Ukibanana na Mchafu, Hakika Utachafuka

Ukibanana na Mchafu, Hakika Utachafuka

Wewe hunaga akili na hujawahi kuwa na akili hata siku moja.wewe ni kama tu mleta mada.
Mleta mada ni wewe Lucas mwashambwa,nitakunywa sumu mtu akinilinganisha na wewe,tena koma kabisa. Mimi sifanani na kilaza na shoga kama wewe,kafie mbele huko.
 
Hakuna democracy. Period! Jambo la makonda ni kielelezo tosha
 
Rais ana machaguo mawili tu mbele yake. Aruke pamoja na watanzania wema au aruke na mtu mwovu, naye awe sehemu ya uovu wake.
Mama anatakiwa kufahamu kuwa kuna mtu ambae mikono yake imechafuka damu na anayoongea na kutenda ni damu zinamlilia!
 
Mara nyingi hata watu wazuri walichafuka kwaajili ya kujishikamana na watu wenye matendo machafu. Kuna misemo na mausia mengi kuanzia kwenye vitabu vya dini mpaka kwenye jamii juu ya wale tunaoshikamana na waovu:

Biblia inasema, jicho lako likikukosesha ling'oe maana ni aheri kuingia mbinguni na jicho moja kuliko kubakia nayo yote halafu ukaukosa ufalme wa mbinguni. Jicho hili la kukukosesha ndio hawa watu wanaotuzunguka na kukaribiana nao.

Kuna ule msemo kuwa ndege wafananao huruka pamoja. Nayo ni tahadhari, juu ya wale wanaoambatana au kushikamana na waovu. Ukiwa karibu na jambazi, jamii itakuchukulia nawe ni jambazi. Ukiwa umejishikamana na jambazi linaloua watu, linalopora mali za watu, na linalowapoteza watu, tambua nawe utachukuliwa kuwa ama unafurahia huo uchafu au nawe unashiriki kwenye huo uchafu.

Naambiwa kule Vatican wakiwa wanafanya uchaguzi wa kumpata Papa, mara akichaguliwa, ili kujua Papa huyu atakuwa ni mtu wa namna gani, wanangojea wasikie jina atakalolichagua. Ndiyo maana hata Papa wa sasa alipochaguliwa tu, na kisha kuchagua jina la Francis, ilimaanisha Papa huyu atafuata fadhila ya umaskini kama alivyokuwa Mt. Francis, atakuwa mtu wa msamaha na asiyependa kabisa kumhukumu yeyote. Na ndicho kilichotokea. Kwanza aligomea kuhamia nyumba iliyokuwa maalum kwaajili Papa kwa sababu aliiona ni ya kifahari. Akamsimamisha Askofu wa Ujerumani aliyekuwa ametengeneza kitanda chenye thamani zaidi ya dola 10,000. Alipoulizwa kuhusu mashoga, akajibu tu kuwa kanisa kazi yake ni kumfundisha mwanadamu nini kilicho sahihi kwa kadiri ya mpango wa Mungu, lakini ni nani yeye hata amhukumu mwanadamu mwingine? Kazi yake ni kufundisha, siyo kuhukumu.

Mambo mengi mabaya na ya kutisha wakati wa utawala wa Hayati Magufuli, ni Bashite aliyekuwa akiyasimamia. Akapewa uhuru mkubwa wa kutenda aliyoyataka bila kukemewa wala kuadhibiwa. Na aliweza kufikia hapo baada ya kufanikiwa kumtisha Hayati Magufuli, na kumwaminisha kuwa yeye ndiye pekee aliyempenda na kujitoa maisha yake yote kwaajili yake Rais. Matendo maovu yote aliyoyafanya Bashite kwa jina la wasiojulikana, kuwatisha wafanyabishara wakubwa na kuwabambikia kesi za biashara za madawa ya kulevya, mwishowe lawama zilimwangukia Magufuli. Bwana huyu alifanikiwa kupokonya sehemu ya madaraka ya Rais na kuyatumia katika uovu, kiasi cha kumkaripia hata waziri mkuu na IGP. Marehemu Maguguli alikuja kugundua wakati muda umepita.

Rais Samia, yupo kwenye njia ile ile aliyoipita Rais Magufuli, na kwa vile ndiyo aliyoichagua, pia naye atayavuna matunda yale yale. Ajue kuwa maovu yote atakayoyatenda Bashite, yeye ndiye atabeba gharama yake. Watakaouchukia uovu wa Bashite, watamchukia na yeye pia. Ni suala la muda tu, tutashuhudia mengi.

Rais ana machaguo mawili tu mbele yake. Aruke pamoja na watanzania wema au aruke na mtu mwovu, naye awe sehemu ya uovu wake.
Upo sahihi Binafsi sioni tifauti ya Utawala wa Magufuli na huu kwani Watu ni Wale wale na Ubadhilifu ni Ule ule
Makonda ni yule yule
 
Huna haja ya kuangaika na huyu kiumbe, hajawai kumiliki akili hata siku moja. Amekuwa akitumika kueneza propaganda nyepesi za kukaririshwa bila kujiongoza. Ushoga anaoupigia upatu ni jambo la kukaririshwa kwasababu umekuwepo muda mrefu, ni janga bila kujali itikadi yoyote. Kutokana na propaganda mfilisi za baadhi ya wanakisiasa walitaka ionekane mbele ya jamii kwamba ni agenda ya baadhi ya vyama vya upinzani, upande mwingine dini fulanifulani walijitahidi kukaa pembeni na kurusha mpira Vatican. Wasiokuwa na akili wameingia kwenye hiyo mtego.

Kwa kweli Mwashambwa ni mgonjwa. Ni mental medical case. Ni wa kumsamehe, hajitambui.
 
Back
Top Bottom