Ukimya wa Lowassa unaitesa CCM na UKAWA

Watu wameanza kubadili mitazamo yao na fikra zao kwa lowasa kutokana na ukimya wake ngoja tuamgalie maisha mengine bana
 
Ukiangalia mtiririko wa huu uzi,ukaona ujazo wa povu lililomwagika utagundua kivuli cha Lowassa kinatesa watu!
Nawahakikisha Lowassa akiongea inaweza kuwa msaada kwenu,mnaweza kupona roho zenu.

Hebu mpeni nafasi mzee wetu atuhutubie Jangwani!
 
Mkuu sio kwamba uchaguzi ndio ulikua maigizo?????
 
Katika kufungisha ndoa huwa wanauliza kuna mtu ana neno hawa wawili wasioane? EL alinyamaza na akaambiwa anyamaze hadi 2020 nampa hongera kwa ukomavu wa kisiasa kanyamaza
 
Wewe ndio unaumizwa ila sio siye. Lowassa kwasasa ni sawa na joka la kibisa. Lowasa hana sumu yoyote ya kuweza kumdhuru mtu.

Sasa hivi tupo na tingatinga limeshatia maguu mitaan watu wanafarakana.
 
Ukiangalia mtiririko wa huu uzi,ukaona ujazo wa povu lililomwagika utagundua kivuli cha Lowassa kinatesa watu!
Nawahakikisha Lowassa akiongea inaweza kuwa msaada kwenu,mnaweza kupona roho zenu.

Hebu mpeni nafasi mzee wetu atuhutubie Jangwani!

Wanaotakiwa kuongea si EL. Yeye alishamaliza kazi yake. Wanaopashwa kuongea ni chadema/ukawa wenye chama. El aliomba njia tu. Hana wadfa wowote chamani. Afterall huenda na daktari wake amemshauri apumzike.
 
ukawa hawana haja ya kuwaza.ccm ndio wahangaike.
 
mkuu waache bavicha wajifariji angalau kidogo mkuu,maana kipigo walichopata bado hawaamini
 
Ukifeli mfululizo kwenye fursa ulizowekeza inakubidi utulie na kutafakari
 
Alisema akishindwa atarudi munduli kuchunga ngombe wake.
Lini umeona mchunga ngombe akipewa nafasi ya kuongea na taifa?
Lini mchunga ngombe akatufanya tuwe tunaishi na kwa mashaka?
Ngombe wenyewe alionao amesema hawafiki 1000 sasa mchunga ngombe wa idadi hiyo kweli awe gumzo ktk nchi?
 
mkuu waache bavicha wajifariji angalau kidogo mkuu,maana kipigo walichopata bado hawaamini

Ndio ni pigo kwetu na kwenu,mmeiba kura, mmeiba waziwazi na ndio maana Lowassa kuwa kimya mnateseka,mnaweweseka!

Lowassa, rais wa mioyo ya watu!
 
hii mazingaombwe mlishafanya sana peleka huko. mara ni mteule wa mungu mara nabii katabiri ooh gwajima sijui nini. sasa unataka lowassa aseme nini wakati moyoni anajua mshindi ni magufuli. pamoja na kuutaka kufa kupona urais lowassa ni mtu wa amani. anachunga kauli. nyinyi wenye mahaba bila akili mnaweza vunja amani ya nchi.
 
Ukiangalia mtiririko wa huu uzi,ukaona ujazo wa povu lililomwagika utagundua kivuli cha Lowassa kinatesa watu!
Nawahakikisha Lowassa akiongea inaweza kuwa msaada kwenu,mnaweza kupona roho zenu.

Hebu mpeni nafasi mzee wetu atuhutubie Jangwani!
Ulifanikiwa vipi kutoroka? Wee pia una harufu ya IT team ya mzee! Naona wewe ndo umebaki msumbufu humu, unalia lia tu!
 
Kwa bara mambo ya uchaguzi tena wa urais yameshazikwa toka Magu aapishwe so hata akishinda anaongea ni wastage of time and energy.Hivi Kuna mtu mwenye akili timamu anasubiria kusikia Lowassa atasema nini kwa sasa?Wanaoteswa na ukimya wa Lowassa labda wale ULIPO TUPO maanake hawajui wataelekezwa kwenda wapi.
 
Reactions: nao
Ulifanikiwa vipi kutoroka? Wee pia una harufu ya IT team ya mzee! Naona wewe ndo umebaki msumbufu humu, unalia lia tu!

Sijawahi kutafutwa,labda nianze kutafutwa sasa and I am fine with that.
 
hAKUNA kITU kITU kIBAYA kAMA dharau, wewe unadharau wafugaji sio, hakuna shida, endelea

Kila kitu kinatafsiri mbili .
Tafsiri mbaya na tafsiri nzuri.
Ww umetafsiri vibaya maadiko yangu ingwa mm sikuwa na nia mbaya hiyo ulio iita ya dharau.
Maandiko hayo hayo ungetaka kuyatafsiri vizuri ungeweza kitafsiri.
Lakini pia huwezi kuwa nafkra nzuri kama hukupata malezi mazuri inawezekana umelelewa na mama wa kabu.
Kwahiyo umekulia ktk mazingira ya migogoro na misuguwano nandio athari inayo kuandama..
 
Hii ni hatari, na ndio ufikiri wa wana CCM walio wengi.wanahisi hatuelewi,wanahisi wanajua kila kitu zaidi ya kila mtu,wanahisi wanaweza kuzungmza au kutenda watakavyo na ikawa sawa tu.

Ukijaribu kuweka hisia zako wazi,mara moja wanaita Kovaaa,Kova njoo mshuhulikie huyu,mfungulie kesi,Muweke sero,msumbue sumbue atuondolee kelele.

Hii ni hatari kubwa!
 
Mtu anapo jenga hoja nivyema akajibiwa kwa hoja sivyema hoja ikajibiwa kwa kulalama.
Unapolalamika na kuhisi unaonewa unapunguza uwezo wa kifikira na kungamua mambo.
Nahili ndio tatizo nililo liseama huko nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…