Ukimuona mtu mwenye kitambi

mimi ukiwa na kitambi hata sigeuki kukuangalia. Ki ukweli kama wanawake wanapenda vitambi maombi kwao yanahitajika.

na wew mwenye kitambi unajifia, ushindwe na ulegee, magonjwa ya moyo mnatembea nayo.
 
Usipojipenda mwenyewe huwezi kumpenda mtu mwingine.
Kitambi ni kutojipenda wewe na afya yako.
Unataka ule kila kitu,ilimradi kitaingia mdomoni.
Ni uroho na ufisadi.
Watu wengi sana wana mwili mkubwa lakin hawana kitambii,ila
pia kuna watu wegi wembamba ila matumbo makubwa sana,
Siyo sifa kuwa na tumbo angalia afya yako.
achana na kasumba za kizaire,tumbo kubwa ndo pesa.

Wana muzik wa zaire hapa bongo wana vitambi,je wana hela????
 
Kitambi kinaleta kuaminika, hata ukitaka mkopo wa benki wanaangalia kwanza kitambi. Sasa wewe nenda na mifupa yako uone kama hujatolewa baro. Pili, wanawake wengi hasa wanavyuo huwa wanafagilia sana vitambi kwa imani kuwa pesa ipo, kitu ambacho kwa kiasi kikubwa ni kweli. Ukweli ni kuwa kufuga kitambi ni aghali kuliko hata kulea mke, aghalabu watu wenye vitambi ni watu wenye pesa. Mfano halisi, mkipotezana na mtu kwa muda mrefu na mkakutana ukiwa umenenepa atakuuliza; vipi mzee inaelekea mambo safi eeeh?
 
Kitambi kinaleta kuaminika, hata ukitaka mkopo wa benki wanaangalia kwanza kitambi. Sasa wewe nenda na mifupa yako uone kama hujatolewa baro. Pili, wanawake wengi hasa wanavyuo huwa wanafagilia sana vitambi kwa imani kuwa pesa ipo, kitu ambacho kwa kiasi kikubwa ni kweli. Ukweli ni kuwa kufuga kitambi ni aghali kuliko hata kulea mke, aghalabu watu wenye vitambi ni watu wenye pesa. Mfano halisi, mkipotezana na mtu kwa muda mrefu na mkakutana ukiwa umenenepa atakuuliza; vipi mzee inaelekea mambo safi eeeh?
Hii inanikumbusha siku moja nilikwenda kwenye duka la dawa hapa bongo. Wakati naongea na muhudum juu ya mahitaji yangu akatokea mtu mmoja mwenye umbile kubwa saana kwa maana ya kitambi. Yule muhudumu akaniweka pembeni kwanza. Yule bwana akanunua panadol tu, tena wakati ule ilikuwa shs 100 zinafungwa kwenye kiji-mfumko akaondoka zake. Hapo ndio muhudum akageuka kwangu kuendelea kunisikiliza, nikamwambia nimepona nakwenda. Kwahiyo kitambi kilimsaidia yule bwana ku-bypass foleni.
Lakini naomba pia tukumbuke hapa kuna watu hawana vitambi lakini maumbile yao hayaendani na Body Mass Index (BMI). Haya link hii hapa kisirisiri tumbukiza weight na height yako utajiona uko wapi
BMI healthy weight calculator - Health tools - NHS Choices Hapa labda mzee wa JF ndio atakuwa sawa. (sijamtaja mtu hapo)
 
Mnaona sifa kuwa na vitambi,siku ukizimika ghafla,ndugu zako watasema 'si bure umetupiwa 'jini',mtaanza kutafutana uchawi na ndugu na majirani
Ondoa minyama uzembe hiyo!

Hapo kwenye 'red' nataka nikukumbushe kwamba anyejua ni lini utazimika ni MUNGU pekee iwe kwa mwenye kitambi na asiye na kitambi.
 
Naona kitambi kinaninyemelea, nafanya jitihada kuhakikisha kisitokee, hivi ukimuona mtu mwenye kitambi;
1. Unasema mambo yake safi?
2. Unamuonea huruma kwa hali hiyo maana flexibility inakuwa hakuna na matatizo ya afya yanaongezeka?
3. Unatamani umshauri afanye mazoezi kupunguza hali hiyo?
4. Unatamani na wewe ukipate kama huna?
5. Au unawaza nini hasa?
Angalizo; Naomba ieleweke kwamba lengo si kuwakejeli watu wenye vitambi bali kuangalia mitazamo ya watu na namna bora ya kuboresha afya zetu.

uzembe, ulaji ovyo na kutoujali mwili wako
 
Naona kitambi kinaninyemelea, nafanya jitihada kuhakikisha kisitokee, hivi ukimuona mtu mwenye kitambi;1. Unasema mambo yake safi?2. Unamuonea huruma kwa hali hiyo maana flexibility inakuwa hakuna na matatizo ya afya yanaongezeka?3. Unatamani umshauri afanye mazoezi kupunguza hali hiyo?4. Unatamani na wewe ukipate kama huna?5. Au unawaza nini hasa?Angalizo; Naomba ieleweke kwamba lengo si kuwakejeli watu wenye vitambi bali kuangalia mitazamo ya watu na namna bora ya kuboresha afya zetu.
Kwenye namba mmoja nagoma, 2, na tatu nakubali.
 
daaah kuna siku ilitokea kwenye basi; wale jamaa wanopanda ili kuuza dawa na sabuni kwa wasafiri, mmoja wao akaanza kunadi dawa zake mwishowe akatoa dawa akasema hii ni dawa ya kuongeza kitambi, kisha akaanza kutoa faida za kitambi, mojawapo akasema kitambia kitakusaidia kuaminika mjini!!! watu walicheka sana!!!!!!!!!!!!
 
IF you really want to lose weight, watching calories isn't tha answer. Eat healthy, natural, animal-free food and you won't need to diet. It is when the human body is filled with food that is not designed to cope with- animal flesh, diary products, etc that people put on weight. You wouldn't put sugar in your car tank and expect it to run. Give it the wrong fuel and you are asking for trouble.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom