Ukichukua fedha benki sasa ni roho mkononi

Ukichukua fedha benki sasa ni roho mkononi

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956
uporaji.jpg

Katuni inayoonyesha ujambazi wa kutumia pikipiki na bastola unavyoshika kasi jijini Dar es Salaam.

KWA UFUPI
Matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha yamekuwa sugu na kusababisha wananchi wanaopeleka au kutoa fedha benki kuvamiwa, kujeruhiwa au kuuawa mchana kweupe na majambazi wanaotumia pikipiki.

Dar es Salaam. Ni roho mkononi. Hayo ndiyo maneno matatu yanayofaa kuelezea hali ilivyo jijini Dar es Salaam na maeneo kadhaa nchini kwa sasa, hasa pale mtu anapobeba fedha nyingi.

Matukio ya ujambazi kwa kutumia silaha yamekuwa sugu na kusababisha wananchi wanaopeleka au kutoa fedha benki kuvamiwa, kujeruhiwa au kuuawa mchana kweupe na majambazi wanaotumia pikipiki.

Wananchi wamekuwa wakihoji ni kwa jinsi gani majambazi hao hupata taarifa za mtu aliyekwenda benki ama kuweka au kuchukua fedha.

Mkazi wa Tabata Kimanga, Dar es Salaam, Salum Mashati alisema: “Haiingii akilini, utasikia mtu kaporwa fedha akitoka benki. Eti majambazi wanasema kabisa toa hizo milioni 20, wanajuaje kuwa una kiwango hicho? Huenda watu wa benki wanashiriki uhalifu huu.”

Hata hivyo, meneja wa tawi moja la benki lililopo Mlimani City, ambaye hakupenda jina lake litajwe alikanusha madai hayo... “Si kweli kwamba benki zinashirikiana na majambazi kufanya uhalifu huu. Kwanza wahudumu (bank tellers) hawaruhusiwi kuingia na simu wanapohudumia wateja.

“Hata mteja anapoingia benki hukatazwa kuongea na simu au kuandika ujumbe. Mazingira tuliyojiwekea hayaruhusu kabisa mawasiliano kati ya benki yetu na watu wa nje wakati wa kazi. Nadhani vitendo hivi vya ujambazi vinaanzia kwa wateja wenyewe kutoa taarifa juu ya mipango yao kwa watu ambao si waaminifu,” alisema.

Kauli ya Polisi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alitupa lawama kwa wananchi akisema wamekuwa hawaombi ulinzi wa polisi wakati wa kupeleka au kuchukua fedha benki.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwahi kutoa wito pia kwa taasisi za fedha kulindwa na polisi badala ya walinzi binafsi.

“Wakuu wa benki wanaogopa gharama za ulinzi kwa jeshi la polisi ili kuhakikishiwa usalama lakini mwishowe wanaibiwa kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya kile ambacho wangelipa kwa polisi,” alisema.

Baadhi ya matukio

Juni 23, mwaka huu, Sista wa Shirika la Mtakatifu Maria, Parokia ya Mwenyeheri Anwarite, Makoka, Dar es Salaam, Clecensia Kapuli aliuawa kwa kupigwa risasi na majambazi wakati akitoka Benki ya CRDB, Tawi la Mlimani City na kuporwa fedha. Agosti 8, mwaka huu, Meneja wa Kampuni ya ununuzi wa korosho na ufuta ya Olam, Jaffari Mgumba aliporwa Sh47 milioni baada ya kuchukua fedha za ushirika katika Benki ya DTB Tawi la Quality Plaza.
Mtu mwingine ambaye jina lake halikufahamika alichukua mkopo wa Sh10 milioni, lakini kwa bahati nzuri, kiasi fulani cha fedha kilibaki benki na kingine akafanya malipo palepale na wakati anaondoa akiwa amebaki na Sh2 milioni alivamiwa na majambazi waliomtaka awapatie Sh10 milioni alizochukua.

Tukio jingine la hivi karibuni ni kuuawa kwa mmiliki wa Kampuni ya Sowers African iliyopo mkabala na Mlimani City, Adson Cheyo Agosti 22, mwaka huu alipokuwa akitoka Benki ya KCB kuchukua na kuporwa fedha hizo.

Kabla ya tukio hilo, kulikuwa na ujumbe uliokuwa ukisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ukionya watu kutembea na fedha nyingi katika maeneo ya Mlimani City, Millennium Tower na Kibo Complex kwa madai si salama. chanzo.Ukichukua fedha benki sasa ni roho mkononi - Kitaifa - mwananchi.co.tz

huyo meneja anasema benki teller hawaruhusiwi kuingia na simu?! juzi nimeshuhudia bank teller wa DTB anahudumia huku simu iko sikioni[kaibana katikati ya kichwa na bega wala hajali watu,mwisho akaiweka chini akawa anaendelea kuchat mara anashika simu mara anahudumia.....ilikuwa asubuhi nilimwangalia tu nikamwacha wala sikutaka kuharibu siku yangu maanake wana maneno machafu sana wahudumu wakibongo!
 
lazima tukubali kuwa majambazi wanapofanya uhalifu wao wanapewa mchongo na mtu wa ndani...kuna kuwa na( inside job)
lazima mtu anauza habari kwa majambazi..mfano kuna mama mmoja alikuwa anaishi kunduchi alikuwa na nyumba drive in nyumba hiyo aliwapangisha wachina kila ikifika wakati wa kodi anakuja chukua kwa wachina, sasa kuna wakati ulifika akaja chukua kodi ya nyumba yake karibu na drive in hapa wachina wakampa hela yule alipewa hela saa 12 jioni yule mama akarudi kunduchi usiku majambazi wakamvamia wakampiga sana wakachukua hela, uchunguzi ulipokuja fanywa na polisi kumbe mfanyakazi wake wa ndani aliuza issue kwa majambazi baada ya kumsoma mama huyo kwa muda mwingi.....
 
kweli kabisa tabia hiyo wanazo sana bank tellers na baadhi ya wateja wakingia bank wanakuwa na simu...
 
huyo meneja anasema benki teller hawaruhusiwi kuingia na simu?! juzi nimeshuhudia bank teller wa DTB anahudumia huku simu iko sikioni[kaibana katikati ya kichwa na bega wala hajali watu,mwisho akaiweka chini akawa anaendelea kuchat mara anashika simu mara anahudumia.....ilikuwa asubuhi nilimwangalia tu nikamwacha wala sikutaka kuharibu siku yangu maanake wana maneno machafu sana wahudumu wakibongo!

Mkuu hukupaswa kunyamazia hicho kitendo cha huyo mhudumu... hata kama hukutaka kurushiana nae maneno ungetoa taarifa kwa meneja, hapo ungekua umetoa msaada mkubwa
 
mkuu hukupaswa kunyamazia hicho kitendo cha huyo mhudumu... Hata kama hukutaka kurushiana nae maneno ungetoa taarifa kwa meneja, hapo ungekua umetoa msaada mkubwa

mameneja wao wengi wana akili kama za hao wafanyakazi....nishawahi kuwashitakia sana na hakuna meneja anachoweza kufanya,hawana professionalism....huwa nawablast mimi mwenyewe mpaka meneja anakuja na na yeye nampa maneno yake,ila siku hio sikutaka kuanza siku vibaya nilimwangalia tu na kumsikitikia.
 
lazima tukubali kuwa majambazi wanapofanya uhalifu wao wanapewa mchongo na mtu wa ndani...kuna kuwa na( inside job)
lazima mtu anauza habari kwa majambazi..mfano kuna mama mmoja alikuwa anaishi kunduchi alikuwa na nyumba drive in nyumba hiyo aliwapangisha wachina kila ikifika wakati wa kodi anakuja chukua kwa wachina, sasa kuna wakati ulifika akaja chukua kodi ya nyumba yake karibu na drive in hapa wachina wakampa hela yule alipewa hela saa 12 jioni yule mama akarudi kunduchi usiku majambazi wakamvamia wakampiga sana wakachukua hela, uchunguzi ulipokuja fanywa na polisi kumbe mfanyakazi wake wa ndani aliuza issue kwa majambazi baada ya kumsoma mama huyo kwa muda mwingi.....

uporaji mwingine tunajitakia sometimes!!! Mbona mimi kodi ya nyumba naenda kulipia benki??!! Mwenye nyumba hataki nimpe cash namuwekea benki nampigia simu anacheki salio lake,simple!
 
Kuna watu wakichukua pesa bank wana mbwembwe mpaka kero....sasa wajifunze
 
uporaji mwingine tunajitakia sometimes!!! Mbona mimi kodi ya nyumba naenda kulipia benki??!! Mwenye nyumba hataki nimpe cash namuwekea benki nampigia simu anacheki salio lake,simple!
wewe unafanya safi hapo mkuu ila kuna ile kusahau kama huyo mama naona alikuwa na moto na hela siku ile, kingine timing unafanyiwa unategewa mtego ili siku moja unase bahati mbaya yule mama akanasa...alichezea kipigo sana na kama unavyojua kunduchi hakuna msaada
 
wabongo wengi siku hizi hatuna long term planning za maisha utakayoishi. ndio maana vijana wakiajiriwa tuu wanaanza kutafuta namna ya kuiba. watu wa benki ndio hao, wakiona mkinga kaingia benki na kubeba m200 akafunge mzigo wanaita watu wao wampore. ukikutana na trafic kijana utatamani umtemee mate usoni. analazimisha umpe rushwa ni balaa. ndivyo hivyo na office zingine. Mafanikio ya kuwa na nyumba za kifahari, magari nk ya haraka haraka ndio yanafanya watu tuwe wauwaji, wezi nk.
Aaafu baada ya hapo unaenda kutoa ushuhuda kanisani ‘Mungu kanipatia gari.'

kuna dhambi tunazozifanya hata shetani anazikataa.
 
Watu wengine wanapopata hela wanakuwa na mbwembwe zisizo na maana,wengine hata wakiwa bar wanasambaza upendo mpaka kero.
 
wabongo wengi siku hizi hatuna long term planning za maisha utakayoishi. ndio maana vijana wakiajiriwa tuu wanaanza kutafuta namna ya kuiba. watu wa benki ndio hao, wakiona mkinga kaingia benki na kubeba m200 akafunge mzigo wanaita watu wao wampore. ukikutana na trafic kijana utatamani umtemee mate usoni. analazimisha umpe rushwa ni balaa. ndivyo hivyo na office zingine. Mafanikio ya kuwa na nyumba za kifahari, magari nk ya haraka haraka ndio yanafanya watu tuwe wauwaji, wezi nk.
Aaafu baada ya hapo unaenda kutoa ushuhuda kanisani ‘Mungu kanipatia gari.'

kuna dhambi tunazozifanya hata shetani anazikataa.
hahahaha aise kweli kila mtu ana haraka na maisha ya utajiri kila mtu hataki kuchelewa....mfano kuna mmiliki wa sheli moja ya mafuta hapa dar alifanya sana umafia ashamporaga hadi jamaa yangu wa karibu mtandao wake ulikuwa tz na kenya ila sahvi ukienda kwake ni mungu anaabudiwa kashatubu.....naona kashasamehewa makosa yake
 
Lazima watu wa benki wanahusika wezi hawawezi ota kuwa kila atokae benki amechukua pesa

sehemu yoyote ikitokea uhalifu lazima kuna mtu anatoa information anawapa wahalifu, na wahalifu wanakula sahani moja na baadhi ya maskari wakipiga hela wanawapoza na wao huo ndy ukweli
 
hahahaha aise kweli kila mtu ana haraka na maisha ya utajiri kila mtu hataki kuchelewa....mfano kuna mmiliki wa sheli moja ya mafuta hapa dar alifanya sana umafia ashamporaga hadi jamaa yangu wa karibu mtandao wake ulikuwa tz na kenya ila sahvi ukienda kwake ni mungu anaabudiwa kashatubu.....naona kashasamehewa makosa yake

Akauze vyooote alivyonavyo na kuwagawia masikini fedha alizonazo ndipo ataeleweka
 
Bank ndo zao, ukienda bank kuchukua mshiko mrefu ukaona teller anachelewesha huduma inabidi ushtuke mapema!
 
Angalia Tofaui yetu sie na Kenya.
Madawa ya Kulevya:
Uthubutu wa Raisi Kenyata
Kenya wamejitahidi sana kudhibiti hili na juzi tu Mfano wa Kuiripua meli iliyohusika.Hii inaitwa ni kuthubutu.
Hapa kwetu Tungeunda tume,watu wakisahau tume inapotea.Mchezo wa kusema Dawa zimeoneakana sehem bila wahusika kuwepo ni mpango wa ku boost jina kwa kutoa Dawa zilizokamatwa na kutuchezea akili ili tuone kweli.Hapa kila kitu tunaogopa kushtakiwa,wakati Kenyatta amesema hataki hata kumjua mwenye meli,ameiripua na wao watajipanga.Hapa kwetu Meli ingekaa kama ya Magufuli mwisho wa siku ingepotezwa kinyemela.

Ulinzi na Usalama wa Majiji vs Ujambazi:
Kenyatta ameziba masikio ya Wabunge waliolalamika Fedha za wananchi kutumika nyingi.Anatumia Billions of Money kuweka Camera za kisasa Jiji zima.Yaani hata ukitema mate unaonekana.Hii ni hatua kubwa sana na ni mfumo wanaotumia nchi zilizoendelea,na ndio maana hata matukio ya wenzetu inakuwa rahisi kupata ushahidi na kumfuatilia mtu baada ya tukio.
Yaani wewe ukifanya tukio basi jua muda mfupi tu unakamatwa kwa kutumiwa kwa signal za Camera,ni mfumo unapa Kenya Credit kubwa sana na inaitumia nafasi hiyo kuvutia zaidi wawekezaji.Maana Jiji la Nairobi walilibatiza jina la NAIROBBERY,la kini Muda mfupi litakuwa Jiji lenye kuvutia wawekezaji wengi kwa kuwa litakuwa ni miongoni mwa majiji Salama.
Majambazi na uhalifu mwingine wowote wanatumia udhaifu wa usalama wa nchi husika,maana ujambazi mwingine eti mtu anaiba halafu anatembea hata kwa miguu anasepa zake.Maana anajua kabisa kwamba hakuna jipya,lakini kama jiji ni salama basi hatua kumi hafiki watu wanae,maana Camera zita detect.
Tanzania:Sei tunajenga Daraja la Kigamboni ili iwe kama la Manzese watu wapigae kabali napesa iwe haina maana kutumika pale.

Tujifunze,Jiji la Dar linakuwa ni miongoni mwa majiji hatari.Yaani hata watalii wanapewa warning ya jiji hilo.
Kuzuia bodaboda sio dawa.Kwani kabla ya bodaboda watu walikuwa wanatumia magari na wanaiba vilevile.
Kama jiji halitawekwa mfumo kama Kenya licha ya kwamba ni Billions of money basi uwekezaji nao unapotea bila sie kujijua,hakuna muwekezaji anaewekeza sehem ambayo sio Salama.
Tutakaa na mikakati ya kula posho kwa kuvutia wawekezaji wakati ugonjwa wetu tunaujua.
Hata kama una huduma zote muhim,kama usalama sio mzuri hunalako.
Inakera sana huu ujambazo wa kitoto unaofanyika Dar
 
Back
Top Bottom