UKAWA yaaibika Dodoma

UKAWA yaaibika Dodoma

47pro

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2015
Posts
1,204
Reaction score
333
Aliyekuwa mgombea Urais wa CCM ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Januari Makamba, jana alimshukia mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA, Edward Lowassa kwamba ni mroho wa madaraka.

Makamba alitoa kauli hiyo katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma wakati akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde. January alisema kuwa Lowassa ameivuruga demokrasia ndani ya Chadema na kupeleka mizengwe itakayokiua chama hicho na umoja wao.

Yale siyo mabadiliko kama wanavyojinadi bali ni uroho wa madaraka kwa mtu mwenye uroho na chama chenye uroho, lakini hawezi na hawawezi kushika madaraka ya kuongoza nchi, alisema Makamba.

Alisema kinachoendelea kwa vyama vinavyounda Ukawa ni maigizo na siyo mabadiliko ya kweli kwa sababu mgombea urais ametoka CCM na Sera za CCM na mgombea mwenza ametoka CUF na sera za huko, hivyo hawawezi kuungana kwa pamoja kwa sababu hawajui nini maana ya kile wanachogombea.

Hata hivyo, Makamba alikiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu kuliko uchaguzi wowote uliowahi kutokea katika mfumo wa vyama vingi na akawataka wana CCM kujiandaa kikamilifu.

Alisema CCM kinapaswa kuwa makini na imara wakati wote ili kutoyumba na wakifanya hivyo watajikuta wanapata mchanganyiko ambao utaleta shida katika maendeleo.

Kwa upande wake mgombea ubunge Mavunde alijipachika jina la Mr Makao akisema lazima ataipelekea Dodoma
hadhi ya kweli katika kufikia makao ambayo yamekuwa yakisemwa kama hisani.

Mavunde aliomba wananchi kumwamini na kumpa nafasi hiyo kwani ana uhakika kwa miaka mitano ataifanya Dodoma kupaa kiuchumi huku akisema atashughulika na watu wenye kipato cha chini pamoja na kumaliza migogoro ya ardhi.
 
Kama ni uroho wa madaraka kwanini yeye januanry aligombea uraisi? Kwanini aliwawekea mapingamizi wengine, si angeacha na kupambana na wapinzani wake kwenye sanduku la kura
 
Watu wanaendelea kusonga mbele na silaha za sumu, hakika mwaka huu, hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe jingine kabla ukombozi haujafika!
 
Magufuli asipige kampeni bac mana naye ni mroho wa madaraka....pia akupende hakuna mwanasiasa acye penda madaraka
 
  • Thanks
Reactions: rr3
Yeye alipo omba ridhaa ya chama kumteua alitaka nini??aache kutuhadaa lowasa katikisa chama hata mkwere analifahamu hilo😛😱
 
  • Thanks
Reactions: rr3
ha ha haha mpika majungu ccm naona sasa kaishiwa vikorombezwo
 
kama yeye January si mroho wa madaraka ajitoe kwenye mbio za ubunge.Miaka mitano aliyowakilisha wananchi imemtosha
 
Huyo ni wa kupuuzwa yeye hataki ushindani halafu anaita wenzie waroho.
Magufuli Oyeee. Hata sisi UKAWA tunamkubali bali Mzee Lowassa tunamzuga ili tule hela yake anayoturudishia kiaina. Upo hapo
 
Uroho na tamaa ndio ubinadamu hai.ikifikia roho itaki chochote na mwili au tamanii chochote Mara nyingi ni kwa mgonjwa alie karibia kukata roho.hivyo sioni kosa la Lawosa kkutaka toka rohoni kuwa raisi.
 
Kama ni maigizo anamnadi wa nini huyo mgombea!? Si asubiri hayo maigizo na mgombea wake hapo October 25.
 
kama yeye January si mroho wa madaraka ajitoe kwenye mbio za ubunge.Miaka mitano aliyowakilisha wananchi imemtosha

JM hajijui na wala hajui kuwa mambo yake tunayafahamu sana ila tumekaa kimya
 
mimi huwa nashangaa hawa wanasiasa uchwara sasa yeye amewekea wenzake mapingamizi kwa uoga wa kushindwa hiyo pia ni tamaa ya madaraka
 
Sipendi kuweka ushahidi wa namna ninavyojua JM,

Kwanza alishaambiwa kuwa hatuongozwi na mnyoa unga! sasa leo unadhani wale waliomwambia hivyo si wanafahamu udhaifu wake?
 
Back
Top Bottom