Ukimya wa Lowassa wakitia homa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Ukimya wa Lowassa wakitia homa Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Kichale

Member
Joined
Mar 12, 2015
Posts
16
Reaction score
7
Baada ya mchakato mzima wa Chama Cha Mapinduzi kumtafuta mgombea wake wa urais kwa mwaka 2015 kumalizika, huku ukigubwika na sintofahamu nyingi kutokana na rafu za waziwazi kuchezeka kwa moja ya mgombea wake ambaye ni Mhe Edward Lowassa bado ameendelea kuwa kimya na kutosema chochote na kuzidi kukipa maswali mengi chama chake.

Nguvu nyingi zilitumika ikiwa ni pamoja na kuvunja Kanuni, taratibu na sheria zilizojiwekea tangu kuundwa kwa chama hicho nia ikiwa ni kuhakikisha kinazima ndoto ya mgombea huyo. Nguvu hiyo ya ziada ilibidi kutumika baada ya kugundua nguvu kubwa aliyonayo mgombea huyo ndani ya chama hicho na kwamba hakuna hoja ya msingi ya kuweza kukata jina lake ndani ya Kamati Kuu.

Kama ilivyo ada miaka yote ya uchaguzi ndani ya chama hicho kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho, Kamati ya Maadili haina mamlaka ya kukata jina la mgombea awaye yoyote yule kwa kuwa kikanuni kazi hiyo hufanywa na Kamati Kuu tena kwa hoja za msingi.

Mwanasiasa Mkongwe wa chama hicho Ndugu Kingunge Ngombale Mwiru ametanabaisha vyema katika press aliyoifanya hivi juzi nyumbani kwake masaki na kuita waandishi wa habari kwa kuwaeleza kuwa kilichofanywa na CCM safari hii ni Uhuni, batili na si haki.

Kwa kuonyesha kutoridhishwa na kile kilichofanyika ndani ya Chama hicho, mamia ya Wanaccm wameanza kurudisha kadi za Chama hicho na kuhamia katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Tangu kuisha kwa mchakato huo wa kuteuliwa mgombea huyo wa CCM ni takribani wiki moja sasa ila Mhe Lowassa ameendelea kuwa kimya na kutozungumza lolote, ingawa aliita waandishi wa habari hivi majuzi nyumbani kwake jijini Dar es salaam na ghafla akaghairisha mkutano ule.

Habari za ndani zinasema kughairishwa kwa mkutano ule ghafla ni baada ya kuitwa na chama chake kuombwa wazungumze kwani inasemekana ana mpango wa kukihama chama hicho, ambapo inasemekana Mhe Lowassa hakuitikia wito huo.

Habari hizo ambazo zimekuwa zikitiliwa mashaka kuwa ni za kweli baada ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kushindwa kutangaza mgombea wake wiki iliyopita, ikisemekana bado wanafanya mazungumzo na Lowassa zimekuwa zikikichanganya CCM na kutumia kila namna kumfanya Mhe Lowassa kuachana na maamuzi hayo.

Baada ya jitihada za CCM kumwita wapate kuzungumza kufeli, wamekuwa wakitumiwa watu wa karibu wa Lowassa kumshawishi na kumshauri kama kweli ana mawazo hayo ayatupilie mbali kwani kitendo hicho kitamuondolea heshima yake kwa jamii au kumsababishia matatizo.

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), ukiendelea kuwa na kigugumizi juu ya nani atakaepeperusha bendera ya umoja huo, hivi juzi akihojiwa na waandishi wa habari ndani ya Colloseum Hotel Mhe James Mbatia amesema tayari wamempata mgombea ambaye ndio chaguo la watanzania na watakuwa tayari kumtangaza baada ya wiki moja.

Kila mtanzania macho yake na masikio vikisubiri kwa hamu zote kufahamu kama yanayovuma ni kweli ama lah. Kama ni kweli, ina maana Slaa na Lipumba wamekubali kumpisha Lowassa, nA kama sio kweli, ina maana Lowassa amekubali kushindwa kirahisi hivyo.

Ni jumatatu ama jumanne ya wiki ijayo tutapata kujua kama yaliyomo yamo, tuvute subira.
 
UKAWA wakimpokea Lowassa itajishushia heshima iliyopo ya kuwa kiongozi wa mapambano ya ufisadi. Wawe na Lowassa wasiwe na Lowassa, Magufuli ndiye atakayeshinda uchaguzi
 
UKAWA wakimpokea Lowassa itajishushia heshima iliyopo ya kuwa kiongozi wa mapambano ya ufisadi. Wawe na Lowassa wasiwe na Lowassa, Magufuli ndiye atakayeshinda uchaguzi

Aaah..! Kumbe ndicho ulichokua unamaanisha.
Jk ni chaguo la Mungu.. Na hatimae watanzania tumeona anavyoimaliza ccm. Asante Jk
 
Aende ukawa awe mwanachama wa kawaida na siku ya kumtangaza mgombea wa ukawa basi yeye amuunge mkono bila kusema chochote
 
UKAWA wakimpata Lowassa wanachukua nchi kwa ushindi wa kishindo


Saa 2 asubuhi wanashinda kwa Landslide victory... tht will leave no questions & doughts to CCM kuwa wameshindwa... Lowassa ndio habari ya kila kona ya Tanzania na nje ya Tanzania... very genius political dude, strategic, political tactician and technician, atasomba wananchi kura zooooooooote ukawa... wait & see, historia mpya ya nchi yangu naiona
 
Mzee ana ulinzi mkali kuliko mgombea mteule wa ccm...hata kuongea na media haruhusiwi...
 
UKAWA wakimpata Lowassa wanachukua nchi kwa ushindi wa kishindo

Na ni UKAWA hao hao waliomshutumu sana Lowasa kuwa fisadi wa Richmond......wao hujipambanua kama wasafi, iweje waamue kuingia katika viatu vya Lowasa fisadi?
 
Back
Top Bottom