Ukiishi Dar unakuwa bora kuliko wengine!

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,108
Hii ndio changamoto unayokumba vijana wengi kwamba kama ukiishi Dar es salaam unaonekana bora kuliko wengine wanaoishi mikoa mingine,sasa nilienda mkoa Fulani kama kawaida mida ya jioni baada ya shughuli za hapa na pale nikajisogeza kijiweni,basi yule aliyekuwa anasikilizwa na wote ni yule aliyewahi kuishi Dar sisi wengine tulionekana kama malofa!

Nilipoona dharau zinazidi ikabidi nijifanye natoa Simu (mfukoni nilikuwa na passport) nikaidondosha makusudi baada ya kudondoka chini kila mmoja akataka aione!

Wakakuta mtu mzima nimezunguka nchi kibao tu za kimataifa halafu nipo simple tu!hadi naondoka mkoa ule yule kijana wa Dar hakuonekana tena kijiweni[emoji2] ,Dar ni mkoa kama mikoa mingine na kuna watu Dar wanaoishi majumba mabovu kuliko mikoa mingine, vijana wa Dar mjirekebishe!ni hayo tu
 
ongera sana hasa hapo kwenye red
 

Kweli kabisa!
Kambi popote !
Maisha ni kujipanga tu!
Waache kukariri maisha!
 
Una sababu gani ya kwenda kijiweni na passport mfukoni? Au na wewe ulienda kuwakoga hao wa mkoani.
 
Tena uswazi mwing san huko dar
 
Hata mtuseme vipi hatuachi ng,ooo maana hiyo ndiyo mbinu yetu ya kuwapata mabinti wa mikoani kirahisi
 
Wanayo mikoa yao yakufanya hvyo hata wao wanajua
 
Sie wa dar hua tunaita Mikoa mingine kua ni Mikoani.
Yaani wewe huwezi kuishi Geita, Songwe, Njombe au Katavi kisha ukaniita mi wa dar eti wa Mkoani, utakua umefeli sana.
Ila mi nikikuita wewe hivyo ni sawa sawa kabisa,
Yote hii ni kwa sababu tu NIKO DAR.

Kuna mikoa ambayo watu hupenda kusikiliza story kutoka kwa mtu alietokea Dar wakiamini kua Dar kuna vitu vingi sana vya kusimulia. Wanaamini pia mkikaa kundi la watu wengi basi alietoka Dar ndio Mjanja hata kama huku dar alikua Lofa tu. Nilishawahi kupataga Demu mahali bure bure tu sababu tu nlivyoongea kidogo tu basi akazimika na lafudhi ya Dar, kwamba lafudhi zenye mchanganyiko wa kilugha za hapo mahali zimemchosha.

Asikuambie mtu bana kuhusu Dar, ingetokea nimezaliwa mkoa mwengine basi ningefosi tu nije niishi Dar.
 
Ivi hapo wenye tatizo vijana wa dar, au wa mikoani kuwapa hadhi vijana wa dar?
 
Nadhani vijana wengi wa mikoani mna inferiority complex mbele ya madogo wa Dar,Japo sio kweli kwamba ukiwa unatokea mikoani ni inferior mbele ya mtu wa Dar.

Mtu akitokea Dar sio kweli ni mjanja kuzidi wewe ila ni hisia tu nakukoswa kujiamini.Nimewahi kukaa na masela kibao wa Dar wapo wanjanja na wapo maboya just kama mikoani tu.

Nimezaliwa Mwanza sijawahi tamani kuzaliwa wala kuishi Dar.Maisha ni yaleyale.

Nauona hata huu uzi umeletwa kwa sababu ya inferiority complex pia.

No one can make you inferior without your consent.
 
Rubbish from daresalaam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…