Ukimchimbia shimo mwenzako, jua utadumbukia mwenyewe. Na haya ndio yaliyotokea

Kulupango

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
288
534
Siku moja mshauri wa raisi alimueleza raisi kwamba waziri wako fulani bin fulani anakusema vibaya kwenye majimbo ya mkoa wake, na baya zaidi anatangaza kwamba kichwa chako ni kirefu na mdomo wako huwa unatoa harufu mbaya wakati wa vikao (kwa kifupi anasema kinywa chako kinanuka).

Basi baada ya mshauri kumueleza hivyo raisi, raisi aliumia sana.. akamuuliza mshauri haya maneno unayo nieleza ni ya kweli? Mshauri akasema 'hakika kabisa' mimi nimekua mshauri wako wa miaka mingi, hizi habari za wewe kunuka kinywa zimeenea majimboni.

Basi mshauri akaenda nyumbani kwake kuendelea na shughuli zake. Baada ya siku 5 kupita yule waziri Fulani bin fulani akaelekea mji mkuu ili aende kuonana na raisi na kumkabidhi ripoti ya majimbo mbalimbali, kabla ya kwenda ofisini kwa raisi akakutana na yule mshauri njiani.. mshauri yule akamueleza waziri 'Wewe umekuwa waziri shupavu sana ndugu yangu, kabla hujajielekeza kwa raisi naomba kwanza uje nyumbani kwangu nimeandaa chakula kwa kazi nzuri unazo zifanya huko mikoani, mimi kama mshauri wa raisi nakuomba uje tupate walau baraka nyumbani kwangu,

Basi siku hiyo waziri akajiandaa vizuri ili akitoka huko kwa mshauri moja kwa moja ajielekeze kwa raisi kumpatia ripoti za mikoa.

Huyu waziri alifika kwa mshauri na kukuta chakula kimeandaliwa vizuri, ambapo ilikuwa ni nyama ya kuchoma na kachumbari iliyojaa vitunguu.
Vyakula hivi vilitengwa makusudi na huyu mshauri wa raisi, basi bila kupoteza muda pale yule waziri na mshauri wakaanza kula, katikati ya chakula simu ikapigwa ya waziri ikimuhitaji kufika ofisi ya raisi mara moja, basi kwa haraka haraka yule waziri akainuka bila kunawa vizuri ile shombo ya nyama ya mbuzi ya kuchoma na yale mavitunguu, hivyo hivyo akajielekeza kwa raisi,

Alipofika ofisini kwa raisi akamkabidhi raisi ile ripoti ya mikoa, baada ya hapo wakazungumza mambo machache ya hapa na pale.. lakini wakati wakizungumza huyu waziri akawa kama mtu anaejifumba mdomo kwa mkono, kama anazuia kitu fulani hivi mdomoni..badi raisi kuona vile akaseme kimoyo moyo '"ahaaa kumbe zile habari ni za kweli, yakwamba huyu ananitangaza mimi nanuka kinywa si unaona anaongea namimi huku anajifumba mdomo".

Basi baada ya maongezi hayo mafupi raisi akampa yule waziri barua, akamueleza hii barua ipeleke idara fulani.. basi waziri bila shaka akainuka na kuelekea huko kwenye idara husika alikoelekezwa aipeleke barua hiyo,, kufika njiani akakutana na yule mshauri.. mshauri kwa haraka haraka na shauku akamuuliza vipi huko umezungumza nini na raisi? Kuna habari yoyote mpya raisi amekupa? ..

Waziri akasema nimefika kwa raisi tumezungumza mazungumzo ya kawaida tu, lakini baada ya mazungumzo amenikabidhi hii barua niipeleke idara fulani.. basi yule mshauri akauliza kwa shauku "Hivi hamjazungumza lolote tofauti na hayo? Waziri akasema hapana, basi yule mshauri akajua mule kwenye barua kutakuwa na neema ambazo raisi anampa waziri hizo neema, basi huyu mshauri akashikwa na tamaa ili azipate yeye, akamwambia waziri naomba hiyo barua niipeleke mimi kwenye hiyo idara husika, waziri akamwambia nitakupaje barua wakati mimi ndio nimeagizwa?

Mshauri akasema 'bana wewe' mimi ndio mshauri wa raisi lete hiyo barua niipeleke kwenye hiyo idara husika wewe nenda kapumzike, ujue mimi ndio mshauri wa raisi hivyo nitakuwa mwepesi pia kurejesha majibu ya barua kwa raisi, kwa hiyo naiyomba hiyo barua niipeleke mimi huko, wewe nenda kapumzike umechoka na safari, Basi yule waziri akaona isiwe shida, kwakuwa wewe ndio mshauri haya ipeleke hii hapa chukua.

Yule mshauri akaichukua ile barua na akaanza kuilekea kwenye idara husika, huku akiwa na shauku huwenda ni neema waziri anataka kupewa hivyo bora aipate yeye..

Alipofika kwenye idara husika akawapa ile barua, watu wa idara wakaifungua ile barua.. barua inasema ni Amri kutoka kwa rausi, tena imeandikwa kwa herufi kubwa kwamba "YEYOTE ATAKAE IFIKISHA HII BARUA HAPO KWENU MCHINJENI" NI AMRI KUTOKA KWA RAISI" ... muhuri na saini ya raisi.

Wale watu wa idara wakamkama mshauri hapo hapo wakamchinja.

Yule waziri baada ya muda kupita ikabidi aelekee kwenye ofisi ya raisi, alipofika ofisini raisi akastaajabu.. akamueleza, Waziri? Upo? waziri akajibu ndio nipo kwani kuna nini mkuu!.

Raisi akamueleza hembu kaa hapa kwenye kiti, waziri akakaa, raisi akamueleza barua niliyokupa umeifikisha kwenye idara husika? Waziri akajibu "nilipotoka hapa kwako nilikutana na mshauri njiani akaomba aipeleke yeye kwakuwa ndiye mshauri wa raisi, basi sikutaka mvutano nae nikampatia akaipeleka.
Raisi pale pale akaishiwa nguvu na kuseme "Nimeua nafsi isiyostahiki kifo"

Akamgeukia waziri, wewe ilikuaje ukawa unanitangaza majimboni yakwamba mimi nina kichwa kurefu na pia mdomo wangu unanuka? Ilikuaje? (Kwa ukali).

Waziri akashangaa! Akasema mimi..!! Hapana mkuu mimi sijakutangaza na wala habari hizo ndo kwanza nasikia kwako raisi wangu, sijahusika na habari hizo.

Raisi akasema, wewe ulikuja hapa ukawa unaongea namimi kwa kufumba kinywa ulikuwa unamaana gani? Waziri akajibu "ni kweli mkuu, mimi nilipotoka safari kabla ya kuja hapa niliitwa na mshauri kufika nyumbani kwake alikuwa ameandaa nyama ya kuchoma na vitunguu, nilikula khafla nikapokea simu kutoka ofisini kwako, ikabidi niinuke nikanawa haraka haraka nikaja kwako.. nilikuwa nafumba mdomo ili kuzuwia harufu mbaya ya vitunguu na nyama isije ikakufikia wewe raisi wetu ukaudhika. Sasa kule kufumba mdomo ni kujitahidi nisije kukukera kwa harufu yangu ya kinywa iliyojaa vitunguu na nyama ndio maana nikazuwia kwa mkono, lakini sikuwa na maana unayonieleza hapa.

Basi raisi akasema, mshauri alinieleza kwamba wewe unanisema vibaya kwenye majimbo, hivyo nilipanga nafasi yako nimpe yeye nawewe nikuuwe na hivi nazungumza nawewe tayari mshauri atakuwa ameshachinjwa. Shimo alilo lichimba limemfukia mwenyewe. Nenda kaendelee na kazi.
 
Husuda ni mbaya sana; na hayo ndiyo malipo yake.

Mtukufu mtume Muhammad (saw) alisema kuhusu husuda; "Jiepusheni na husuda kwani husuda inakula mema ya mtu jinsi moto unavyokula (unavyounguza) kuni".
 
Mbona tuhuma ndogo sana? Kunuka mdomo tu jamani?


Kwa kiongozi kunuka mdomo au kunuka kikwapa ni tuhuma kubwa kwani yeye mara kwa mara hukutana na watu mbalimbali, hali hiyo inaweza ikawa kero kwa watu wanaomzunguka nk.
 
Back
Top Bottom