Ukiahidi ndoa ukapotea una haki ya kushitakiwa

Ukiahidi ndoa ukapotea una haki ya kushitakiwa

aleesha

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
835
Reaction score
1,215
Usipojua haki zako unaweza kuuziwa chochote kilicho chini ya kiwango na usiwe na cha kufanya au usipojua wajibu wako unaweza ukalazimishwa kutimiza zaidi ya unavyopaswa.
Huwezi kufika mahali ambapo hupajui kwa kupaona au kwa maelekezo na hakuna ubishi kwamba huwezi kudai haki ambayo huijui.
Ndio maana zipo sababu za msingi kwa mfanyabiashara kutambua haki na wajibu wake kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 haki za mfanyabiashara aliye kwenye ndoa au anatayerajia kuingia na anawajibika vipi kwa mujibu wake.
Sheria hiyo imeainisha haki za kumiliki mali kwa kila mwanandoa iwe pamoja au binafsi, kupewa cheti cha ndoa na kukataa au kukubali kuolewa. Kila mtu anayo hiyari ya kufunga ndoa na si kulazimishwa. Upo usawa kwa wanawake wote endapo ndoa ni ya zaidi ya mke mmoja.
Kwa walio kwenye ndoa, sheria inatoa haki ya kutowajibika kwa madeni ya mwenza wako yaliyokuwepo kabla ya kufunga ndoa. Mke anapewa haki ya kutumia fedha, mali za mumewe au kukopa kwa kutumia jina la mumewe kwa lengo la kujipatia mahitaji yake muhimu pamoja na ya watoto.
Endapo itathibitika wanandoa hawataweza kuishi tena pamoja kama mke na mume sheria inaruhusu kutengana au kuvunjwa kwa ndoa husika.
Kuoa au kuolewa tena baada talaka ya ndoa ya kwanza kutoka serikalini au mamlaka nyingine zinazotambulika kisheria na kutopigwa au kupewa adhabu ya aina yoyote.
Mke anayo haki ya kukaa na watoto walio chini ya miaka saba endapo wanandoa wametengana au kutalikiana. Mjane kuishi mahali popote atakapo, kuoa au kuolewa na mtu yeyote wa chaguo lake au kukaa bila kuolewa baada ya mwenzi wake kufariki.
Kumchukulia hatua za kisheria mtu aliyetoa ahadi ya kukuoa au kuolewa naye lakini akaivunja ahadi hiyo kwa sababu isiyo halali. Kudai mali, mahali au zawadi yoyote iliyotolewa kwa lengo la kufunga ndoa endapo itathibitika kuwa haitaweza kufungwa tena kutokana na sababu mbalimbali.
Unayo haki kumchukulia hatua mtu aliyethibika kuzini na mume au mke wako au kumshawishi au kumsababisha mume au mke wako kuondoka nyumbani na kuitelekeza familia yake.
Kama unazo sababu unaweza kuweka pingamizi la kutofungwa kwa ndoa iliyotangazwa na unaweza kuchagua kufunga ndoa ya kiserikali, kimila, kiislamu au kikristo. Ukiwa nje unaweza kufunga ndoa katika ofisi za ubalozi wa Tanzania.
Sheria inawataka wanandoa kufanya tendo la ndoa kikamilifu mara tu baada ya kufunga ndoa, mume kumtunza mke kwa chakula, malazi, mavazi na mahitaji mengine muhimu na mke kumtunza mume kama hajiwezi kutokana na matatizo ya afya, akili au ulemavu ikiwa ana uwezo wa kufanya hivyo.
Kumbuka, ndoa haitakiwi ifungwe kisirisiri na huruhusiwi kuuza au kufanya matumizi ya mali za familia bila ridhaa ya mwenza wako na unawajibika kwa mwenza wako kwa uzembe au hasara utakayoisababisha.
Mume au mke hawajibiki kwa uzembe au hasara iliyofanywa na mmoja wao kwa mtu mwingine. Huruhusiwi kuoa au kuolewa tena ikiwa umeshafunga ndoa na mtu mwingine kama ndoa yako ni ya mke au mume mmoja na haijavunjika.
Kila ndoa inayofungwa lazima iwe na mashahidi wawili au zaidi. Ikumbukwe kwamba haki hizi huwezi kuzipata ikiwa huzitambui na ifahamike pia kutokujua sheria si kinga ya kukufanya usiwajibishwe kisheria pindi itakapohitajika kufanya hivyo kutokana na suala litakalokuwapo mezani kwa wakati husika.
 
Sjui tutawachukulia hatua wangapi, najaribu kuwaza tu huko mahabusu kutajaa
 
lakini ni lazima anaye claim fidia ya breach of promise to marry athibitishe kwamba kuna madhara kayapata, iwe gharama alizotumia katika kupalilia uchumba akiamini ndoa ipo njiani kuja. kama kwa kukimbiwa tu hakuna madhara aliyopata basi hawezi pewa fidia. na hayo madhara yawe halisia sio eti kanisababishia msongo wa mawazo nk.
 
Back
Top Bottom