happy amos
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 251
- 434
Leo nimekaa nimefikiria sana kuhusu ndoa
sikupata majibu. Yaani ukifikiria sana unaweza usione maana sana ya kuolewa.
Nakumbuka kuna kipindi dada angu mkubwa aliniambia mdogo wangu ndoa ni utumwa tu kwetu wanawake sasa namuelewa. Mfano mimi kabla sijaolewa nilikuwa na maisha yangu na ndoto zangu nyingi tu. Nilipanga mwaka huu usiishe sijajenga walau nyumba ya vyumba 3 na nikawa na juhudi za kufanikisha hilo.
Lakini tangu nimeolewa naona nakamilisha ndoto za mume wangu tu yaani malengo yake yeye aliyoyapanga kabla hatujawa pamoja naona ndio ninayo au tunayotimiza leo.
Mwenzangu nilimkuta kajipangia kutofanya chochote mpaka amalize kujenga kwao na kusomesha wadogo zake, tulivyoanza kuishi pamoja ndoto zangu za kutafuta kiwanja zikazimwa naambiwa subiri kwanza tumalize majukumu ya nyumbani.
Nikiwaza saaaaaana naona natimiza ndoto zake tu au za nyumbani kwao.
MTU unakosa jinsi sababu tuliumbwa tuwe chini yao na wao wawe juu yetu inabidi kuwa mdogo tu.