Ukilewa sifa sana mwishowe unaanza kuropoka mambo yasiyo na mantiki kabisa

Jambo moja nafahamu ni kuwa una wivu mkuu dhidi ya huyu bwana,kadiri anavyozidi uikubalika ndivyo unavyozidi kuugua moyoni,nafuu yako ni watu kuacha kumsifia TL
Kweli mkuu huyu jamaa ana wivu ule wa kiafrika....hizi ngozi nyeusi sijui kwa nini tuliumbwa hivi
 
Huyu jamaa nimeona ni mpenda sifa sana na mpiga porojo.

Kitu kingine ni mtu anayependa sana attention kwenye media.

Hajui kama kuwa mbunge ni kukubali mfumo uliopo na mbaya zaidi anaitumikia serikali kwa njia ya kuishauri na kuipangia bajeti.

Hata kwa wale wanaamini kuna Mungu, sijawahi kuwaona wanatoa ushauri kwa shetani ambaye mfumo wake wa utawala ni tofauti na Mungu. Wanachofanya ni kukataa kushirikiana na mfumo wa shetani.

Leo anashirikiana na serikali bungeni halafu anaanza kupiga porojo za kusema hawezi kushirikiana na serikali ya kidikteta.

Leo anaanza kudai ACT-Wazalendo ni CCM B na eti CUF na CHADEMA tu ndio wapinzani. Jamaa amesahau kuwa alituambia pia kuwa CUF ni CCM B.

Huyu jamaa anashangaza kweli!

Well, nilitaka kusahau, sio huyu Tundu Lissu aliyeomba akaonane na Rais Magufuli ambaye amechaguliwa kwa mfumo asioutaka?

LINK>>Tundu Lissu: Tumeomba mwaliko wa Rais Magufuli tukampongeze Ikulu
 
Boss Nyani Ngabu Ni kipi kigeni alichozungumza Mh. Tundu Lissu? Mbona unajitoa Ufahamu? Maswali yako yote mbona Mh. Lissu alishayajibu? Unajishushia Heshima yako Mkuu. Uwe unaleta Mada zenye kujifikirisha. Mbona Rais anayasema sana haya. Mpaka anaenda mbali kuomba aombewe? Kwani Rais hajasema kila mahali ni Madudu? Kila mahali ni Feki? Den tupe maana ya Mfumo kwa wewe unaelewaje? Wewe ni mmoja wa Member wakongwe. Kama hauna Mada ya kuandika bora uwe mchangiaji au soma kimya kimya tu. Sio lazima uanzishe Mada isiyo na Mashiko. Hii ni moja ya Mada zako mbovu na pumba ulizoandika.

Huyu mwanasheria mkuu wa CHADEMA eti anadai kuwa anapinga mfumo uliomweka rais Magufuli madarakani.

Cha ajabu ni kwamba hicho chama chake kimeshiriki chaguzi zote za vyama vingi tokea 1995 na kama sikosei miaka yote ya uchaguzi mkuu walikuwa na mgombea urais.

Sasa eti leo anapinga mfumo uliomweka madarakani rais Magufuli. Kwa msingi huo pia alipinga urais wa Mkapa na Kikwete pia.

Kama anapinga huo mfumo uliopo kwa nini alimpigia kampeni Dkt. Slaa 2010 alipogombea urais?

Kama anapinga mfumo uliopo kwa nini yeye na wenzake walibadili gia angani na kumchukua Lowassa aliyetemwa na CCM kuwa ndo mgombea wao?

Kama Lowassa angeshinda hiyo 2015 sidhani kama angeupinga huo urais wake. Si ajabu angeteuliwa kushika nyadhifa mojawapo angekubali haraka haraka kwa bashasha na hamu ya mtoto aliyepewa jojo.

Eti anapinga mfumo uliomweka Magufuli madarakani....kwani yeye ni mfumo gani uliomweka huko bungeni?

Si kashiriki chaguzi ambazo zilifanyika chini ya katiba hii hii inayotumika sasa! Tume ya uchaguzi iliyomtangaza Magufuli kuwa ndo mshindi ndo hiyo hiyo iliyomtangaza yeye Lissu kuwa mshindi wa hicho kiti chake.

Kwa hiyo ina maana pia anaupinga mfumo uliompeleka yeye bungeni, siyo?

Siku zote hawa watu nimekuwa nikiwaambia kama wakitaka wawe na mamlaka ya kimaadili dhidi ya mfumo wa uchaguzi tulionao basi waache kushiriki chaguzi zinazofanyika chini ya tume ya uchaguzi iliyopo pamoja na katiba hadi hapo zitapopatikana mpya.

Zaidi ya hapo wataishia kuonekana ni wanafiki wafamaji tu!

Oh kingine...eti [yeye Lissu] anamwambia Magufuli kwamba kama anataka Lissu atumikie nchi hii basi tubadilishe katiba.

Kwani sasa hivi yeye Lissu kuwa mbunge hatumikii nchi hii kwa katiba hii hii anayoitaka ibadilishwe?

This guy is so overrated when truth of the matter is he is just a fair to middling lawyer!
 
Boss Nyani Ngabu Ni kipi kigeni alichozungumza Mh. Tundu Lissu? Mbona unajitoa Ufahamu? Maswali yako yote mbona Mh. Lissu alishayajibu? Unajishushia Heshima yako Mkuu. Uwe unaleta Mada zenye kujifikirisha. Mbona Rais anayasema sana haya. Mpaka anaenda mbali kuomba aombewe? Kwani Rais hajasema kila mahali ni Madudu? Kila mahali ni Feki? Den tupe maana ya Mfumo kwa wewe unaelewaje? Wewe ni mmoja wa Member wakongwe. Kama hauna Mada ya kuandika bora uwe mchangiaji au soma kimya kimya tu. Sio lazima uanzishe Mada isiyo na Mashiko. Hii ni moja ya Mada zako mbovu na pumba ulizoandika.

Hujajibu hoja.
 
Kaka huna cha kuongelea sikuhizi, mbona kuna vitu vingi sana vya kuongea vya maana kuliko kuanza kujadili mtu. Tanzania ni ya wote, si lissu tu. Weka ideas zako hapa, sio kuanza kumjadili mtu. Akili ya hivi, mnaijua nyie wenyewe
Wakati wa Kikwete, Lissu alikua hivi hivi ila huyu bwana hakuwahi kumuona amelewa sifa ila toka ameingia Ngosha mwenzie amekua mbaya wake
 
Huyu jamaa nimeona ni mpenda sifa sana na mpiga porojo.

Kitu kingine ni mtu anayependa sana attention kwenye media.

Hajui kama kuwa mbunge ni kukubali mfumo uliopo na mbaya zaidi anaitumikia serikali kwa njia ya kuishauri na kuipangia bajeti.

Hata kwa wale wanaamini kuna Mungu, sijawahi kuwaona wanatoa ushauri kwa shetani ambaye mfumo wake wa utawala ni tofauti na Mungu. Wanachofanya ni kukataa kushirikiana na mfumo wa shetani.

Leo anashirikiana na serikali bungeni halafu anaanza kupiga porojo za kusema hawezi kushirikiana na serikali ya kidikteta.

Leo anaanza kudai ACT-Wazalendo ni CCM B na eti CUF na CHADEMA tu ndio wapinzani. Jamaa amesahau kuwa alituambia pia kuwa CUF ni CCM B.

Huyu jamaa anashangaza kweli!

Haeleweki kabisa aisee.

Tatizo lake anapenda kufungua mdomo wake kama kasuku.

Anaunanga mfumo uliomweka Magufuli madarakani wakati ndo mfumo huo huo uliomweka yeye bungeni na ndo mfumo huo huo ambao chama chake huwa kinashiriki chaguzi chini yake.
 
with this sort of mentality, one wonders whether rubbing shoulders with the so called "exposed" actually makes you become "exposed"

lazima kuna kitu mbaya Lissu alishakufanyiaga.
hizi threads unazomfungulia si bure!!
Lissu atawatoa roho watu...ni mpinzani ndio maana anashunda mahakamani kila siku...yaani anatamka very happily kabisa. Hapa akina Nyni Ngabu roho zinateketea tu..hahahhahahaaa
 
Alichofanikiwa Lissu (na kwa hilo nampongeza) ni kuwaaminisha chadema, na wengine, kwamba yeye ni bingwa wa sheria na neno lake ndiyo sheria ilivyo. Yaani anachofanya ni "sheria-siasa", kwa maana ya kuchanganya sheria na porojo za siasa za kipinzani dhidi ya Serikali.

Yaani jamaa anafungua mdomo wake anaishia kujichanganya tu kila kona...kushoto..kulia...katikati...

Hivi kama Lowassa angeshinda naye asingemtambua kisa mfumo uliomweka madarakani?
 
Back
Top Bottom