Ukikopesha tarajia kukosa undugu, urafiki na hizo pesa

Mzee wa kusawazisha

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
1,251
2,000
Habari za mwamko wakuu humu ndani, nabandika uzi huu ili tulijadili kwa pamoja swala hili.

Binafsi Nina roho ya huruma pale mtu unakuja na shida serious unataka kuzima pesa. Nitolee mfano mzuri ndio ulionifanya niandike uzi huu..

Mwaka 2016 dada yangu mmoja baba na mama mmoja walikua wanacheza vikoba kwa kawaida siku ya kuvunja kama una deni hupati kitu. Sasa yeye alikwama Sana. Nilikua chuoni mwaka wa Kwanza aliniomba nimwazime pesa jumla Laki mbili na 80 ili akivuja tu vikoba atanirudishia.. Walivunja na hakunipigia hata simu nikasamehe,.

Mwaka 2017 alitetereka kidogo kibiashara kiasi hata kodi ya fremu anadaiwa Mwenye fremu alitaka atoe vyombo vyake ndani akanipigia simu nikiwa chuoni tena wiki ya UE Nika risk nikaweka bond simu ili nimuokoe nikamtumia laki 1 japo nilipata baada mwezi m1 na tulipatana baada ya wiki 1.

Mwaka Jana mwezi wa 12 Mwanzoni alinijia tena kuniazima pesa alikwama tena Kuna akaahidi baada ya wiki atanirejeshea Kuna pesa anaisubiri nikampa laki 1 na nusu. Wiki imepita akaomba nimwongezee tena nikampa 20000.
Wiki hii juma 3 anarudisha laki 1 badala ya laki na 70..nikatulia bila kuuliza nikajua Kesho yake angeniambia lolote.

Nami pia kwa Kua niliamini angenirudishia hiyo pesa nikakopa kwa mtu laki na nusu ili niendeleshe biashara yangu kwa bahati biashara hajaenda Sawa jamaa ananidai pesa yake Maana mda umeisha laki nimempa ila bado anataka yote. Na Dada yangu mpaka kufikia Jana nilibidi nifoke kwa Mara ya Kwanza kabisa maana na mimi nadaiwa..

Familia imekaa kikao kwa ajili yangu kisa nadai ela naambiwa Sina utu na sisaidii wenzangu na sisi ni ndugu wa kuzaana Nguvu zote zimeisha hapa sina la kufanya nikikumbuka niliyoyafanya kwa Dada yangu Toka mwaka juzi. Karibuni kwa upembuzi wa kina juu ya jambo hili nadai ili nirudishe deni najibiwa hivyo hapo.Sent using Jamii Forums mobile app
 

Heisenberg

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
1,115
2,000
Kuna dem mmoja aliniambia nimkopeshe elfu 20 atalipa next weekend yake. Nikampa. Sasa hivi anajibaraguza tuu hana cha kufanya. Nafuu angeniomba nisinge shindwa kumpa. Sasa natafuta namna ya kurudisha 20 yangu.

Hata indirect itarudi tuu

Push to Start
 

DullyJr

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
9,812
2,000
Shemeji kwanini unakuja kumtangaza dada yako huku?!!!yaani kaiona hii post hapa analia tu na umenipa kazi ya kumbembeleza usiku kucha hatulali

SIJAPENDA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
17,472
2,000
Aliyekwambia ndugu/rafiki anakopeshwa nani??

Ngojeni niwape trick moja ya kuishi na ndugu na jamaa.

Kwanza kabisa jijengee dhana kwamba ndugu/rafiki ni jukumu lako kumsaidia kama unaweza,ili likitokea jambo lolote usianze kuumia.

Hivyo basi,anapoomba msaada anajua kabisa uwezo unao wa kumsaidi,ila atakuja na lugha za kijanja,mara nikooeshe au niazime.wewe pigia tu mstari kwamba hii ni sadaka,badala yake lia hali ngumu kisha mwambie mimi sina ulichoomba nimfanyia kitu flani sasa hivi,nimebakiwa na nusu yake tu,ukimpa hiyo nusu nyingine ataenda kukomaa anapojua.

Mfano ile ya kwanza ungekuwa ulimpa 140 usingeumia leo kiasi hiki.hii ya pili ungempa 70 vivyo hivyo.

Na ukiona trend inazidi,yaani anakuzoea wakati mwingine unakaza hutoi.
 

Mushi92

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
3,912
2,000
Samahani lakini we jamaa ni kiazi.
Unakopeshaje pesa mpya...kabla haujapata mwafaka wa pesa ya nyuma?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom