Ukimya wa prof baregu juu ya mchakato wa katiba

Ukimya wa prof baregu juu ya mchakato wa katiba

Hilo ndilo tatizo kuuubwaaa sana.

Baregu alipendekezwa na CHADEMA kuwa mmoja wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Hakwenda wala hakuteuliwa ili aweze kuwa msemaji wa CDM kwenye Tume au hakuteuliwa ili aweze kuipa taarifa CDM kwa kila kinachoendelea pale TUME. na kama angetoa taarifa ningemuona ni mjinga sana asiyejua maana ya kazi yake.

Hivi kumbe ndivyo mnavyotaka afanye atoe taarifa kuhusu kinachoendelea pale TUME?

Hayupo pale kuitumikia CDM kwa hiyo hapaswi kutoa taarifa zozote za Tume kwenda CDM. Baregu yupo pale kuwatumikia Watanzania na anayepaswa kutoa taarifa za Tume ni Mwenyekiti wa Tume na amekuwa akifanya hivyo.

Ulidhani Prof.Baregu aliupata u profesa kwa kuiba wake za watu alikaa shule. ana akili kuliko Mbowe, Slaa na wengine wa aina yao.

Ana linda heshma na haiba yake. Hivi leo akianza kutoa siri za Tume kesho CDM ikashika Nchi unadhani watamuamini tena? watajua huyu kazi yake ni kutoa siri.

Mzee Baregu hana Njaa kama wale vijana waliopo kwenye mitandao ya simu pale VODACOM, AIRTEL, TIGO, TTCL ZANTEL waliopandikizwa na CDM ili kuratibu kila aina ya ujumbe unatoka kwa Viongozi au watu maarufu au mashuhuri wa CCM au Seriikalini.

Nawaambia vijana hao maisha yao yapo hatarini nina uhakika kuwa siku CDM wakichukua Nchi watakaopigwa risasi za vichwa ni wao maana CDM itawahofia kuwa wanaweza kununuliwa tena na kutoa taarifa.

Nawasihi vijana hao waaache kabisa mtindo wa hatari.

Acha kuzunguka, mbona Gari la mamilioni hakulikataa, wakati alikuwa na uwezo huo?

 
Jamani huyu mtu anawajibika kwenye tume husika kwa sasa. Haiwezekani akaanza kuongea ovyoovyo maendeleo ya katiba mpya wakati naye anamwenyekiti wake. Kumbuka alipokuwaanaanza kazi hii aliapa kuwa msiri. Akikengeuka tu keshokutwa atatakiwa kutetewa mahakamani. Mwacheni afanye kazi yake kama mjumbe siyo kama mtu wa CHADEMA. Mabere Marando anakazi nyingi siyo aende kutetea hata kesi zisizo za msingi God bless TZ.
 
Tulieni acheni fitna zenu mzee Baregu ndio kwanza anapaua vigae nyumba yake halafu mnakuja hapa na vidomodomo vyenu!! na hiyo kadi yenu atawatupia usoni mkiendelea na makelele kama kuku anayekumbusha afunguliwe banda asubuhi.
 
Hiyo siyo ishu, ishu ni kwamba amepewa gari jipya la mamilioni ya shilingi na analipwa pesa yakukufuru na yeye kama mpigania haki za wanyonge alipaswa kuonyesha mfano kwa kukataa hilo gari na kutumia la bei nafuu na kukataa pia pesa Haramu na badala yake kukubali pesa inayoendana na uhalisia na kinachobaki apeleke kusaidia Masikini, lkn wapi Pesa gari na marupurupu mengine anachikichia halafu mkataba ukiisha utamuona Majukwaani akiimba wimbo CCM Mafisadi, kumbe anachosahau ni kwamba hata yeye ni FISADI pia!

Hoja yako hii hata Mh. Mbowe uzalendo ulimshinda baada ya miezi sita akaliomba tena gari lake KUB lakini kabla ya hapo, alikuja na mkwala wa kiwango cha juu kwa hii statement,
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2011/2012


Utangulizi
Mnamo tarehe 21/06/2011 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2011/2012.

Pamoja na Bajeti ya Serikali kukubali na kuzingatia baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani CHADEMA kama vile ;
a) Kupunguza kodi na tozo mbalimbali kwenye mafuta ya petrol na dizeli.
b) Kupunguza kiwango cha faini za makosa ya barabarani kutoka shilingi 300,000/50,000 hadi kufikia ukomo wa shilingi 30,000.
c) Kufuta leseni za biashara kwenye Majiji,Halimashauri za Wilaya na Vijiji.
d) Kufuta misamaha ya kodi kwenye makampuni yanayotafuta mafuta na gesi Nchini.
e) Kuongeza pesa kwenye bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kwa kuhakikisha kuwa kodi ya skills development levy 2/3 inapelekwa kwenye bodi kwa ajili ya Mikopo.

Katika kupitisha bajeti hiyo wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani wa CHADEMA tuliamua kupiga kura za HAPANA kwenye mapendekezo hayo ya Serikali kutokana na sababu mbalimbali na haswa hizi zifuatazo;
1. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuondoa posho za vikao (sitting allowances) kwenye mfumo wa malipo ndani ya serikali.
2. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa magari yote aina ya “Mashangingi” yanayotumiwa na viongozi na watumishi wa umma yauzwe kwa mnada ndani ya miezi sita na viongozi hao wakopeshwe magari kwa ajili ya kufanya majukumu yao mbalimbali.
3. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kufuta/kupunguza misamaha mikubwa ya kodi ambayo Makampuni ya Madini yanapata ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
4. Serikali imekataa kuingiza pensheni kwa ajili ya wazee wote nchini ya shilingi 20,000 kila mwezi ili kuweza kuwapunguzia ukali wa maisha wazee wetu .
5. Serikali imekataa Kufuta/kuondoa misamaha ya kodi kwa kipindi cha miaka 10 kwenye maeneo maalum ya uwekezaji (EPZ).
6. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa tunapunguza gharama za safari na haswa kuhakikisha kuwa ni viongozi wakuu na wenzi wao tuu ndio waruhusiwe kusafiri kwa kutumia daraja la kwanza (first class) ambao ni ;


  • Rais
  • Makamu wa Rais
  • Waziri Mkuu
  • Spika
  • Jaji Mkuu

Mawaziri wasafiri kwa kutumia daraja la pili (bussines class) na viongozi wengine wote wa umma na watumishi wa umma wakiwemo wabunge wasafiri kwa kutumia daraja la kawaida (economy class).

Pia misafara ya viongozi wakuu ipunguzwe ili kupunguza gharama za kuhudumia misafara hiyo pindi wanaposafiri nje ya Nchi.

Hitimisho.


  1. Tumeamua kumwandikia katibu wa Bunge barua ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhuriona kwa ajili ya posho na wabunge wa CHADEMA hawatasaini fomu za posho.
  2. Kuhusu magari, kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe ameamua kurejesha gari yake aina ya “Shangingi” alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada.

Tunawataka wabunge wengine waunge mkono hoja hizi kwa masilahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na ;
………………………
Mhe. Freeman A. Mbowe (Mb),

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni

21 Juni 2011

  • Baada ya muda kupita aliamua kula matapishi yake lakini akaja na mbinu ya medani za kivita na kusema,
Kufuatia tuhuma zilizo elekewa kwake juu ya matumizi shangingi la kambi ya upinzan mbowe alikua na haya yakusema:

"Mimi nilikataa gari kwa kipindi cha miezi sita na nikawa natumia gari langu kwa shughuli zote za vikao vya bunge,lakini nataka umma uelewa kuwa kwa nafasi yangu natakiwa kulipwa posho ya madaraka sh 200000 kila mwezi,kupewa nyumba ya kuishi ikiwa samani zake.

Ila mpaka sasa sina nyumba ya serekali,wala mlinzi,wala kulipwa fedha za mawasiliano,vyote natumia fedha zangu...kama ningetaka ningedai mambo mengi ambayo natakiwa kupata lakini kulingana na hali ya uchumi wa nchi ni lazima nitumie fedha zangu ili kunusuru uchumi" alisema.

Source: Tanzania daima 22 june, 2012​

Mpaka ninaandika hapa, Mh. Mbowe anatanua na gari lake la KUB kama taratibu za 'kifisadi' zilivyo.

Hawa ndiyo wanasiasa wetu. Ukitaka ukubali, ukitaka ukatae.​

 
Hoja yako hii hata Mh. Mbowe uzalendo ulimshinda baada ya miezi sita akaliomba tena gari lake KUB lakini kabla ya hapo, alikuja na mkwala wa kiwango cha juu kwa hii statement,

  • Baada ya muda kupita aliamua kula matapishi yake lakini akaja na mbinu ya medani za kivita na kusema,

Mpaka ninaandika hapa, Mh. Mbowe anatanua na gari lake la KUB kama taratibu za 'kifisadi' zilivyo.

Hawa ndiyo wanasiasa wetu. Ukitaka ukubali, ukitaka ukatae.​


Ndio maana mimi nasema Chagua Fisadi Bw. Lowasa, hao wengine wote wasanii tu, angalau Fisadi Bw.Lowasa kila mtu anajua kwamba amepiga Hela lkn anarudisha kwa kiasi fulani kwa kuwekeza kwenye jamii, na pia Mchapa kazi haijapata tokea Tanzania!

Fisadi Bw.Lowasa Uraisi 2015 TZ!


 
Anayelalamikia UFISADI Hajapata nafasi - Kardinali Pengo!

Ni hatari sana kwa watu tuliowategemea kufanya kama anavyofanya baregu. Njaa manamalegeza. Ukiona mtu kastaafu halafu kaomba kuendelea ujue hapo kuna tatizo la kuishi! Mdomo unafungwa
 
Ndio maana mimi nasema Chagua Fisadi Bw. Lowasa, hao wengine wote wasanii tu, angalau Fisadi Bw.Lowasa kila mtu anajua kwamba amepiga Hela lkn anarudisha kwa kiasi fulani kwa kuwekeza kwenye jamii, na pia Mchapa kazi haijapata tokea Tanzania!

Fisadi Bw.Lowasa Uraisi 2015 TZ!


Hahahaha! Huo ni utashi wako mkuu.

Hujasikia wakisema kuwa wao tayari wana rais wa mioyoni mwao na wanachosubiri ni filimbi ya uchaguzi mkuu kupulizwa na tume ya uchaguzi!!
 
Kwa pesa anazolipwa baregu ni haki take kukaa kimya mwacheni Mzee Wa watu amalizie maisha
 
Baregu ni muadilifu kwani huwezi kutoe siri za tume wakati uliapa kuitii labda asingekubali uteuzi huo.
 
Back
Top Bottom