Caroline Danzi
JF-Expert Member
- Dec 19, 2008
- 3,713
- 1,263
Na vile vitambi vya mataputapu inakuwaje??tusidanganyane wakuu hapa, huwezi kupata kitambi kama huna pesa bwana ama kama mlo wako wa shida
Hii inanikumbusha siku moja nilikwenda kwenye duka la dawa hapa bongo. Wakati naongea na muhudum juu ya mahitaji yangu akatokea mtu mmoja mwenye umbile kubwa saana kwa maana ya kitambi. Yule muhudumu akaniweka pembeni kwanza. Yule bwana akanunua panadol tu, tena wakati ule ilikuwa shs 100 zinafungwa kwenye kiji-mfumko akaondoka zake. Hapo ndio muhudum akageuka kwangu kuendelea kunisikiliza, nikamwambia nimepona nakwenda. Kwahiyo kitambi kilimsaidia yule bwana ku-bypass foleni.Kitambi kinaleta kuaminika, hata ukitaka mkopo wa benki wanaangalia kwanza kitambi. Sasa wewe nenda na mifupa yako uone kama hujatolewa baro. Pili, wanawake wengi hasa wanavyuo huwa wanafagilia sana vitambi kwa imani kuwa pesa ipo, kitu ambacho kwa kiasi kikubwa ni kweli. Ukweli ni kuwa kufuga kitambi ni aghali kuliko hata kulea mke, aghalabu watu wenye vitambi ni watu wenye pesa. Mfano halisi, mkipotezana na mtu kwa muda mrefu na mkakutana ukiwa umenenepa atakuuliza; vipi mzee inaelekea mambo safi eeeh?
Mnaona sifa kuwa na vitambi,siku ukizimika ghafla,ndugu zako watasema 'si bure umetupiwa 'jini',mtaanza kutafutana uchawi na ndugu na majirani
Ondoa minyama uzembe hiyo!
Naona kitambi kinaninyemelea, nafanya jitihada kuhakikisha kisitokee, hivi ukimuona mtu mwenye kitambi;
1. Unasema mambo yake safi?
2. Unamuonea huruma kwa hali hiyo maana flexibility inakuwa hakuna na matatizo ya afya yanaongezeka?
3. Unatamani umshauri afanye mazoezi kupunguza hali hiyo?
4. Unatamani na wewe ukipate kama huna?
5. Au unawaza nini hasa?
Angalizo; Naomba ieleweke kwamba lengo si kuwakejeli watu wenye vitambi bali kuangalia mitazamo ya watu na namna bora ya kuboresha afya zetu.
Kwenye namba mmoja nagoma, 2, na tatu nakubali.Naona kitambi kinaninyemelea, nafanya jitihada kuhakikisha kisitokee, hivi ukimuona mtu mwenye kitambi;1. Unasema mambo yake safi?2. Unamuonea huruma kwa hali hiyo maana flexibility inakuwa hakuna na matatizo ya afya yanaongezeka?3. Unatamani umshauri afanye mazoezi kupunguza hali hiyo?4. Unatamani na wewe ukipate kama huna?5. Au unawaza nini hasa?Angalizo; Naomba ieleweke kwamba lengo si kuwakejeli watu wenye vitambi bali kuangalia mitazamo ya watu na namna bora ya kuboresha afya zetu.
Really?mhh mie nikimuona mtu mwenye kitambi namfananisha na maiti inayotembea