figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Asilimia mbili ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI nchini yapo miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 ambapo ushamiri kwa vijana wa kike uko juu zaidi ya ule wa vijana wa kiume hasa katika umri wa miaka 23 hadi 24.
Hayo yamebainishwa na naibu waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Dkt Abdallah Posi katika mkutano wa wadau wa masuala ya vijana ambapo amesema kuna uwiano usio lingana katika mwitikio wa UKIMWI kidunia ambapo UKIMWI unasababisha vifo vingi kwa vijana balehe katika Afrika.
Imeelezwa kwamba Wasichana wana uwezo wa kupata maambukizi mara mbili zaidi ya wavulana ambapo kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa viashiria vya VVU na malaria 2011/2012, kiwango cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI miongoni mwa wasichana ni asilimia 6.6 wakati wavulana ni asilimia 2.8
Miaka mitano ijayo inatoa fursa kubwa kwa Tanzania kuendeleza juhudi na kupanua utekelezaji wa mikakati ya kumaliza janga la UKIMWI ifikapo mwaka 2030.