Ukawa wekeni hili wazi

Ukawa wekeni hili wazi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,706
Reaction score
57,202
Habari ndugu,
Maada hi ilipaswa iwe jukwaa la inteligensia lakini naomba mods muiache hapa watakaoelewa na waelewe..na
Ili kunielewa mada yangu naomba usilete ushabiki u ccm na u chadema uweke kando kuwa kama mtu mwenye fikra huru..mwanzo nilijua kifungo kibaya kwa mwanadamu ni dini pekee ipo kwa ajili ya wachache kunufaika uwongo mwing ndani yake,nisigusie sana kuhusu dini ili kuepusha kuchokoza watu kiimani
Kifungo cha pili alichoweza kufungwa binadamu ni siasa...tumefanywa mitaji na binadamu wenzetu hivi vyama vinaendeshwa na watu kama sisi na tunajua watu tuna sifa za unafki,tamaa,uwongo kama wewe usivo na huruma na wengne basi tambua hata huyo unayemwona mchapakazi au mkombozi vile vile ni binadamu na anajionea huruma yeye kuliko anavyokuonea wewe
unajua siasa ina mambo mengi wananchi sasa hivi hatufanyi reasoning tumeishia kutumika kama mitaji ya wanasiasa
Leo hii tunawashabikia viongozi wa ccm au wa ukawa tunajifanya hatuoni kama wenyewe wako pale/watakuwepo kwa ajili ya maisha yao,familia zao na koo zao..tupo kama misukule
Inauma sana great thinker amefanywa kama mtumwa chini ya tajiri lowasa au mbowe tunajifanya hatuoni kama wale wanapesa/wanataka pesa kama kweli wangekuwa na nia na huruma na wananch kwanini wasituambia sera zao wazi ni lini rasilimali zetu zitakuwa chini ya serikali watakayounda,tumeishia kuwashabikia.ndugu zangu wale hawana uzalendo
Ukirudi kwa upande wa ccm ndo matatizo matupu najuta kuzaliwa tanzania nchi hi wanafaidika wachache kama kweli kina kikwete na magufuli wangekuwa na huruma wangewezaje kuwatazama maskini wa kutupwa vijijini ilihali hata mlo hawapati..tunaona tumeletewa maendeleo kumbe ndo wananufaika wenyewe mfano eti mtu anaisifia serikali ya ccm imemsaidia yeye sasa iv ana smartphone hajiulizi kama amenunua hvo amenufaisha mtengenezaji na mtengenezaji naye kamuwezesha mwanasiasa kisha anaekewa mifumo inayomkinda..siasa bwana unafurahia serikali ya ccm eti imejenga barabara unasahau kama ni kwa pesa zako unasahau pia kama hzo barabara ni kwa ajili ya kuwarahisishia kupitisha mizigo yao ambayo wanakuuzia tena kwa pesa yako
Tusidanganyane siasa ni mchezo unaocheza na akili ya binadamu,sisi ni watumwa tunashangilia maigizo ya binadamu wenzetu ambao hawatupi elimu ili tuendelee kuwa wapumbavu
Hakuna atakaye kuja kutukomboa only strong ndo wata survive wengne tutaendelea kulalamikiwa na vizazi vinavokuja kwa maamuzi tunayofanya sasa kwa ushabiki..watoto wetu watakuja kushangaa kwa nini tulisikiaga kuwa kuna watu walichota mabilion lakini hawaulizwa?watoto wetu watakuja kushangaa mmoja wapo wa anayesemakana fisadi anashangiliwa kwanini tunajisahaulisha mapema hivi?binadamu tuna tatizo gani?
Ccm mmetupoteza mpaka wasomi na watu wanajiita watakatifu(viongozi wadini)mme wanununua hivo hivo pia kwa upinzani mnadanganya mpaka ma great thinker humu ndani wanawashabikia..jibu ni kuwa na nyie mnadanganya na wazungu (wawekezaji) kwa kupewa uwongo kisha mnatapeliwa ,siasa mfumo wa kijinga sana mtu kweli unajikuta unamshabikia mwizi au yule ambaye sio mwizi unamwona hafai
Taifa hili linachekesha,viongozi wote wanachekesha,wananchi mnachekesha hivi mnadhani wale waarab wanavofanya vita kulinda rasilimali mnadhani wanakosea..walioiba mabilioni wanaonekana wazuri
UKAWA MMEONEKANA MNAWEZA KULETA MABADILIKO WANAYOTAKA WATU LAKINI JE MBONA KUNA MAMBO HAMUWEKI SAWA?NI KIVIPI MTAZUIA MAKAMPUNI KUMILIKI RASILIMAL ILA TAIFA NDO LIMILIKI KILA KITU AU NDO YATAKUWA KAMA CCM KUACHIA WATU WAVUNE MADINI?WAZUNGU WATU WABAYA SANA
Ukawa ningewaona wa maana kama mnge utangazia umma kuwa mkishka nchi rasilimal zitalindwa nyie mnasubiri mpaka siku ya kufungua kampeni ili mkusanye watu wengi lengo ni kuwa lipiza ccm?ETI LEO SIASA ZA TANZANIA ZINABEBWA NA MISAMIATI YA KITOTO MFANO KILA CHAMA KINATAKA KIPATE MAFURIKO siasa za majitaka sana
Embu jiulize kwani kampeni zikifunguliwa kwenye ukumbi mfano mlimani city hazitafunguka?
MY TAKE:NAJUA WENGI MTANIDHARAU KWAMBA NIMEANDIKA ULOFA LAKINI LAZIMA TUJUE KUWA SISI TUNASHABIKIA UTUMWA CHINI YA BINADAMU WENZETU KIPINDI TUNARUSHIANA VIJEMBE JUU YA VISIVYO NA UMUHIMU KULE WENGNE WANAKULA VIZURI WENGNE VBY
Nimejitoa rasmi kwenye ushabiki nataka niwe mtu huru kichwan nibaki na vitu vya msing vinavyonihusu mimi moja kwa moja
USHABIKI UNAKWENDA KUHARIBU TAIFA MTANIAMBIA
Waasalam
 
My dear Joh Mitazamo! A once great physicist ever lived, Albert Einstein said 'Politics is difficult than physics'. He did not lie, he was very correct. Most of us just talk about politics but we don't understand what it really is. Once you grasp just a glimpse of it, you will never complain at all! That's how it is, as long as you have a viable justification to anything!
I urge you to just watch from a distance, maybe you will get to understand it! Clean people accomplish nothing in politics anywhere on this planet! Politics everywhere and is part of every minute! So just brace yourself buddy!
 
Clean people accomplish nothing in politics. . . . . . . Unsheathed reality. . . .
 
Fact mkuu

Siasa mbovu za tanzania kuwah kushuhudiwa itakuwa ni uchaguzi huu.watu vichwani wamejaza madudu hawajiuliz sababu wanamuamini fulani ndo mkombozi akati huyo fulani ana zaid ya bilion kumi bank na anajua kuna binadamu mwenzake hata chakula hapati
 
Uchaguzi umefika ni lazima tuchague. Sasa tumchague yupi kati ya walioko mbele yetu? Huyu ambaye wenzake wanaomfahamu vizuri kuliko sisi wamemkataa kuwa ni mwizi, japo yeye anasema yeye na wao wote wezi? Au tumchague huyu ambaye wamemleta kuwa amaweza asiwaumbue kuwa waliiba.Hapo ndo mtihani, ukweli ni kwamba huyu mpya kwa vile ameona jinsi hali ilivyombaya halika atafanya kazi kama punda kutetea ugali wake. Lowasa anatafuta kinga ya kitoshitakiwa kama wenzake. Ndo maana binafsi naona Magufuli anatosha.
 
Hakuna aliye kuwa msafi, ila ccm tokea miaka ya 60 ambapo inamiaka Zaidi ya 50 ktk kushika dola lakini mabadiliko waliyo yaleta hayaridhoshi hivyo ni bora wakae pembeni tuwape na wengine tuone watafanya nn. Na hiwezi kusema ukawa hawawezi kuleta maendeleo au hawana uwezo wa kuongoza nchi kama hujawapa nafasi, so siasa huwezi kuiepuka ktk maisha ya kila siku.
 
Uchaguzi umefika ni lazima tuchague. Sasa tumchague yupi kati ya walioko mbele yetu? Huyu ambaye wenzake wanaomfahamu vizuri kuliko sisi wamemkataa kuwa ni mwizi, japo yeye anasema yeye na wao wote wezi? Au tumchague huyu ambaye wamemleta kuwa amaweza asiwaumbue kuwa waliiba.Hapo ndo mtihani, ukweli ni kwamba huyu mpya kwa vile ameona jinsi hali ilivyombaya halika atafanya kazi kama punda kutetea ugali wake. Lowasa anatafuta kinga ya kitoshitakiwa kama wenzake. Ndo maana binafsi naona Magufuli anatosha.

Nashukuru kwa kuwa unafanya reasoning,kwa mtizamo wako una chembe chembe za u great thinker sio kama wengine wanaoangalia sura
Watu wajinga sana wanawaonea huruma waizi wanaowajua je wale wengne ambao shutuma zao hazijavuma? Binafsi me kura yangu naieleleza ukawa lakini nikiwa na wasiwasi mkubwa unaochagizwa na shaka moyoni mwangu
 
Mkuu why ujipe shaka kwanini usipeleke kura yako kwa tinga tinga ambalo halina makundi pia ni mchapa kazi. huvi jiulize huyu mamvi akichukua nchi pesa zake arudishaje? bila shaka atachukua chake mapema. Mgufuli oyeeeeeeeeeeeeee...........
 
Kufikiri si jambo jepesi, kwani yahitaji akili utulivu ili kuweza kuchambua, na si wote tunapenda kushughulisha akili zetu. Asante kwa ujumbe wako, huwenda kwa wenye kujitambua wakapunguza ushabiki na kufanya maamuzi sahihi kwa mustakbali wa taifa letu.
 
Uchaguzi umefika ni lazima tuchague. Sasa tumchague yupi kati ya walioko mbele yetu? Huyu ambaye wenzake wanaomfahamu vizuri kuliko sisi wamemkataa kuwa ni mwizi, japo yeye anasema yeye na wao wote wezi? Au tumchague huyu ambaye wamemleta kuwa amaweza asiwaumbue kuwa waliiba.Hapo ndo mtihani, ukweli ni kwamba huyu mpya kwa vile ameona jinsi hali ilivyombaya halika atafanya kazi kama punda kutetea ugali wake. Lowasa anatafuta kinga ya kitoshitakiwa kama wenzake. Ndo maana binafsi naona Magufuli anatosha.

kwa kuyatetea yale majambazi yaliyoko ccm maghufuli atosha...
 
Mkuu why ujipe shaka kwanini usipeleke kura yako kwa tinga tinga ambalo halina makundi pia ni mchapa kazi. huvi jiulize huyu mamvi akichukua nchi pesa zake arudishaje? bila shaka atachukua chake mapema. Mgufuli oyeeeeeeeeeeeeee...........

Na huo ndo ushabiki upimbi ninaoukataa unamshangiliaje homo sapiens mwenzako?je mtu msafi na mchafu unawatofautishaje?
 
Mkuu why ujipe shaka kwanini usipeleke kura yako kwa tinga tinga ambalo halina makundi pia ni mchapa kazi. huvi jiulize huyu mamvi akichukua nchi pesa zake arudishaje? bila shaka atachukua chake mapema. Mgufuli oyeeeeeeeeeeeeee...........

maghufuli si tatizo. tatizo letu ni ccm. kwa mtazamo wangu lowasa atosha..
 
unachoongea ni sahihi kabisa ila ukiwaambia hivyo vijana wa ukawa wanakushushia mitusi. ukawa ina vijana wasomi lakini wenye hoja za kitoto ( kwa mitusi yao hatatapewa uongozi na wataendekea kuitwa Complete loafers)
 
unachoongea ni sahihi kabisa ila ukiwaambia hivyo vijana wa ukawa wanakushushia mitusi. ukawa ina vijana wasomi lakini wenye hoja za kitoto ( kwa mitusi yao hawatakuja kupewa uongozi wa nchi na wataendekea kuitwa Complete loafers)
 
Siasa mbovu za tanzania kuwah kushuhudiwa itakuwa ni uchaguzi huu.watu vichwani wamejaza madudu hawajiuliz sababu wanamuamini fulani ndo mkombozi akati huyo fulani ana zaid ya bilion kumi bank na anajua kuna binadamu mwenzake hata chakula hapati

kuwa na pesa sio tatizo. tatizo hao wanaopiga kampeni tuwachague je wana uwezo wa kuwasaidia watanzania?
 
Kufikiri si jambo jepesi, kwani yahitaji akili utulivu ili kuweza kuchambua, na si wote tunapenda kushughulisha akili zetu. Asante kwa ujumbe wako, huwenda kwa wenye kujitambua wakapunguza ushabiki na kufanya maamuzi sahihi kwa mustakbali wa taifa letu.

Nashukuru mkuu wewe ni mmoja wa watu wasioyumbishwa na matakwa ya homosapiens mwenzako..watu hawajiulizi vipi keki ya taifa itagawanywa sawa kwa hio miaka kumi ijayo,aidha ishinde ccm au ukawa lazima watu wahoji mgawanyo ulio sawa , jiulize kuna wananch vijijini hawana hata viatu je kina lowasa hawakuwepo madarakani je kina magufuli wamewah kufikiria kugawana mali zao na maskini
mimi hoja yangu ni kuwa tushiriki kwenye siasa kudai rasilimal zilindwe kwa nguvu zote

Ushabiki tulio nao sisi ni wa kijinga tunamshabikia mtu mwenye urafiki na kina chenge?
Viongoz wote wabaya tu,hawana nia ya dhati au hata kama wanayo wanawaonea huruma marafiki zao wafanyabiashara kuliko mpiga kura
MY TAKE:TUBADILIKE TUWAHOJI HAWA WANAOTAKA UONGOZI WANA MISIMAMO GANI NA RASILIMALI ZINAZOENDELEA KUPUNGUA
Tujenge utaifa japo tunampenda lowasa lakini pia tuthubutu kumuuliza atafanya nini kumilikisha migodi yote kwa serikali
 
unachoongea ni sahihi kabisa ila ukiwaambia hivyo vijana wa ukawa wanakushushia mitusi. ukawa ina vijana wasomi lakini wenye hoja za kitoto ( kwa mitusi yao hatatapewa uongozi na wataendekea kuitwa Complete loafers)

na wewe umeingia kwenye ushabiki uleule tu...
 
Mkuu why ujipe shaka kwanini usipeleke kura yako kwa tinga tinga ambalo halina makundi pia ni mchapa kazi. huvi jiulize huyu mamvi akichukua nchi pesa zake arudishaje? bila shaka atachukua chake mapema. Mgufuli oyeeeeeeeeeeeeee...........

Vizuri sana mkuu
 
Back
Top Bottom