Ukienda sheli usiseme weka full tank unaitwa mwambie hivi

Jul 23, 2023
38
136
Habar wadau wa Jamiforums leo nimeona niwaletee hii.

Tanzania wauza Mafuta asilimia 90 wote ni wezi na gari ya mafuta wanaiuza mara mbili kwa wateja je wanafanyaje

Watu wa Petrol station wengi ni Matapeli hasa kwa wale watu wanao enda kujaza mafuta full tank kwenye gari hasa wale ambao walikuwa na mafuta kiasi tayari ndani ya gari sababu mara nyingi huwa wanaiba hapo ukitaka kuamin ilo kama full tank yako huwa unajaza kwa shilingi laki 2 siku weka mafuta ya elfu hamsini halafu nenda sheli yoyote waambie wakuwekee full tank machine itasoma laki2 ile ile

Kwa wenye magari mnaweza mkajaribu hili pia na mamlaka mfatilie.
 
Hueleweki unataka kusema nini, full tank maana yake ajazie mafuta mpaka juu na fuel attendant anakuwa anabonyeza mafuta kwa kushika trigger ile yawe yanasoma mpaka yakifika juu kabisa ya tank ndio anaacha kisha wewe mwenyewe unaona kiasi alichoweka then unamlipa hela yake sasa kuibiwa hapo kuko wapo.
 
hata hua sielewi hawa jamaa wanaibaje mafuta, hadi nimtafute mfanyakazi mmoja wa petrol station aniambie siku moja. mimi hua nashuka, namwambia weka full, nakaa pale nakuwa naye, naangalia awe ameweka number ya pesa inasoma, na aondoe mkono kwenye handle, aweke kwenye gari aiache iwe automatic yenyewe, hadi amalize ndio asogeze mkono pale. hata hapo wananiibia?
 
Habar wadau wa Jamiforums leo nimeona niwaletee hii.

Tanzania wauza Mafuta asilimia 90 wote ni wezi na gari ya mafuta wanaiuza mara mbili kwa wateja je wanafanyaje

Watu wa Petrol station wengi ni Matapeli hasa kwa wale watu wanao enda kujaza mafuta full tank kwenye gari hasa wale ambao walikua na mafuta kiasi tayari ndani ya gari sababu mara nyingi hua wanaiba apo ukitaka kuamin ilo kama full tank yako hua unajaza kwa shilingi laki 2 siku weka mafuta ya elfu hamsini halafu nenda sheli yoyote waambie wakuwekee full tank machine itasoma laki2 ile ile

Kwa wenye magari mnaweza mkajaribu hili pia na mamlaka mfatilie.

Hii ni kweli kabisa….iliwahi nitokea nikamuacha aendelee kuweka mpaka ikafika laki tatu ndio ikajaa….nikamwmbia hii gari ina tank ya lita 85 hizo lita zingine zimeenda wapi!?nilikomaa mpk meneja akaitwaa…nikalipa 85 x2317 by that time nikasepa.
 
Hueleweki unataka kusema nini, full tank maana yake ajazie mafuta mpaka juu na fuel attendant anakuwa anabonyeza mafuta kwa kushika trigger ile yawe yanasoma mpaka yakifika juu kabisa ya tank ndio anaacha kisha wewe mwenyewe unaona kiasi alichoweka then unamlipa hela yake sasa kuibiwa hapo kuko wapo.
Full tank namaanisha ajaze mafuta full sio aweke ya kias kazaa
 
Hueleweki unataka kusema nini, full tank maana yake ajazie mafuta mpaka juu na fuel attendant anakuwa anabonyeza mafuta kwa kushika trigger ile yawe yanasoma mpaka yakifika juu kabisa ya tank ndio anaacha kisha wewe mwenyewe unaona kiasi alichoweka then unamlipa hela yake sasa kuibiwa hapo kuko wapo.
Ile nozzle huwa ina tundu la return ambalo ili kuzuia mafuta yasimwagike, tank la gari yako likijaa mafuta yanarudi kwenye pump(tank la petrol station).

Sasa pump attendant asipoiweka ile nozzle kwenye auto mode, akawa anajaza kwa mkono moja kwa moja itafikia hatua mafuta yatajaa kwenye tank la gari yataanza kurudi kwao huku pump machine inaendelea kusoma tu.

Ili kuepuka hilo, hakikisha akiwa anakujazia full tank nozzle ipo kwenye auto mode, ile trigger ya nozzle iwe imenasia kwa juu (hapo hata pump attendant anaweza kuhudumia gari nyingine huku kwako mafuta yanaingia), kwa mfumo huo mafuta yakianza tu kurudi kwenye pump machine, machine inakata kuingiza mafuta hivyo inaacha kuendelea kuhesabu maokoto.
 
Ahsante Kwa elimu japo Sina gari
 
hata hua sielewi hawa jamaa wanaibaje mafuta, hadi nimtafute mfanyakazi mmoja wa petrol station aniambie siku moja. mimi hua nashuka, namwambia weka full, nakaa pale nakuwa naye, naangalia awe ameweka number ya pesa inasoma, na aondoe mkono kwenye handle, aweke kwenye gari aiache iwe automatic yenyewe, hadi amalize ndio asogeze mkono pale. hata hapo wananiibia?

Wanaset kwenye mashine kupunja ndio maana ewura wakienda kuangalia zile mashine za pump wakikuta zipo chin wanapigwa fine
 
Ile nozzle huwa ina tundu la return ambalo ili kuzuia mafuta yasimwagike, tank la gari yako likijaa mafuta yanarudi kwenye pump(tank la petrol station).

Sasa pump attendant asipoiweka ile nozzle kwenye auto mode, akawa anajaza kwa mkono moja kwa moja itafikia hatua mafuta yatajaa kwenye tank la gari yataanza kurudi kwao huku pump machine inaendelea kusoma tu.

Ili kuepuka hilo, hakikisha akiwa anakujazia full tank nozzle ipo kwenye auto mode, ile trigger ya nozzle iwe imenasia kwa juu (hapo hata pump attendant anaweza kuhudumia gari nyingine huku kwako mafuta yanaingia), kwa mfumo huo mafuta yakianza tu kurudi kwenye pump machine, machine inakata kuingiza mafuta hivyo inaacha kuendelea kuhesabu maokoto.
Hapo sasa nimekuelewa concept yako mkuu, maelezo yamenyooka.
 
Back
Top Bottom