Umeandika ukweli wako umemaliza.....acha tuparuane hapa,
Uzuri ni kwamba ndoa wala haziko sawa.
Aliemuoa mwajuma ndala ndefu sio sawa nawe ulioa mwanamke wa maana (ukimuambia habari za ustaarabu wa mwanamke wala hatokaa akuelewe kisa kaoa mwajndala ndefu anahisi kila mke yupo hivo)
Alieolewa na chapombe wake nae ukimwambia habari za ustaarabu wa mwanaume hakuelewi vile vile kisa ye kaolewa na famba.
kila mtu ana namna ya kuishi kwenye ndoa yake kwa staili yake na ikafanya kazi vema kabisa, ndio maana mbuzi anaishi kwa majani ila mbwa haishi kwa majani.