hali ya maisha si nzuri kwani wazaz wanashindwa kuwapatia mahitaji yao muhimu kutokana na ugumu wa maisha unaotokana na kupanda kwa gharama za vyakula na nauli kuongezeka, matababu ya kubahatisha, wanafunzi kufeli na kuhitimu bila ya kujua kusoma na kuandika, shida ya maji na mambo mengine mengi yanatofanana na hayo.

Tukiacha itikadi zetu za kichama na kuutanguliza utaifa mbele utajua mambo yote hayo yanatokana na kuwa na katiba mbovu inayoshindwa kumtetea mwananchi wa chini kabisa ili naye afurahie maziwa na asali zilizopo nchini mwake. Katika hotuba ya majumuisho ya waziri mkuu haoni umuhimu wa kulipatia kipa umbele swala hili zito la mchakato wa katiba mpya na kubeza kuwa upinzani unapiginia hili kwa kutazama 2015. Ukitafakari kwa kina kauli hii inathibitisha kuwa kumbe hata wao wanajua kuwa katiba iliyopo inapendelea upande mmoja wa chama cha siasa ndio maana badala ya kufikiri kwa mapana juu ya kuwa na katiba mpya kiongozi mwandamizi anawaza seheu moja tu ya uchaguzi 2015 na hivyo kutoona umuhimu wa kuupa kipaumbele mchakato wa katiba.

Hali inayoendelea sasa kwa anayefuatilia mchakato huu katiba mpya kwa kutanguliza uzalendo wa taifa lake atakubaliana na mimi kuwa mchakato umechakachuliwa kwani wajumbe waliochaguliwa na wananchi wamefanyiwa mchujo na viongozi kata WDC ambao vigezo walivyotumia hakuna anayejua na kuwaacha wananchi katika hali kubwa ya kukosa imani na mchakato unaendelea hivi sasa. Nilifikiri kuwa kwa kuwa katiba ya wananchi uteuzi wa mwisho ungefanywa na wanachi wenyewe kuliko ilivyo hivi sasa ambapo viongozi wachache wa WDC ambao zaid ya asilimia tisini ni kutoka ccm ndio wanaofnya mchujo na hivyo kufanya mchakato mzima kubakwa na chama kimoja cha siasa.

Hili ni swala ambalo pinda na wabunge wa ccm hawapaswi kulibeba kwa ushabiki. Kiongozi wa kambi ya upinzani kalileta kama kipa umbele kwa sasa lkn pinda anabeza na wabunge wengine waliokosa uzalendo wanashangalia .Kama tutalibeba taifa hili kiushabiki ktk masuala mazito hatutafika popote.

Profesa Baregu ambaye ni mjumbe wa tume ya katiba na ndiye mwakilishi pekee wa chadema kinachonishangaza ni ukimya wake na ushirikiano wake kwa chama kilichomteua. Wakati mkt na kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni akipambana na udhalimu huu profesa baregu yupo kimya kana kwamba haelewi kabisa kinachoendelea juu mchakato.Sasa nashindwa kuelewa ni kulewa nafasi hizi ndogo ndogo au anaona msimamo wa chama juu hili si sahihi.Kama kiongozi mahili tunayemwamini kwa uzoefu , umri na elimu yake atoe msimamo wake juu hiki kinachoendelea vinginevyo atajishushia sifa na heshima ailiyonayo kwa wananchi na chama chake.

Kama ungesikiliza hotuba ya Mh. Mbowe kwenye uzinduzi wa Kanda ya Pwani (Kibaha), basi ungeelewa ni nini kinacho endelea kati ya CHADEMA na Mwakilishi wa CHADEMA kwenye Tume ya Katiba Prof. Baregu. Vinginevyo usingerukia kwenye hitimisho. Wapo watu maalum kwa shughuli za Majukwaani, ndiyo maana wengine hawasikiki na haina maana kwamba hawafanyi kazi iliyo tarajiwa.
 
Neno uzalendo kwa watanzania ni msamiati. Hata hawa wanaopiga kelele kuhusu ufisadi na matumizi mabaya ya pesa, ni wachache sana wanaoweza kukataa mbadala wa kubadilisha maisha yao forever and ever in split second inayotumika kutaja jina lake na kuandikwa kwenye payslip.

Cheza na pesa!. Ukimuuliza atakupa majibu ya ki-layman na kusema yeye ni mjumbe tu utafikiri kama hana hata input yoyote kwenye mambo ya tume.

Ninafikiri hata anamshangaa Mwenyekiti wa CHADEMA kwa kauli yake ya kutaka CHADEMA ijitoe kwenye mchakato wa katiba.

Hebu angalia jinsi wanavyopata pesa yetu ya kodi na yeye akiwa mmojawapo hata hajalalamika.
Unajua kuwa wajumbe wa kamati ya katiba wanalipwa sh. 450,000= kwa siku na wamenunuliwa magari 60?

Kwa mwaka kila mjumbe kuvuna zaidi ya milioni 300/-

Wasio wajumbe yaani watumishi kutumia bilioni 4.3/-

Sh bilioni 2.0 kulipia nyumba wafanyakazi wa Sekretariati

Serikali imefanya kufuru ya kutenga Sh. bilioni 40/- kwa ajili ya wajumbe 34 wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba. Kwa mujibu wa kasma ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoko kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13.

Iliyopewa jina la Vote Number 8 (Fungu namba 8), wajumbe 34 wa tume hiyo wametengewa posho ya Sh. bilioni 10 watakayolipwa kwa kipindi cha mwaka mmoja jambo ambalo baadhi ya wabunge wamesema hawaridhiki na kuhoji serikali inatafuta kitu gani kwa tume hiyo.

Wajumbe wa kawaida wa tume hiyo kwa mujibu wa mchanganuo wa bajeti, watalipwa posho ya Sh. karibu 450,000 kwa siku lakini Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Tume fungu lao ni kubwa zaidi ambalo limeongezewa viburudisho na takrima.
Kwa mujibu wa taarifa za uchambuzi wa posho hizo, kila mjumbe kuanzia mwaka wa fedha wa Julai 2012 hadi Julai 2013, atakuwa amejikusanyia zaidi ya Sh milioni 294 jambo ambalo baadhi ya wabunge waliohojiwa na NIPASHE Jumapili walisema ni maajabu ya Firauni.

Pamoja na kuhakikishiwa kuwa na ukwasi mkubwa, pia wametengewa Sh. milioni 10 kwa ajili ya matibabu kwa wale ambao wameelezwa kuwa hawapo kwenye utaratibu wa kugharamiwa tiba na serikali.
Dau kubwa ambalo lipo kwenye bajeti hiyo kwa mujibu wa wabunge hao ambao wameomba majina yao yasitajwe, ni kutengwa Sh. milioni 250 zinazodaiwa zitatumika kwa ajili ya usafi na ulinzi wa ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Wajumbe hao 34 kutoka Bara na Visiwani wametengewa Sh milioni 10 kugharamia mazishi na kuwasafirisha wajumbe wa tume hiyo watakaofariki dunia wakati wakiwa kwenye mchakato wa kukusanya maoni.
Sambamba na hilo, tume hiyo imetengewa zaidi ya Sh. bilioni 10 kununua magari 56 ambayo sita kati yake ni Land cruiser heavy duty zenye mikonga zitakazofungwa vipaza sauti ili kukusanya watu watoe maoni yao na mengine 50 yatakuwa ni mashingingi ya kisasa maarufu kama V8. Kwa sasa tume hiyo inadaiwa kuazimwa magari kutoka Wizara ya Sheria na Katiba.

Baadhi ya wabunge waliliambia gazeti hili kuwa bajeti na idadi ya magari imepunguzwa badala ya kutumia Sh. bilioni 10 zitatumika Shilingi bilioni sita na kwamba yatakayonunuliwa ni magari 26 badala ya 56 lakini idadi ya Land cruiser heavy duty zitakazofungwa vipaza sauti haijabadilika.

Ofisi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba pia inatarajiwa kutumia Sh milioni 256 kugharamia umeme na maji ambapo kila huduma imepangiwa kugharimu karibu Sh milioni 128, yaani umeme Sh. 127,992,000 kadhalika maji nayo yamepangiwa kugharimu kiasi hicho na kuwafanya wabunge wachambuzi kuhoji sababu za gharama za umeme na maji kufanana.
Tume hiyo imetengewa posho ya takrima iliyoitwa hospitality services ya jumla ya Sh. milioni 300 huku simu za TTCL pamoja na gharama za nukushi (fax) zikifikia karibu Sh. milioni 127 wakati zile za mkononi zitawagharimu walipa kodi zaidi ya Sh. milioni 91.2.

WAFANYAKAZI WA SEKRETARIATI YA TUME

Kundi hili sio la wajumbe bali hawa ni watumishi wa ofisini watawala, wahasibu, makatibu muhtasi, wafagizi, wataalamu wa kompyuta, madereva na wengine nao wametengewa mafungu kadhaa ikiwemo posho ya kujikimu wakisafiri nayo ni Sh bilioni 4.3.

Kingine ambacho wabunge waliochambua Vote No 8 ama fungu hilo walisema kilichowashangaza ni kutenga Sh bilioni 2.0 kwa ajili ya kulipia nyumba za wafanyakazi wa Sekretariati ya Tume na kuhoji hivi wafanyakazi hao hawana nyumba jambo lililoelezewa na wawakilishi hao wa wananchi kuwa ni ulaji ambao wanasubiri kuuhoji wakati serikali ikiwasilisha bajeti hiyo.

Pia wafanyakazi hao ambao watalipwa posho ya Sh. 50,000 kwa siku wametengewa Sh. milioni 300 kwa ajili ya kununulia vifaa vya chai ambavyo havikuelezwa ni vitu gani pamoja na vitafunwa. Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaongozwa na Jaji Joseph Warioba ambaye ni Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Jaji Augustine Ramadhani.

Hilo ndilo tatizo kuuubwaaa sana.

Baregu alipendekezwa na CHADEMA kuwa mmoja wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Hakwenda wala hakuteuliwa ili aweze kuwa msemaji wa CDM kwenye Tume au hakuteuliwa ili aweze kuipa taarifa CDM kwa kila kinachoendelea pale TUME. na kama angetoa taarifa ningemuona ni mjinga sana asiyejua maana ya kazi yake.

Hivi kumbe ndivyo mnavyotaka afanye atoe taarifa kuhusu kinachoendelea pale TUME?

Hayupo pale kuitumikia CDM kwa hiyo hapaswi kutoa taarifa zozote za Tume kwenda CDM. Baregu yupo pale kuwatumikia Watanzania na anayepaswa kutoa taarifa za Tume ni Mwenyekiti wa Tume na amekuwa akifanya hivyo.

Ulidhani Prof.Baregu aliupata u profesa kwa kuiba wake za watu alikaa shule. ana akili kuliko Mbowe, Slaa na wengine wa aina yao.

Ana linda heshma na haiba yake. Hivi leo akianza kutoa siri za Tume kesho CDM ikashika Nchi unadhani watamuamini tena? watajua huyu kazi yake ni kutoa siri.

Mzee Baregu hana Njaa kama wale vijana waliopo kwenye mitandao ya simu pale VODACOM, AIRTEL, TIGO, TTCL ZANTEL waliopandikizwa na CDM ili kuratibu kila aina ya ujumbe unatoka kwa Viongozi au watu maarufu au mashuhuri wa CCM au Seriikalini.

Nawaambia vijana hao maisha yao yapo hatarini nina uhakika kuwa siku CDM wakichukua Nchi watakaopigwa risasi za vichwa ni wao maana CDM itawahofia kuwa wanaweza kununuliwa tena na kutoa taarifa.

Nawasihi vijana hao waaache kabisa mtindo wa hatari.
 
Nadhani hujawahi kuwa mjumbe wa tume...tume ina msemaji mkuu....kila mjumbe akianza kukiuka taratibu na misingi ya tume ni uvunjaji wa kanuni za tume....Baregu anasheshimu kanuni na taratibu za tume japo yaweza kuwa huwa anawapa dondoo na mambo yanavyokwenda viongozi wake wa Chama....
Tusi-politicize kila kitu...busara za Prof.Baregu kutoku-politicize hiki kitu...kunampa credit ya kufanya kazi na kugundua mengi ndani yake!

Hamna chochote, ingekuwa kweli Mzalendo hivyo angelikataa Gari la gharama kubwa na kutumia la gharama ndogo, kumbuka hata kama ni Mwenyekiti wa tume hulazimishwi kutumia hilo gari, angetuonea huruma walipa kodi na kuchukua dogo lake, pia asingekubali kulipwa pesa HARAMU na Serikali, kama kweli Mzalendo pia angeweza kuiambia Serikali ipeleke nusu ya Pesa HARAMU anayolipwa kusaidia Masikini, lkni wapi, Gari jipya la gharama anatumia na Pesa HARAMU anakula!
 
Yeye kama mjumbe wa tume ulitaka afanyeje? Kwa mawazo yako, yeye kama mjumbe wa tume unadhani anawajibika kwa tume au kwa CDM?

Hiyo siyo ishu, ishu ni kwamba amepewa gari jipya la mamilioni ya shilingi na analipwa pesa yakukufuru na yeye kama mpigania haki za wanyonge alipaswa kuonyesha mfano kwa kukataa hilo gari na kutumia la bei nafuu na kukataa pia pesa Haramu na badala yake kukubali pesa inayoendana na uhalisia na kinachobaki apeleke kusaidia Masikini, lkn wapi Pesa gari na marupurupu mengine anachikichia halafu mkataba ukiisha utamuona Majukwaani akiimba wimbo CCM Mafisadi, kumbe anachosahau ni kwamba hata yeye ni FISADI pia!

Back
Top Bottom