Hili nyambizi la Urusi lililopata hitilafu na kuibuka ili lisizame .. Nalilinganisha na ccm! Kwa kawaida nyambizi linatembea chini ya maji na huwezi kuliona bali kwa mitambo maalum
Likiwa juu ya uso wa bahari hivi tambua limepata shida kubwa.. Lione lilivyojaa haya ....NA HII NDIO CCM
Na hapo haliwezi tena kusonga mbele mpaka livutwe na manowari...!View attachment 1882125
Vina na mistari kwenye ngeli za kiarifa[emoji1533][emoji1752][emoji1545]Nyambizi isipopiga mbizi,
Nyang'au atalia ka nyau,
Nyahela naye agawe hela.
Nyakati zakuja kwa wakati,
Nyebunduki watupa bunduki,
Nyerere alisema kwa shere,
Nyaisanga pamoja kiranga,
Nyamageso pamoja nyangweso,
Nyote yowe pigeni kwa wote,
Nyamagana hakuna pigana,
Nyegezi nako acha mapenzi,
Nyambizi ashindwe piga mbizi,
Nyamafu alo nyambizi mfu,
Nyambizi kwa kupora vya wizi,
Nyarugusu si nyambizi busu.
"The time for liberation is dawning"
Thus tunasema raisi akifa turudi kwenye uchaguzi tumpate mtu qualified chaguo la wananchi na sio hii ya kupeana.Siku zote Makamu wa raisi hawezi kuwa Smart maana rais hawezi chagua Makamu Smart kumzidi Yeye Ili kuibalance ndoa.Wachaguliwa wote hawako qualified kwa kazi kwani hawakupita kihalali na hiyo inareflect moja kwamoja kwenye utendaji wao.
Hivyo na hao wanao wateua hawako qualified,, kwani unqualified persons ndio wanofanya hizo teuzi.
Tungeachwa tuchague tungechagua watu waliofit kwa hizi kazi, nao wangeteua watu waliofit kufanya kazi.
Kwasasa mwendo wetu ni MZOBEMZOBE.
Jiandae kuzama na jahazi au uruke uliache jahazi lizame na wengine.
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Tumeruhusu washenzi watutawale.Nimefuatilia yanayoendelea katika taifa letu kwa sasa naona kila siku zanavyosonga mbele matumaini yanazidi kupotea. Kimsingi kuna ombwe la uongozi katika taifa letu kwa sasa linaloonyesha kuwa viongozi wetu hawa wameshindwa ku-perfom na sasa wamebaki kuhangaika na Chadema.
Ukiona kiongozi anashindwa kujua agenda ya watanzania ni nini kwa sasa basi ujue huyo ni kiongozi wa genge la watu tu ndani ya serikali kwa maslahi ya hilo genge.
Na kwa hakika yanayo tokea sasa hivi ni matokeo ya ubakaji wa Uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana ambapo kimsingi wanalazimisha kutawala watu ambao hawakuwachagua na katika hili kila mtanzania anajua.
Inavyoonyesha sasa hivi watanzania wanaishi kama mateka wa kundi hili dogo kwa kutumia nguvu na propaganda nyepesi dhidi ya wananchi bila kujua kuwa Tanzania ya kizazi hiki siyo ile ya miaka wa sitini na sabini.