Ukerewe watu wanakwepa kodi kwa kushirikiana na Maafisa biashara

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
3,871
8,381
Moja kwa moja kwenye mada.

Huku Ukerewe kuna kasumba ya watu wa TRA kupita kwenye maduka kukagua wafanya biashara kama wameshalipia mapato na kama wana leseni ya biashara. Cha ajabu, kuna maduka hawajawahi kulipa kodi wala leseni ya biashara na maafisa mapato (TRA) na watu wa leseni wakifika pale wanawapita tu, wala hata hawaulizi wala kudai kodi kisa wenye maduka ni watumishi wa serikali, lakini sisi walala hoi tunalipa kodi na tuna leseni kabisa lakini watumishi hawalipi kodi.

Rais Magufuli, huku Ukerewe watumishi wako wa TRA na leseni wanawakwepesha wafanya biashara kulipa kodi kwa kuwa ni watumishi wa serikali, sasa sijui ni kuwaogopa au kubebana!

(MKITAKA USHAHIDI NAWAPA)

Goite
 
Back
Top Bottom