UKAWA yaanza kutoa huduma za afya bure jijini Dar es Salaam

UKAWA yaanza kutoa huduma za afya bure jijini Dar es Salaam

SIMU YA TOCHI

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2014
Posts
1,385
Reaction score
894
Ile kauli ya mabadiliko sasa imeanza kuonekana kwa vitendo ambapo tangu UKAWA ishinde na kuongoza jiji la Dar, sasa wakazi wa Dar watanufaika na huduma mpya ya TIKA(TIBA KWA KADI) ambayo huduma hii itawahusu wakazi wote wenye ajira na wasio na ajira (mama lishe, vijana mtaani, boda boda ) n.k. Zoezi hili limeanza leo ambapo utalipia elfu arobaini kwa mtu mmoja mmoja na kukabidhiwa kadi ambayo itakufanya upate huduma ya afya kwa mwaka mzima bure.

Kadi hii inakupa fursa zifuatazo;
1.Huduma za Ultra sound na X- Ray kwa mwaka mzima na mara nyingi utavyojisikia bila kudaiwa pesa yoyote
2.Vipimo vyote vya Malaria, Typhoid, kichocho, UTI
3.Huduma za upasuaji wa aina zote
4.Tiba ya T.B
5.Ambulance kumfuata mgonjwa wako sehemu yoyote alipo bila gharama yoyote mpaka sasa zipo ambulance zaidi ya ishirini kwaajili ya hili.

Wakazi wa Dar changamkia fursa hii ya huduma bora ya afya chini ya UKAWA.
 
263917.jpg
 
Ile kauli ya mabadiliko sasa imeanza kuonekana kwa vitendo ambapo tangu UKAWA ishinde na kuongoza jiji la Dar, sasa wakazi wa Dar watanufaika na huduma mpya ya TIKA ambayo huduma hii itawahusu wakazi wote wenye ajira na wasio na ajira (mama lishe, vijana mtaani, boda boda ) n.k. Zoezi hili limeanza leo ambapo utalipia elfu arobaini kwa mtu mmoja mmoja na kukabidhiwa kadi ambayo itakufanya upate huduma ya afya kwa mwaka mzima bure.

Kadi hii inakupa fursa zifuatazo;
1.Huduma za Ultra sound na X- Ray kwa mwaka mzima na mara nyingi utavyojisikia bila kudaiwa pesa yoyote
2.Vipimo vyote vya Malaria, Typhoid, kichocho, UTI
3.Tiba ya T.B
4.Ambulance kumfuata mgonjwa wako sehemu yoyote alipo bila gharama yoyote mpaka sasa zipo ambulance zaidi ya ishirini kwaajili ya hili.

Wakazi wa Dar changamkia fursa hii ya huduma bora ya afya chini ya UKAWA.
Nini maana ya Bure! Ina maana hata kuongea na simu ni bure kwa sababu unalipia vocha then unajiunga na kifurushi? Rekebisha sio bure bali ni utaratibu mzuri tu wa utoaji huduma kwani ugonjwa hauna miadi.
 
Sasa hapo kwenye bima ya afaya UKAWA wanahusikaje? Hiyo si ni mipango ya Mhe Rais! Acheni kupumbaza watu.

Umesoma habari au umekurupuka?bima ni kwa wafanyakazi lakini hii ya Ukawa ni TIKA ambayo yenyewe inawagusa wasio na ajira na wenye ajira.
 
Ile kauli ya mabadiliko sasa imeanza kuonekana kwa vitendo ambapo tangu UKAWA ishinde na kuongoza jiji la Dar, sasa wakazi wa Dar watanufaika na huduma mpya ya TIKA ambayo huduma hii itawahusu wakazi wote wenye ajira na wasio na ajira (mama lishe, vijana mtaani, boda boda ) n.k. Zoezi hili limeanza leo ambapo utalipia elfu arobaini kwa mtu mmoja mmoja na kukabidhiwa kadi ambayo itakufanya upate huduma ya afya kwa mwaka mzima bure.

Kadi hii inakupa fursa zifuatazo;
1.Huduma za Ultra sound na X- Ray kwa mwaka mzima na mara nyingi utavyojisikia bila kudaiwa pesa yoyote
2.Vipimo vyote vya Malaria, Typhoid, kichocho, UTI
3.Tiba ya T.B
4.Ambulance kumfuata mgonjwa wako sehemu yoyote alipo bila gharama yoyote mpaka sasa zipo ambulance zaidi ya ishirini kwaajili ya hili.

Wakazi wa Dar changamkia fursa hii ya huduma bora ya afya chini ya UKAWA.

Hapana, hiyo si huduma mpya, huku kwetu mkoa wa Pwani "Tiba kwa Kadi" (TIKA) tunayo kwa takriban miaka miwili au zaidi kidogo sasa.

Ilianzishwa wakati Mwantum Mahiza alikuwa mkuu wa mkoa kwa ubunifu wa Jakaya Kikwete, enzi alipoeneza vituo vya afya kata zote.
 
huo utaratibu sio mpya.

mbona upo tz nzima kupitia mpango wa CHF.

ingekuwa huduma bure, hiyo elf 40 inalipwa ya nn?

Sehemu gani nyingine tanzania wanapotoa huduma ya TIKA?
Huu utaratibu ni kuwahudumia wakazi wote wenye ajira na wasio na ajira serikali wao walibase kwa wenye ajira kwa kutumia bima huku ikiwasahau maskini wasio na ajira na kipato ila UKAWA imeliona hilo na kulifanyia kazi.
 
Kwa kujifariji na matumaini hamjambo!! Hiyo no 3 na 4 mbona hakuna mgonjwa anayechajiwa? Na hiyo 1 na 2 bure ipo wapi hapo kama kuna elfu 40? Tekenyaaaaa... Chekaaaa....
Hivi ukiwa na shilingi elfu 40 unaweza kupata hizo huduma zote ndani ya mwaka mzima .Msiwe wafia chama hata kwenye jambo la haki . Hiyo gharama ni sawa na bure tu na hapo ndio unapoona nani hasa anaurafiki na masikini sio kuomba uombewe wakati unatutia kwenye gharama kubwa za maisha.
 
Back
Top Bottom