Ukiiaminisha akili yako, haitakuangusha

Ukiiaminisha akili yako, haitakuangusha

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,648
Reaction score
10,844
Zig Ziglar alikuwa akikatiza mitaa ya jiji la New York alipokutana na omba omba wa aina yake. Alikuwa akiomba msaada wa dola moja, na kwa kila aliyeitikia ombi lake, alimzawadia penseli.

Ziglar alimpa dola moja ila hakukukubali kupokea penseli. Hakuwa na uhitaji nayo. Na kwa nini apokee kitu cha maskini? Aliona kama hiyo ni sawa na mtu mzima kunywa uji wa mtoto.

Aliweka noti ya dola moja kwenye sahani ya omba omba na kuondoka zake. Hatua chache baadaye, alikumbuka kuna kitu alipaswa kufanya kwa huyo mtu, ambacho hakuwa amekifanya. Haraka sana, aligeuza na kumwendea yule omba omba. "Nipe penseli yangu", alimwambia, "nilikupa dola moja kwa hiyo nipatie na mimi penseli yangu"

Bila hiyana, omba omba alichukua penseli moja na kumkabidhi Zig Ziglar. Akiwa na tabasamu zito, Ziglar alimtazama usoni omba omba na kumwambia, "Wewe ni mfanyabiashara kama mimi. Mimi ninamiliki kampuni inayowafundisha watu kufanikiwa, lkini wewe unajipatia kipato chako kwa biashara ya penseli"

Baada ya kumwambia hayo, aliondoka na kumwacha omba omba akiwa ameduwaa. Hakuwahi kuambiwa maneno kama hayo.

Miaka michache baadaye, Ziglar alimpata mgeni ofisini kwake. Ni yule yule omba omba aliyemkuta mitaa ya New York miaka ya nyuma, lakini safari hii hakuwa omba omba. Alikuwa "Somebody" mwenye heshima zake. Alienda kumshukuru kwa kumbadilisha maisha yake.

Ile kauli, "Wewe ni mfanyabiashara kama mimi" ilitosha kupindua fikra zake. Alipoondoka Ziglar, aliendelea kutafakari alichokisikia kiasi cha kumfanya aanze kujiona akiwa amevaa suti kama ya Ziglar, tena akiwa anongea na watu wanaoheshimika.

Siku alipoenda kuonana na Ziglar, siyo kwamba tu alikuwa amevaa kinadhifu kama Ziglar, bali pia alikuwa mmiliki wa kampuni iliyokuwa imeajiri watu kadhaa. Alimshukuru Ziglar kwa ukarimu wake uliomfanya kuwa alivyokua, mfanyabiashara.

Alimweleza kuwa katika watu wote waliompatia msaada, ni yeye peke yake ndiye aliyejali vya kutosha kiasi cha kumtamkia maneno ambayo ndiyo aliyoyahitaji kuliko kitu kingine chochote.

Japo aliendelea na shughuli yake ya kuombaomba hata baada ya kuambiwa hivyo, ile taswira iliyotengenezwa na kauli ya Ziglar haikumwachia. Iliendelea kukua ndani mwake mpaka hatimaye akachukua hatua zilizompa mafanikio. Maneno machache yalimgeuza kutoka kuwa omba omba hadi "bosi" anayemiliki kampuni.

Hiyo ni moja ya mifano jinsi imani ya mtu inavyoweza kumkwamisha au kumfanikisha. Alikuwa omba omba kwa sababu aliamini kuwa ndivyo alivyo, lakini alipoamini kuwa atafanikiwa, alifanikiwa.

Naamini watu wengi hawajui kuwa akili ni mtumishi wao mwaminifu. Chochote akiamonicho mtu, kiwe kizuri au kibaya, ndicho akipatacho.

Ukiiaminisha akili yako kuwa utakwama, usitegemee matokeo tofauti. Ukiamini kuwa utafanikiwa, ni suala la muda tu, hatimaye itakuwa hivyo.

Mwanasaikolojia mashuhuri kaandika, "Whatever the mind can conceive and believe, can achieve" na Biblia imeandika, "...aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo"

Sikumbuki kama imeandikwa kwenye kitabu cha 'The Magic of Thinking Big' au 'The Power of Your Subconscious Mind', nafikiri ni mojawapo ya hivyo vitabu. Ni habari ya mwanamke mmoja aliyepewa taarifa mbaya muda mfupi baada ya kujifungua mtoto wake wa kiume.

Mwanaye ndiyo kwanza alikuwa ametimiza miezi sita alipogundulika kuwa ana kansa. Daktari alimwambia kuwa angeweza kuishi kwa kipindi kisichozidi miezi sita. Maana yake, asingeweza kushuhudia mwanaye akitimiza umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja.

Nini jibu la mwanamke baada ya Daktari kumsomea hiyo hukumu? "Siwezi kufa kabla sijamwona mwanangu akiwa Chuo Kikuu!"

Miezi sita baadaye, bado alikuwa hai. Hata baada ya miaka ishirini, kmwanaye akiwa ameshakuwa mtu mzima kiumri, bado Kansa iliendelea kutii maamuzi yake. Alikufa mwanaye akiwa Chuo Kikuu mwaka wa pili.

Kwa kipindi chote hicho, ilibidi kansa ipewe likizo ndefu hadi shauku ya huyo mwanamke ilipotimia. Amini katika mambo mema. Wasaidie wengine kujiamini. Akili yako ipo makini kuchukua chochote uaminicho na kukifanyia kazi. Ukiilisha taarifa nzuri, itakuletea matokeo chanya.

Wasaidie na wengine kwa kuwaambia mambo mema kuwahusu. Kilichotokea kwa omba omba wa Marekani kinaweza kutokea kwa "Mnyonge" wa Tanzania. Ni "Genius" asiyejifahamu. Anahitajika mtu anayejali kwa kiwango cha kutosha, na kumthibitishia kuwa anamwamini ili na yeye aweze kujiamini.

Kujikubali kunamfanya mtu ajiamini. Kujiamini kunauweka huru "Ugenius" wa mtu.

Upo tayari kumwibua alau "Genius" mmoja aliyefukiwa na unyonge?

Barikiwa!
 
Aliweka noti ya dola moja kwenye sahani ya omba omba na kuondoka zake.

Hatua chache baadaye, alikumbuka kuna kitu alipaswa kufanya kwa huyo mtu, ambacho hakuwa amekifanya. Haraka sana, aligeuza na kumwendea yule omba omba.
"Nipe penseli yangu", alimwambia, "nilikupa dola moja kwa hiyo nipatie na mimi penseli yangu"

Bila hiyana, omba omba alichukua penseli moja na kumkabidhi Zig Ziglar.

Akiwa na tabasamu zito, Ziglar alimtazama usoni omba omba na kumwambia, "Wewe ni mfanyabiashara kama mimi. Mimi ninamiliki kampuni inayowafundisha watu kufanikiwa. Lakini wewe unajipatia kipato chako kwa biashara ya penseli"

Baada ya kumwambia hayo, aliondoka na kumwacha omba omba akiwa ameduwaa. Hakuwahi kuambiwa maneno kama hayo.

Miaka michache baadaye, Ziglar alimpata mgeni ofisini kwake. Ni yule yule omba omba aliyemkuta mitaa ya New York miaka ya nyuma, lakini safari hii hakuwa omba omba. Alikuwa "somebody" mwenye heshima zake. Alienda kumshukuru kwa kumbadilisha maisha yake.

Ile kauli, "Wewe ni mfanyabiashara kama mimi" ilitosha kupindua fikra zake.
Alipoondoka Ziglar, aliendelea kutafakari alichokisikia kiasi cha kumfanya aanze kujiona akiwa amevaa suti kama ya Ziglar, tena akiwa anongea na watu wanaoheshimika.

Siku alipoenda kuonana na Ziglar, siyo kwamba tu alikuwa amevaa kinadhifu kama Ziglar, bali pia alikuwa mmiliki wa kampuni iliyokuwa imeajiri watu kadhaa.

Alimshukuru Ziglar kwa ukarimu wake uliomfanya kuwa alivyokua, mfanyabiashara.

Alimweleza kuwa katika watu wote waliompatia msaada, ni yeye peke yake ndiye aliyejali vya kutosha kiasi cha kumtamkia maneno ambayo ndiyo aliyoyahitaji kuliko kitu kingine chochote.

Japo aliendelea na shughuli yake ya kuombaomba hata baada ya kuambiwa hivyo, ile taswira iliyotengenezwa na kauli ya Ziglar haikumwachia. Iliendelea kukua ndani mwake mpaka hatimaye akachukua hatua zilizompa mafanikio.

Maneno machache yalimgeuza kutoka kuwa omba omba hadi "bosi" anayemiliki kampuni.

Hiyo ni moja ya mifano jinsi imani ya mtu inavyoweza kumkwamisha au kumfanikisha.

Alikuwa omba omba kwa sababu aliamini kuwa ndivyo alivyo. Lakini alipoamini kuwa atafanikiwa, alifanikiwa.

Naamini watu wengi hawajui kuwa akili ni mtumishi wao mwaminifu. Chochote akiamonicho mtu, kiwe kizuri au kibaya, ndicho akipatacho.

Ukiiaminisha akili yako kuwa utakwama, usitegemee matokeo tofauti. Ukiamini kuwa utafanikiwa, ni suala la muda tu, hatimaye itakuwa hivyo.

Mwanasaikolojia mashuhuri kaandika, "Whatever the mind can conceive and believe, can achieve"

Na Biblia imeandika, "...aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo"

Sikumbuki kama imeandikwa kwenye kitabu cha THE MAGIC OF THINKING BIG au THE POWER OF YOUR SUBCONSCIOUS MIND, nafikiri ni mojawapo ya hivyo Vitabu. Ni habari ya mwanamke mmoja aliyepewa taarifa mbaya muda mfupi baada ya kujifungua mtoto wake wa kiume.

Mwanaye ndiyo kwanza alikuwa ametimiza miezi sita alipogundulika kuwa ana kansa. Daktari alimwambia kuwa angeweza kuishi kwa kipindi kisichozidi miezi sita. Maana yake, asingeweza kushuhudia mwanaye akitimiza umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja.

Nini jibu la mwanamke baada ya Daktari kumsomea hiyo hukumu?

"Siwezi kufa kabla sijamwona mwanangu akiwa Chuo Kikuu!"

Miezi sita baadaye, bado alikuwa hai. Hata baada ya miaka ishirini, kmwanaye akiwa ameshakuwa mtu mzima kiumri, bado kansa iliendelea kutii maamuzi yake.

Alikufa mwanaye akiwa Chuo Kikuu mwaka wa pili.

Kwa kipindi chote hicho, ilibidi kansa ipewe likizo ndefu hadi shauku ya huyo mwanamke ilipotimia.

Amini katika mambo mema. Wasaidie wengine kujiamini. Akili yako ipo makini kuchukua chochote uaminicho na kukifanyia kazi.

Ukiilisha taarifa nzuri, itakuletea matokeo chanya.

Wasaidie na wengine kwa kuwaambia mambo mema kuwahusu. Kilichotokea kwa omba omba wa Marekani kinaweza kutokea kwa "mnyonge" wa Tanzania. Ni "genius" asiyejifahamu. Anahitajika mtu anayejali kwa kiwango cha kutosha, na kumthibitishia kuwa anamwamini ili na yeye aweze kujiamini.

Kujikubali kunamfanya mtu ajiamini. Kujiamini kunauweka huru "ugenius" wa mtu.

Upo tayari kumwibua alau "genius" mmoja aliyefukiwa na unyonge?

Barikiwa!!!
Nzuri!
 
Unaweza "kutubariki" kidogo kwa ushuhuda wako?
Long story short, nina tabia ya kujinenea mambo mema kwenye kazi za mikono yangu, na hii naifanya repititively,

Na i put my heart in to it, asee mbona inakuwa kabisa yaani simple example

nikijiwekea mawazo akilini tu kuwa nataka kulala masaa 4 tu niamke muda fulani inakuwa hivyo,

Kwenye business ni hivyo hivyo, yaani kwenye ku meet na ku achieve small goals nilizojiwekea lazima nifikirie na kusema kitu 1 repipitively na naweka imani kubwa juu yake kina tokea

Very sensational and true ni power of subconscious mind hiyo

Kuna kitabu nilikuwa nasoma kinanisaidia sana nadhani ni power of the mind hivi vitu vipo kabisa mkuu
 
👏👏👏🙏🙏🙏
 
Zig Ziglar alikuwa akikatiza mitaa ya jiji la New York alipokutana na omba omba wa aina yake. Alikuwa akiomba msaada wa dola moja, na kwa kila aliyeitikia ombi lake, alimzawadia penseli.

Ziglar alimpa dola moja ila hakukukubali kupokea penseli. Hakuwa na uhitaji nayo. Na kwa nini apokee kitu cha maskini? Aliona kama hiyo ni sawa na mtu mzima kunywa uji wa mtoto.

Aliweka noti ya dola moja kwenye sahani ya omba omba na kuondoka zake. Hatua chache baadaye, alikumbuka kuna kitu alipaswa kufanya kwa huyo mtu, ambacho hakuwa amekifanya. Haraka sana, aligeuza na kumwendea yule omba omba. "Nipe penseli yangu", alimwambia, "nilikupa dola moja kwa hiyo nipatie na mimi penseli yangu"

Bila hiyana, omba omba alichukua penseli moja na kumkabidhi Zig Ziglar. Akiwa na tabasamu zito, Ziglar alimtazama usoni omba omba na kumwambia, "Wewe ni mfanyabiashara kama mimi. Mimi ninamiliki kampuni inayowafundisha watu kufanikiwa, lkini wewe unajipatia kipato chako kwa biashara ya penseli"

Baada ya kumwambia hayo, aliondoka na kumwacha omba omba akiwa ameduwaa. Hakuwahi kuambiwa maneno kama hayo.

Miaka michache baadaye, Ziglar alimpata mgeni ofisini kwake. Ni yule yule omba omba aliyemkuta mitaa ya New York miaka ya nyuma, lakini safari hii hakuwa omba omba. Alikuwa "Somebody" mwenye heshima zake. Alienda kumshukuru kwa kumbadilisha maisha yake.

Ile kauli, "Wewe ni mfanyabiashara kama mimi" ilitosha kupindua fikra zake. Alipoondoka Ziglar, aliendelea kutafakari alichokisikia kiasi cha kumfanya aanze kujiona akiwa amevaa suti kama ya Ziglar, tena akiwa anongea na watu wanaoheshimika.

Siku alipoenda kuonana na Ziglar, siyo kwamba tu alikuwa amevaa kinadhifu kama Ziglar, bali pia alikuwa mmiliki wa kampuni iliyokuwa imeajiri watu kadhaa. Alimshukuru Ziglar kwa ukarimu wake uliomfanya kuwa alivyokua, mfanyabiashara.

Alimweleza kuwa katika watu wote waliompatia msaada, ni yeye peke yake ndiye aliyejali vya kutosha kiasi cha kumtamkia maneno ambayo ndiyo aliyoyahitaji kuliko kitu kingine chochote.

Japo aliendelea na shughuli yake ya kuombaomba hata baada ya kuambiwa hivyo, ile taswira iliyotengenezwa na kauli ya Ziglar haikumwachia. Iliendelea kukua ndani mwake mpaka hatimaye akachukua hatua zilizompa mafanikio. Maneno machache yalimgeuza kutoka kuwa omba omba hadi "bosi" anayemiliki kampuni.

Hiyo ni moja ya mifano jinsi imani ya mtu inavyoweza kumkwamisha au kumfanikisha. Alikuwa omba omba kwa sababu aliamini kuwa ndivyo alivyo, lakini alipoamini kuwa atafanikiwa, alifanikiwa.

Naamini watu wengi hawajui kuwa akili ni mtumishi wao mwaminifu. Chochote akiamonicho mtu, kiwe kizuri au kibaya, ndicho akipatacho.

Ukiiaminisha akili yako kuwa utakwama, usitegemee matokeo tofauti. Ukiamini kuwa utafanikiwa, ni suala la muda tu, hatimaye itakuwa hivyo.

Mwanasaikolojia mashuhuri kaandika, "Whatever the mind can conceive and believe, can achieve" na Biblia imeandika, "...aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo"

Sikumbuki kama imeandikwa kwenye kitabu cha 'The Magic of Thinking Big' au 'The Power of Your Subconscious Mind', nafikiri ni mojawapo ya hivyo vitabu. Ni habari ya mwanamke mmoja aliyepewa taarifa mbaya muda mfupi baada ya kujifungua mtoto wake wa kiume.

Mwanaye ndiyo kwanza alikuwa ametimiza miezi sita alipogundulika kuwa ana kansa. Daktari alimwambia kuwa angeweza kuishi kwa kipindi kisichozidi miezi sita. Maana yake, asingeweza kushuhudia mwanaye akitimiza umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja.

Nini jibu la mwanamke baada ya Daktari kumsomea hiyo hukumu? "Siwezi kufa kabla sijamwona mwanangu akiwa Chuo Kikuu!"

Miezi sita baadaye, bado alikuwa hai. Hata baada ya miaka ishirini, kmwanaye akiwa ameshakuwa mtu mzima kiumri, bado Kansa iliendelea kutii maamuzi yake. Alikufa mwanaye akiwa Chuo Kikuu mwaka wa pili.

Kwa kipindi chote hicho, ilibidi kansa ipewe likizo ndefu hadi shauku ya huyo mwanamke ilipotimia. Amini katika mambo mema. Wasaidie wengine kujiamini. Akili yako ipo makini kuchukua chochote uaminicho na kukifanyia kazi. Ukiilisha taarifa nzuri, itakuletea matokeo chanya.

Wasaidie na wengine kwa kuwaambia mambo mema kuwahusu. Kilichotokea kwa omba omba wa Marekani kinaweza kutokea kwa "Mnyonge" wa Tanzania. Ni "Genius" asiyejifahamu. Anahitajika mtu anayejali kwa kiwango cha kutosha, na kumthibitishia kuwa anamwamini ili na yeye aweze kujiamini.

Kujikubali kunamfanya mtu ajiamini. Kujiamini kunauweka huru "Ugenius" wa mtu.

Upo tayari kumwibua alau "Genius" mmoja aliyefukiwa na unyonge?

Barikiwa!
Very touching
 
Uongo tu huu wa motivesheni spika
Huyo ombaomba alijuaje address ya Ziglar Hadi kufika ofisini kutoa Asante,New York ilivyo kubwa vile?😂😂😂😂😂
 
TUPE ushuhuda wako juu ya hili
Ni nyingi, lakini kwa sababu ya muda, acha niutoe mmoja.

Nilikuwa nikifanya kazi kama afisa mauzo kwenye kampuni moja ya vinywaji baridi.

Wakati naianza hiyo kazi, tayari nilikuwa nimeshajifunza kwa sehemu ndogo kuwa mtu anaweza kuwa vile aaminivyo. Hata mimi kuipata hiyo kazi, kulichangiwa na mtazamo chanya niliokuwa nao.

Baada ya kufanya kwa muda, nilipata wazo la kuijaribisha hiyo kanuni kwa dereva wangu, kwa kumbadilisha mtazamo ili apandishwe cheo kuwa afisa mauzo.

Kwa sera za kampuni, hakuwa akikidhi vigezo vya hiyo nafasi.

Kwanza, alikuwa na Elimu ya darasa la Saba, na hakuwa na taaluma yoyote ihusuyo mauzo. Kampuni ilihitaji mtu mwenye alau Elimu ya Sekondari na Mafunzo ya Mauzo.

Pili, hakuwa akijua Kingereza, jambo ambalo lilikuwa ni kikwazo kikubwa sana. Report zilikuwa zikiandikwa kwa English. Idara ya mauzo ilikuwa ikiandaa semina za mara kwa mara, na lugha iliyokuwa ikitumika ni English. Meneja Mkuu alikuwa akifanya kikao na maafisa mauzo mara kwa mara, na kwa sababu alikuwa ni Mkaburu toka Afrika Kusini, lugha pekee aliyokuwa akiitumia ni English.

Pamoja na vikwazo vyote hivyo, nilipomwaminisha vya kutosha, ndani ya miezi minne, aliweza kupandishwa cheo na kuwa afisa mauzo.

Siyo kwamba tu alifanikiwa kuwa afisa mauzo, bali pia aliweza kufanya vizuri sana kwenye nafasi yake mpya kuwazidi waliokuwa wamesomea, tena wenye uzoefu wa muda mrefu.

Alinishukuru sana kwa jinsi nilivyomsadia, na kamwe hakujua kuwa nilikuwa nikimfanyia jaribio. Sikumwambia.
 
Usemacho ni kweli,nimesoma vitabu vya kale mfano the power of subcous, hiki kinaeleza jambo kama lako,lakini pia kitabu cha the grand grimore( imperial ritual of magic) vyote vinasisitiza katika kuamini katika fikara zetu.

Kile unachokiamini ndo kinachotokea
 
Mmh.. hapa kuna madini.
Naweka kambi na tent juu
 
Uongo tu huu wa motivesheni spika
Huyo ombaomba alijuaje address ya Ziglar Hadi kufika ofisini kutoa Asante,New York ilivyo kubwa vile?😂😂😂😂😂
Story siijui lakini it is quietly very simple kwa logic ya kawaida.

Ni mfanyabiashara anayefundisha watu biashara. Maana yake ni mtu anayejulikana. Address za ofisi ni kitu public. Anybody can access at any time.

Mantiki ingekuwa ni je, alijuaje kuwa Ziglar ndiye aliyemuambia hayo maneno? Je, walipata nafasi ya kufahamiana kwa majina? Kama ndiyo, sawa.
 
Karibia kila nilichotamani kukipata hua nakipata. Japo kitachelewa.
Ndio maana mada zangu hua zimeegemea kwenye Masuala ya Nature na Subconscious mind
 
Uongo tu huu wa motivesheni spika
Huyo ombaomba alijuaje address ya Ziglar Hadi kufika ofisini kutoa Asante,New York ilivyo kubwa vile?😂😂😂😂😂
Kwa watu mashuhuri, hata mtoto anaweza akamfahamu, sembuse mtu mzima.

Mtoto wa miaka mitano, anaweza akawa hajawahi kukutana na mama Samia, lakini ikitokea amekutana naye sehemu, atatambua huyo ndiye Mama Samia ambaye amekuwa akimwona kwenye TV.

Si shida kufahamu ilipo ofisi ya mtu mashuhuri. Hata kwa kuulizia tu, unaweza kuifahamu.
 
Back
Top Bottom