Ukiamua kujidanganya jipange kikamilifu

Ukiamua kujidanganya jipange kikamilifu

Mejasoko

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
318
Reaction score
646
Kwanini ni muhimu kuweka plan nzuri? Siku moja wanafunzi wanne wa chuo wanaosoma programme moja walicheza hadi usiku sana hawakusoma na kesho yake kulikua na Test imepangwa.

Kulivyokucha wakawaza plan moja, wakajichafua sana na grease/grisi na oil alafu wakaenda kwa Dean(mkuu wa programme wanayosomea) na wakamdanganya kuwa usiku walienda kwenye harusi na wakati wanarudi gari iliharibika ikabidi wasukume njia nzima usiku kucha na muda huo ndo wamefika chuo kwahiyo hawapo kwenye hali nzuri kufanya Test.

Dean wala hakuwabishia sana akawaambia kwa kuwasaidia wajiandae na Re-test siku 3 zijazo, wakashukuru na wakasema watakua tayari kwa muda huo uliopangwa, kweli walisoma sana hakuna kitu waliacha kusoma.

Siku 3 zilipita muda wa Test ukafika, wao walifika mapema kabla ya Dean, Dean alipofika akawaambia "Test yenu ina masharti ya kipekee sana, wote wanne mtatakiwa mkae kwenye vyumba tofauti kwaajili ya kufanya hiyo test" wote walikubali maana walijiandaa vizuri sana hizo siku 3, hivyo kila mtu hakujali na wakakaa chumba tofauti.

Test ikaja kila mtu akafungua akakutana na maswali mawili tu yenye Marks 100.

Qn 1. Jina lako nani ........ (2 marks)
Qn 2. Tairi ipi ilipasuka?
(a) la mbele kulia
(b) la mbele kushoto
(c) la nyuma kulia
(d) la nyuma kushoto ( 98 marks).

Wanafunzi hawa wote walifeli maana hawakua na plan nzuri ya uongo wao.
Hii ni stori ya kweli iliyotokea Indian Institute of Technology (IIT) Batch ya 1992
 

Attachments

  • IMG-20250103-WA0001.jpg
    IMG-20250103-WA0001.jpg
    57.9 KB · Views: 22
Hii kali ila ina funzo, ukiwa muongo jipange na usiwe mwepesi kusahau.

Nikiwa chuo 2nd year nilisign special baadhi ya masomo, nikiwa nafuatilia ujazaji wa fomu nikaingia kwa Head of department, yule Prof aliniuliza maswali nikiri tu nilimuongopea kwa 99%. Nilipotoka ofisini kwake nikajiuliza mbona kanihoji sana? Kuna kitu kikaniambia tunza kumbukumbu ya uliyoulizwa na uliyoyajibu, nikachukua kadaftari nikaandika yote kabla sijasahau.

Ikafika kipindi cha kufanya mtihani sina ID valid ya kuonesha nimemaliza ada ili nifanye mtihani(kumbuka hapo ni kipindi cha kufanya supplementary kwahyo utaratibu ni tofauti na sikuwa nafaham nlifika usiku alafu asubuhi nna mtihani). Nikatolewa nifuate utaratibu nipate barua kutoka department yangu ili niendelee na mtihani, nafika kwa Head of Dp kanipa kimemo cha kumalizia ule mtiani ili nisichelewe then nirudi baadae kuchukua kibali cha jumla. Nilivyorudi niligongwa maswali nikayapangua yote prof akaniambia kama ni uongo basi ulijipanga maana file lako ninalo nilikuwa nangoja ujichanganye. Sikuona haja ya yeye kufanya vile basi tu ukiwa mwanafunzi ni kujibu kila unachoulizwa.
 
Sawa uongo haufai Ila madogo walikuwa na haki ya kukata rufaa kwa sababu hawakutakiwa kupewa test completely out of topic.

Course ni Semantics and Phonetics; unaniuliza habari za matairi wapi na wapi. Kosa la uongo lilitakiwa litritiwe kivyake Ila wapewe haki yao ya mtihani sahihi.
 
Sawa uongo haufai Ila madogo walikuwa na haki ya kukata rufaa kwa sababu hawakutakiwa kupewa test completely out of topic.

Course ni Semantics and Phonetics; unaniuliza habari za matairi wapi na wapi. Kosa la uongo lilitakiwa litritiwe kivyake Ila wapewe haki yao ya mtihani sahihi.
Mwamba (Dean) alitake personal
 
Back
Top Bottom