Ukiachika jua umejiacha mwenyewe!.

Ukiachika jua umejiacha mwenyewe!.

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
5,186
Reaction score
5,455
Wimbi la wanaoolewa na kuachika linaongezeka kila siku. Ukiwauliza wanawake wanatoa majibu kuwa wanaume ni wakorofi na wenye tamaa.

Wakati huo huo ukiwauliza wanaume nao wanadai wanawake wamekuwa na tamaa.
Hizi zinaweza kuwa sababu kadhaa za ndoa nyingi kuwa sawa ama kuvunjika, unapoingia ktk mahusiano ni jambo moja tu linalokufanya umuoe ama uolewe na mtu fulani si mambo mengi.

Jambo hilo likiwa na misingi imara basi ndoa yako itadumu.
Ktk kuuliza uliza watu waliooa na kuolewa nilipata majibu yafuatayo
1.Mimi nilimuoa mke wangu kwa sababu napenda wanawake wembamba.

2.Nilimuoa huyu mke kwasababu napenda wanawake wanene.
3.Nilimpendea huyu mke sauti yake yaani nampenda kwa hilo tu.
4.Nilimpenda kwa kuwa ni mtumishi wa serikali nilijua kila wakati atakuwa na pesa.
5.Nilimpenda kwa sababu ni msafi mno alinivutia kwa hilo tu.
6.Nilipomaliza masomo nilikuta walishanioea kwa hiyo tukaendelea kuishi na mila zetu kuoewa mke ni kawaida tu.
7.Nilimpenda kwa kuwa ni mchapa kazi.
8.Nidhamu yake tu ilinimaliza hadi nikaamua kutangaza ndoa.
9.Nilikuwa sina kwa kukaa sasa maisha magumu huyu dada akawa anataka tuishi wote kama mme na mke nami kutokana na ugumu wa maisha nikakubali.

10.Nilishinikizwa na mchungaji ila ukweli sikutaka kumuoa huyu.
12.Nilimuoa huyu dada mtumishi wa serikali ili akikopa hela anisaidie mtaji.

Ukiangalia hayo juu utagundua kuna vitu vinawafanya watu waoane na hakika haviwezi kupotea mfano nidhamu, uchapakazi na mengineyo.

Lakini wewe uliyempenda mkeo kisa mnene akija kwako akakuta maisha magumu ina maana mtaachana tu halikadhalika mwembamba akinenepa lazima mtaachana tu.
Wale ambao hamjaingia kwenye ndoa angalieni misingi ya vitu vinavyowaunganisha ikiwa ni vya kudumu au la ili kuweka msingi imara wa ndoa zenu .

Ukijikuta mmeachana na mkeo mmeo basi chanzo ni nyinyi wenyewe mmoja kati yenu kiunganishi kimepotea kutokana na kuwa na msingi mbovu.
Nawatakia maandalizi mema ya Christmas na mwaka mpya .
 
Marriage is among the complex institute in the world ever!!
Hizi ulizotaja haziwezi kwa namna yoyote kusolve tatizo la ndoa kuvurugika.
Hata SMS tu inatosha kuvuruga kabisa ndoa
 
Ndugu /mkuu hizo sababu ulizo-ziorodhesha zilipelekea watu kuoana.
Ila sababu za watu kuachana ni tofauti kabisa na hazina uhusiano na hizo (hapo juu). Kwa maana hiyo mnaweza "kuachana" tena kwa "taraka" wakati hizo sababu (hapo juu) zikiwa bado bora kabisa.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea watu kuachana:-
1.kumuacha unaye mpenda ili kuridhisha matakwa ya ndugu/marafiki/wafanyakazi wenzako wanafiki (bila wewe kuwatambua kiundani kuwa wanakuonea wivu) hapa wanaweza kukujaza upepo kwa maneno/ matendo ya kejeli au kinyume chake kama;- A. "wewe mbona mjanja hivi umeoaje MTU asiyesoma!?"

B."Dada yangu wewe mbona mzuri tu umekubaliji kuolewa na mbulula asiye na mbele wala nyuma! Achika mwaya uolewe na mwanaume mwenye pesa zake" huyo anakuzeesha tu.
---------watu wengi hapa wameangukia pua kwa kushindwa kurudiana kwa hao ndugu wanafiki kutoruhusu tena wawili hao kuweza kukaa meza moja kupatana hivyo kila mmoja kuugulia kivyake "moyoni" huko alipo.

2.Kiburi cha asili (hasa wasichana)--hapa napo ni mtihani mkubwa hasa vijana kushindwa kumhandle mke "kisaikolojia" bila ugomvi wa Mara kwa Mara.
3.ujuaji mwingi pande zote mbili bila kupeana nafasi ya kutoa mawazo/ushauri--hii hupelekea kupigana makofi hata mbele za watu/wageni.


Ndugu zangu yapo mengi nisiwachoshe!
 
Tamaa ya mwanamme isiyo epukika ni kule kutaka kumwaga mbegu kwa kila mdada na si vinginevyo...yaani tuko kama vile nzi ila wengine wamezidi kwani wanachapa hata kuku wakizidiwa. Mwanamke yeye tamaa yake ni pesa, kujionyesha kwa wenzake, kutaka ama kutamani kuchapwa na kila mwanamme amuonaye. Kingine, mwanamke anapenda sana kuonana na jamaa aliyemtupa siku za nyuma ili tu amuonyeshe kuwa sasa kapata na kama lijamaa likitaka kutongoza huyo mwanamke, basi mwanamke anajitahidi kila namna ili amkomoe jamaa akajisifie huko mbeleni kwa wenziwe. Ndoa nyingi uvunjika mara tu jamaa akishagundua kuwa mkewe ni msaliti, hii haina mjadala hata kidogo.
 
Ndugu /mkuu hizo sababu ulizo-ziorodhesha zilipelekea watu kuoana.
Ila sababu za watu kuachana ni tofauti kabisa na hazina uhusiano na hizo (hapo juu). Kwa maana hiyo mnaweza "kuachana" tena kwa "taraka" wakati hizo sababu (hapo juu) zikiwa bado bora kabisa.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea watu kuachana:-
1.kumuacha unaye mpenda ili kuridhisha matakwa ya ndugu/marafiki/wafanyakazi wenzako wanafiki (bila wewe kuwatambua kiundani kuwa wanakuonea wivu) hapa wanaweza kukujaza upepo kwa maneno/ matendo ya kejeli au kinyume chake kama;- A. "wewe mbona mjanja hivi umeoaje MTU asiyesoma!?"

B."Dada yangu wewe mbona mzuri tu umekubaliji kuolewa na mbulula asiye na mbele wala nyuma! Achika mwaya uolewe na mwanaume mwenye pesa zake" huyo anakuzeesha tu.
---------watu wengi hapa wameangukia pua kwa kushindwa kurudiana kwa hao ndugu wanafiki kutoruhusu tena wawili hao kuweza kukaa meza moja kupatana hivyo kila mmoja kuugulia kivyake "moyoni" huko alipo.

2.Kiburi cha asili (hasa wasichana)--hapa napo ni mtihani mkubwa hasa vijana kushindwa kumhandle mke "kisaikolojia" bila ugomvi wa Mara kwa Mara.
3.ujuaji mwingi pande zote mbili bila kupeana nafasi ya kutoa mawazo/ushauri--hii hupelekea kupigana makofi hata mbele za watu/wageni.


Ndugu zangu yapo mengi nisiwachoshe!
Naungana na wewe, lakini pia wewe uliyetii hayo uliyoambiwa still utakuwa chanzo.
Lengo kuu ni kutaka tupate visababishi vikuu vinavyosababisha mpasuko wa ndoa.
Asante kwa mawazo mazuri.
 
Wimbi la wanaoolewa na kuachika linaongezeka kila siku. Ukiwauliza wanawake wanatoa majibu kuwa wanaume ni wakorofi na wenye tamaa.

Wakati huo huo ukiwauliza wanaume nao wanadai wanawake wamekuwa na tamaa.
Hizi zinaweza kuwa sababu kadhaa za ndoa nyingi kuwa sawa ama kuvunjika, unapoingia ktk mahusiano ni jambo moja tu linalokufanya umuoe ama uolewe na mtu fulani si mambo mengi.

Jambo hilo likiwa na misingi imara basi ndoa yako itadumu.
Ktk kuuliza uliza watu waliooa na kuolewa nilipata majibu yafuatayo
1.Mimi nilimuoa mke wangu kwa sababu napenda wanawake wembamba.

2.Nilimuoa huyu mke kwasababu napenda wanawake wanene.
3.Nilimpendea huyu mke sauti yake yaani nampenda kwa hilo tu.
4.Nilimpenda kwa kuwa ni mtumishi wa serikali nilijua kila wakati atakuwa na pesa.
5.Nilimpenda kwa sababu ni msafi mno alinivutia kwa hilo tu.
6.Nilipomaliza masomo nilikuta walishanioea kwa hiyo tukaendelea kuishi na mila zetu kuoewa mke ni kawaida tu.
7.Nilimpenda kwa kuwa ni mchapa kazi.
8.Nidhamu yake tu ilinimaliza hadi nikaamua kutangaza ndoa.
9.Nilikuwa sina kwa kukaa sasa maisha magumu huyu dada akawa anataka tuishi wote kama mme na mke nami kutokana na ugumu wa maisha nikakubali.

10.Nilishinikizwa na mchungaji ila ukweli sikutaka kumuoa huyu.
12.Nilimuoa huyu dada mtumishi wa serikali ili akikopa hela anisaidie mtaji.

Ukiangalia hayo juu utagundua kuna vitu vinawafanya watu waoane na hakika haviwezi kupotea mfano nidhamu, uchapakazi na mengineyo.

Lakini wewe uliyempenda mkeo kisa mnene akija kwako akakuta maisha magumu ina maana mtaachana tu halikadhalika mwembamba akinenepa lazima mtaachana tu.
Wale ambao hamjaingia kwenye ndoa angalieni misingi ya vitu vinavyowaunganisha ikiwa ni vya kudumu au la ili kuweka msingi imara wa ndoa zenu .

Ukijikuta mmeachana na mkeo mmeo basi chanzo ni nyinyi wenyewe mmoja kati yenu kiunganishi kimepotea kutokana na kuwa na msingi mbovu.
Nawatakia maandalizi mema ya Christmas na mwaka mpya .
raha ya ngoma uingie kati ucheze sio umefunga kibwebwe umekaa pembeni unaangalia wenzio.na pili pili usiyoila huwezi jua inawashajeee .........nimekomea hapo
 
Back
Top Bottom