Ukerewe: Wanaokataza abiria kupanda vivuko Ukara Bugolora kukiona

Ukerewe: Wanaokataza abiria kupanda vivuko Ukara Bugolora kukiona

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,197
Reaction score
64,641
JESHI la Polisi wilayani Ukerewe limepiga marufuku mtu yeyote kujihusisha na kusafirisha abiria kutoka kisiwa cha Ukara na kijiji cha Bugorora.

Limesema shughuli hiyo itafanywa na vivuko mbadala vilivyowekwa na serikali.



Mkuu wa Polisi wilayani Ukerewe, Iginas Kapira, alipiga marufuku hiyo wakati akizungumza na wananchi wa kisiwa cha Ukara waliogoma kupanda vivuko vya MV Sabasaba na MV Ukara, katika mkutano wa hadhara.



"Hapa tulipofikia tutaanza kushurutishana maana tumeongea kistaarabu tumeonekana wajinga, narudia kwa mara nyingine anayetaka kusikiliza asikilize, asiyetaka aondoke kimya kimya, maelekezo yameshatolewa, vivuko kuanzia sasa hivi vinaanza kufanya kazi atakayetaka kupanda apande asiyetaka aache, sharti ni moja ole wake atokee mtu amzuie mwingine kupanda sisi tutashughulika naye hilo ni tamko la dola," alisema Kapira.



Aidha, Kapira alisema ni marufuku mtu kupanda mtumbwi bila kibali kutoka kwao na atakayefanya hivyo atawaambia kautoa wapi na ni nani kamruhusu, yeye na abiria wote watachukulia hatua.



"Serikali haiwezi kuwawekea vyombo vya usafiri halafu nyie mnafanya mambo ya ajabu haiwezekani, mnajua jitihada za serikali inazo zifanya za kuwajengea kivuko kipya, mjue meli haiwezi kujengwa kwa muda wa miezi miwili au mitatu, sasa mimi kama msimazi wa sheria nimetoa maelekezo na hayo ni ya kiutendaji siyo kisiasa tena…tutakula nao sahani moja," alisema Kapira.



Mkutano huo wa hadhara ulifanyika mbele ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo chini ya Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Focus Majumbi, kwenye viwanja vya Ofisi ya Ofisa Mtendaji wa Kata ya Bwisya baada ya wananchi hao kufanya mkutano Oktoba 8, mwaka huu katika eneo la Bwisya, uliokuwa na maazimio ya pamoja ya kutotumia vivuko hivyo.



Mwenyekiti wa kijiji cha Bwisya, Oru Magero, alisema vivuko binafsi vilivyofungiwa kutoa huduma ya usafiri ni kati ya kisiwa cha Ukara na maeneo mengine ya Wilaya ya Ukerewe ambayo ni Katende kupitia Sizu kwenda Buguza, Bukungu kwenda Lubaga, Chifule kwenda Kakukuru na cha kutoka Kome kwenda Buguza.



"Hatua ya Jeshi la Polisi kuvifungia vivuko hivyo ni kitendo cha uonevu, kutokana na majanga haya serikali ilileta vivuko viwili vya MV Sabasaba na Ukara, lakini wananchi wamevikataa kutokana na kuvifahamu hususani MV Ukara ni kibovu na kimezibwa na saruji na Oktoba 7, mwaka huu MV Ukara ilizimika majini ndio maana watu wanahofia,"alisema Magero.



Katika kijiji cha Bwisya, baadhi ya wananchi walidai kuwa wanataka watafutiwe kivuko kingine maana mmiliki wa MV Nyehunge alikubali kuleta kivuko kwa gharama ya Sh. 2,000 na wananchi walikubali kulipia fedha hiyo.



"Sisi hatuwezi kutumia vivuko hivi ingawa serikali inatulazimisha, nadhani wao hawahofii usalama wetu wanaona vyombo hivyo viko salama tunaopanda ni watu, basi watuache tutumie vivuko vyetu vya asili, hadi hapo Rais atakapomalizia ujenzi wa kivuko kingine cha tani 50 na chenye uwezo wa kubeba abiria 300 kitakapokamilika," alisema Maria Leonard, mkazi wa Bwisya.

Chanzo: Nipashe
 
Hivi wanaopanda daladala binafsi pale kimara na kuacha kupanda mwendokasi mbona hawalazimishwi
 
Back
Top Bottom