Pole sana Mkuu, sasa nisikilize kwa makini.
Kwanza, tambua UCHAWI ni mpango wa shetani wala sio wa Mungu na maandiko yanasema wachawi sehemu yao ni ktk ziwa na moto.
Pili, Kuhusiana na mambo ya ndoto hususani za kichawi. Mchawi anapokuja kwako kukuroga huwa haji na sura yake yeye, ni mara chache saaaaana kuja na sura yake. Sifa kuu ya UCHAWI ni SIRI, mchawi ukishamjua ile nguvu yake inapungua kwako. Kama ww upo karibu sana na Mungu basi Mungu angekufunilia dhahiri huyo anayekuroga. Kwahiyo Mkuu mtu akitaka kuharibu mahusiano kati yako na dada yako sio lazima akufate kwa njia ya kimwili, anaweza akakufata kwa njia zisizoonekana kwa macho ya kawaida, moja ya njia hizo ni mchawi kukufata kwa sura ya huyo mtu anayetaka ufarakane nae. Na wachawi wakikutana huwa wanajuana hata kama wasipokuwa ktk mishe zao za uchawi. Sasa apo tunaona kuwa mchawi anaweza akakufata hata kwa njia ya ndoto ili tu ukosane na mtu wako wa karibu na mafarako ni mpango wa shetani.
Tatu, Hao unaowaita wataalamu au waganga ndio wachawi waliokubuhu. MGANGA NDIE MCHAWI, ILA SIO KILA MCHAWI NI MGANGA. Ili kujificha ktk jamii Wachawi wengi ambao ni nguli huwa wanajivika vifuniko vya vyeo au taaluma ndani ya jamii, kama wasomaji nyota, shekh, ostadh, mnajimu n.k wanafanya hivi ili kujijengea picha nzuri ndani ya jamii ili msifikirie kabisa kwamba anaweza akawa mtu mbaya. Hao wataalamu wako kwa Mungu ni JEHANUM, Waganga mungu wao ni SHETANI/IBILISI na sehemu yao ni ktk Ziwa la Moto. Mungu aliyeumba Mbingu na Nchi SIO MSHIRIKINA.
Unapoenda kwa Mganga moja kwa moja anatambua ni kitu ulichopandikiziwa na huyo mchawi anyekuroga na anaweza akawasiliana nacho bila wewe kujua. Kazi za hilo jini, aliyemtuma n.k vyote hivyo mganga anaweza akavijua maana na yeye ni mchawi, kama mission ni kukugombanisha basi hiyo mission ni lazima iendelee maana na yeye ni mshirika wa shetani.
Njia ya ww kuwa salama ni YESU tuu, Kwa Yesu hakuna hawa wajinga kukusumbua. Nimepambana sana na hawa wachawi na hawajawahi kumshinda Yesu hata siku moja. Nna uzoefu mkubwa juu ya hawa wapumbavu, kama una swali uliza.